Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 122,494
- 96,074
Ndiyo kuishiwa pumzi huko,sasa wanakimbizana na watoa matamko barabaraniWanaacha kuongea maswala ya msingi ya kimaendeleo, wao kila kitu ni kutoa onyo tu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndiyo kuishiwa pumzi huko,sasa wanakimbizana na watoa matamko barabaraniWanaacha kuongea maswala ya msingi ya kimaendeleo, wao kila kitu ni kutoa onyo tu
Kama taifa sijui wapi tunaelekeaAnazunguka sana, aseme tu kuwa kiongozi wa kiroho wa Kabisa Katoliki amefanya makosa kutoka takwimu na kusema ukweli hadharani.
JPM kafanya watendaji wake wawe watu wa ajabu sana, wenye hofu na kukabidhi akili kwake.
Huyu Abasssi hana akili kazi ni kulinda ugali wake tuUjinga mtupu,mapadri na masister ni Mali kanisa,wazazi wamewatoa sadaka.kwahiyo Wana haki ya kutufahamisha waumini hali ya watumishi wetu.
Wewe unaongelea kupigana, kulipuana na kujitoa mhanga kwa mabomu na misimamo ya kijihad lakini mimi naongelea uimara,ukubwa na mikakati ya kitaasisi ndio hapo tu tunapo pishanaMi nataka tu nikujulishe dini zinazoogopwa na serikali huwa ni waislamu. Maana wale wakimezeshana sumu huwa wanafanya kweli ndo maana serikali inawakumbatia na kuwasikiliza sana.
Acha wajaribu, wao si wanajifanya wababe? Najua hawawezi ndo nawa challenge. Kilangila.unadhani unaweza kumkamata kirahisi kama shehe ponda
Polokwani, aya yako ya mwisho ina ujumbe mzito. Asante kwa kutambua hili. Light watu wangefahamu!Wewe unaongelea kupigana, kulipuana na kujitoa mhanga kwa mabomu na misimamo ya kijihad lakini mimi naongelea uimara,ukubwa na mikakati ya kitaasisi ndio hapo tu tunapo pishana
Hakuna taasisi imara zaid ya ngome ya rumi hilo linajulikana duniani kote na ndio maana hata leo ukisikia pope fransis anakuja tanzania utaona nchi itakavyo simama na ni zaid hata ya ujio wa obama au joe baiden au hata qeen elizabeth na government officials wote utawaona wanavyo haha awe muislam au mkristo awe mkuu majeshi au rais.
Kuna vitu vingi na siri nyingi huzijui kuhusu hii taasisi ya rumi mkuu.
Msemaji mkuu wa Serikali ya Tanzania, Dk Hassan Abbas ametoa onyo kwa vyombo vya habari na watu binafsi kutoa taarifa za maradhi, vifo au wagonjwa bila kuzingatia misingi ya utoaji wa taarifa kwa sababu Serikali ina utaratibu wake wa kutoa taarifa.
Dk Abbas ameyasema hayo leo Alhamisi Machi 4, 2021 wakati akizungumza na Maelezo TV kuhusu tabia aliyoiona hivi karibuni ya vyombo vya habari na baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii kutoa taarifa zinazoihusu Serikali wakati kuna mamlaka husika za kufanya hivyo.
Amesema hata kwenye magonjwa ya kuambukiza na a ya mlipuko, zipo taratibu kwenye sheria za huduma ya jamii zinazoeleza ni kiongozi wa ngazi gani anapaswa kutoa taarifa kwa umma.
“Mtakumbuka mwaka jana Tanzania ilipopata janga la corona mheshimiwa Rais alitoa itifaki ya viongozi ambao watasemea maradhi haya ambapo ukiondoa viongozi wakuu wa kitaifa, viongozi wengine waliopewa jukumu hilo ni Waziri wa Afya na mimi Msemaji Mkuu wa Serikali,” amesema.
Amesema baadhi ya watu wameanza kujitokeza kutoa takwimu za maradhi mbalimbali, vifo au wagonjwa kwamba hilo siyo sahihi na ameviomba vyombo vya habari kuachana na watu wa namna hiyo.
Dk Abbas amesema kila mwanajamii wakiwemo viongozi wa dini anapaswa kushiriki kwa maana ya kutoa elimu, kusisitiza hatua za kuchukua, kushiriki katika kuitoa jamii hofu na kusisitiza mambo ambayo yapo kwenye miongozo.
“Utoaji wa takwimu na masuala mengine ya kisera kwenye maeneo haya yanapaswa kubaki kwa wasemaji rasmi na wataalamu ambao wana dhamana ya kufanya hivyo,” amesema Dk Abbas.
Dk Abbas ambaye pia ni katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, amesema mpaka sasa nchi inakwenda vizuri, wamefanikiwa kuiondoa jamii hofu na watu wanafanya kazi na kushiriki burudani na maisha yanaendelea.
Chanzo: Serikali ya Tanzania yaonya utoaji taarifa za maradhi, vifo