Serikali yaongeza mshahara wa kima cha chini Sekta binafsi mpaka Tsh 358,322

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imetangaza kima cha chini cha mshahara wa sekta binafsi ambapo sasa itakuwa ni Sh358,322 kutoka Sh275,060 ikiwa ni ongezeko la asilimia 33.4.

Kima hicho kitaanza kutumika rasmi Januari Mosi mwaka 2026. Ikumbukwe Serikali ilipandisha kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma kwa asilimia 35.1 (kutoka Sh370,000 hadi Sh500,000), kwa lengo la kuimarisha ustawi kwa wafanyakazi.

Hilo likitangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Kitaifa (Mei Mosi) mkoani Singida katika viwanja vya Bombadia, Mei mwaka huu.

Akitangaza kima hicho cha sekta binafsi leo Ijumaa Oktoba 17, 2025 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhiwani Kikwete kuongezwa kwa kima cha mshahara ni takwa la kisheria.

Amesema tangazo la mara ya mwisho lilikuwa mwaka 2022 hivyo tangazo la leo mwaka 2025 imetimia miaka mitatu. Sheria inataka kila baada ya miaka mitatu kufanyike mapitio ya kima cha chini cha mshahara.

"Nitoe rai kwa waajiri wote wa sekta binafsi kuzingatia na kutekeleza kima hiki kipya cha mshahara kwa kuwa ni takwa la kisheria. Ofisi yangu haitasita kuchukua hatua kwa waajiri watakaokaidi au kushindwa kitekeleza amri hii kwa makusudi.

"Aidha ofisi yangu itaendelea kufatilia kwa karibu utekelezaji wa amri hii, kutoa elimu kwa waajiri na wafanyakazi pamoja na kufanya tathimini ya mara kwa mara ili kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika kikamilifu," amesema.

Chanzo: Mwananchi
IMG_2644.jpeg
 
Utapeli mtupu.
 
Kwanini wasiongezee watumishi wao mishahara? Kama huo uwezo wanao! Kazi kuwabana sekta binafsi ili wapate kodi zao tu...
 
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imetangaza kupandisha kima cha chini cha mshahara kwa sekta binafsi kutoka Shilingi 275,060 hadi Shilingi 358,322, ikiwa ni ongezeko la asilimia 33.4, hii ni kwa mujibu wa tovuti ya Mwananchi.

Akizungumza leo Ijumaa, Oktoba 17, 2025, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete, amesema kuwa ongezeko hilo kwa sekta binafsi ni utekelezaji wa matakwa ya kisheria.

Soma pia: Rasmi Walimu waingia kwenye kundi la wenye kima cha chini cha mshahara Tanzania

1760695360357.png

Kwa mujibu wa Waziri Ridhiwani, mapitio ya kima cha chini cha mshahara hufanyika kila baada ya miaka mitatu, ambapo tangazo la mwisho lilitolewa mwaka 2022.

Ameeleza kuwa Serikali inataka waajiri wote wa sekta binafsi kuhakikisha wanazingatia na kutekeleza kima hicho kipya cha mshahara kwa mujibu wa sheria.

Ameonya kuwa Ofisi yake haitasita kuchukua hatua kwa waajiri watakaokaidi au kushindwa kutekeleza agizo hilo kwa makusudi, akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kufuatilia kwa karibu utekelezaji wake.

“Aidha ofisi yangu itaendelea kufatilia kwa karibu utekelezaji wa amri hii, kutoa elimu kwa waajiri na wafanyakazi pamoja na kufanya tathimini ya mara kwa mara ili kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika kikamilifu," amesema.

Imeelezwa kuwa kima hicho kipya kitaanza kutumika rasmi Januari 1, 2026, ikiwa ni hatua ya kuimarisha ustawi wa wafanyakazi na kuleta uwiano na ongezeko la mishahara ya watumishi wa umma lililotangazwa awali.

Rais Samia Suluhu Hassan, katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) mwaka huu mkoani Singida, alitangaza kupandishwa kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma kwa asilimia 35.1 kutoka Shilingi 370,000 hadi Shilingi 500,000 kama sehemu ya juhudi za Serikali kuboresha maisha ya wafanyakazi nchini.
 
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imetangaza kima cha chini cha mshahara wa sekta binafsi ambapo sasa itakuwa ni Sh358,322 kutoka Sh275,060 ikiwa ni ongezeko la asilimia 33.4.

Kima hicho kitaanza kutumika rasmi Januari Mosi mwaka 2026. Ikumbukwe Serikali ilipandisha kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma kwa asilimia 35.1 (kutoka Sh370,000 hadi Sh500,000), kwa lengo la kuimarisha ustawi kwa wafanyakazi.

Hilo likitangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Kitaifa (Mei Mosi) mkoani Singida katika viwanja vya Bombadia, Mei mwaka huu.

Akitangaza kima hicho cha sekta binafsi leo Ijumaa Oktoba 17, 2025 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhiwani Kikwete kuongezwa kwa kima cha mshahara ni takwa la kisheria.

Amesema tangazo la mara ya mwisho lilikuwa mwaka 2022 hivyo tangazo la leo mwaka 2025 imetimia miaka mitatu. Sheria inataka kila baada ya miaka mitatu kufanyike mapitio ya kima cha chini cha mshahara.

"Nitoe rai kwa waajiri wote wa sekta binafsi kuzingatia na kutekeleza kima hiki kipya cha mshahara kwa kuwa ni takwa la kisheria. Ofisi yangu haitasita kuchukua hatua kwa waajiri watakaokaidi au kushindwa kitekeleza amri hii kwa makusudi.

"Aidha ofisi yangu itaendelea kufatilia kwa karibu utekelezaji wa amri hii, kutoa elimu kwa waajiri na wafanyakazi pamoja na kufanya tathimini ya mara kwa mara ili kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika kikamilifu," amesema.

Chanzo: MwananchiView attachment 3490188
Cc: JamiiCheck
 
Back
Top Bottom