Serikali yaonya utoaji taarifa za maradhi, vifo au wagonjwa bila kuzingatia misingi ya utoaji taarifa

Serikali yaonya utoaji taarifa za maradhi, vifo au wagonjwa bila kuzingatia misingi ya utoaji taarifa

Tunazungumzia taratibu, maadili, kanuni na sheria za utoaji wa takwimu za magonjwa ya kuambukiza na ya milipuko.
1. Katika mlipuko wa ukimwi ulipotokea na hadi sasa unavyoendelea, mapadre kama Kitima walishawahi kutoa takwimu za mapadre na masista walioambukizwa ukimwi na waliofariki kwa ukimwi?

Si ni wengi tu, sasa kwa nini hatoi takwimu hizo ili tuhamasike kuchukua tahadhali zinazopaswa? Kwa nini anaona rahisi kutoa takwimu za gonjwa la corona kwa mapadre na watawa wa kanisa lake? Hajui kwamba corona inaambukizana kwa njia zote ambazo ukimwi unaambukizana pamoja na hizo njia nyingine? Yaani kama mpenzi wako ana corona lazima atakuambukiza, and vice versa, tena kirahisi zaidi kuliko virusi vya ukimwi.

All you need is close contact of any part of his/ her body provided that contact is within 1 metre distance. Contact ya ukimwi si zero distance pekee bali certain parts of your bodies have to be penetrating each other. Hivyo ni rahisi zaidi kupata corona kwa njia ya zinaa kuliko kupata ukimwi kwa njia ya zinaa.

Masista kwa kawaida huishi maisha ya isolation katika makazi yao. Hivyo ndivyo wanavyoishi mapadre kwenye makazi yao. Hutawaona masokoni wala kwenye madaladala. Contact yao na watu wengine ni kwenye nyumba za ibada tu ambamo watu huvaa barakola na kufanya social distancing. Sasa hizo close contact zingine kati ya mapadre na masista zimetokeaje hadi kupelekea vifo 25 za mapadre na 60 za masista kwa kuambukizana corona ndani ya miezi 2 tu? Padre Kitima anataka serikali ifanye nini kunusuru hii hali ya mapadre na masista kuambukizana corona? Hii kasi ya maambukizi kwa watawa hawa, kama takwimu za Kitima ni za kweli, ni kubwa sana xaidi ya mara kumi kuliko hali ilivyo kwa wengine. Yaani wanawazidi hata watoa huduma ya afya walio front line kutibu wagonjwa wa corona mara zaidi ya kumi? Kuna nini huko kwa watawa wetu?

NB: Hadi sasa wimbi hili la sasa la ugonjwa huu, kiwango chake bado kiko chini sana ukilinganisha na wimbi la mwaka jana. Na tayari karibu linafikia mwisho wa msimu wake. Tungefanya copy & paste ncji yetu ingalikuwa kwenye continous lockdown and face masks kwa zaidi ya mwaka mmoja hadi sasa.

Tulikataa kufanya hivyo. Wala hatuko peke yetu kufanya hivyo. Sweden walikataa kama sisi. Hadi sasa kimaambukizi na vifo sisi, Sweden na nchi zingine zilizochukua msimamo huu, ziko far better than those other countries such as USA and most European countries.
Mtu yeyote anayesema maambukizi au vifo vya corona, ni chini, lazima huyo mtu ni mjinga, mwendawaImu, mwongo, mnafiki na mpuuzi.

Utawezaje kusema tatizo ni dogo au kubwa wakati huna takwimu? Enyi wendawazimu mliwahi kuona maiti barabarani huko US, Italy au Brazil? Kuna watu wajinga kabisa wanasena tatizo la corona Tanzania ni dogo eti kwakuwa tu maiti hazionekani barabarani!! Hawa wanaotumia kigezo hiki ni taahira, vichaa au wendawazimu?

Kuna familia zimefiwa na wwtu mpaka 5, wengine 3 au 4, halafu kunatokea wendawazimu wanasema eti tatizo ni dogo! Wajinga wakubwa hawa. Mimi nimefiwa na ndugu yangu, kuna rafiki yangu amefiwa na ndugu zake wa karibu 7, akiwemo mama yake mzazi, mjomba wake, binamu yake na kaka yake.

Wenye akili kama Padre Kitima, wanatumia takwimu. Ameeleza vifo vya mapadre na watawa. Kwa kuangalia ratio ya populatuon ya mapadre na watawa kwa idadi ya Watanzania, ndiyo unajua ukubwa wa tatizo.

Bila takwimu, wajinga wanabwabawaja eti tatizo siyo kubwa. Tatizo siyo kubwa kwa sababu tu waliokufa siyo wewe au mama yako?
 
Utoaji wa taarifa wa serikali umekuwa 'bogus'.

Kazi kubwa ya serikali sasa imekuwa ni kupotosha!
Well said.

Serikali iliyostahili kuwa chombo cha kuaminka, limekuwa genge la uhalifu wa kutoa taarifa za uwongo. Hakuna mwenye ambaye yupo tayari kuzimeza taarifa za uwongo zinazotolewa na serikali.
 
Angalia ulivyo mnafiki na unajiita damu ya yesu, aliyeongea ni kiongozi wako wa dini, leo amekua UCHWARA?
Unadhani mimi ni mtu wa dini???? Hata kidogo!!!!

KIONGOZI YEYOTE WA KIROHO ANATAKIWA AYAONE MAMBO KIROHO, YA KISAYANSI AWAACHIE WANASAYANSI.


YESU NI BWANA NA MWOKOZI
 
Kitima anapaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu/ kisheria. Ni nchi gani hapa duniani ambayo mapadre ndiyo watoa takwimu za corona? Hata huko Italy ambako ndiyo makao makuu ya kanisa katoliki hawajawahi na hawatawahi kufanya hivyo.

Sayansi haitambui uwepo wa Mungu. Science has never discovered the existance of any matter in this universe which has characteristics of being called God. Iweze padre huyu ashabikie sayansi badala ya God?
pumbavu wewe anatoa taarifa za watawa wake
 
Hivi serikali hii haina kazi ya maana ya kufanya hadi inataka kubinafsisha utoaji wa habari wa ugonjwa na vifo? Dah, ama kweli mitano tena!
Ni kawaida ya mtu aliyeshindwa kazi ya msingi kujitungia vikazi vya uongo na kweli ilimradi aonekane yuko busy tu.
 
Hawa vichaa wanakoelekea watakuja kusema mtu ukifiwa usiwaambie jirani zako.
Ni ajabu na kweli. Hii desturi ya kukaa kimya mtu akifa niliwahi kuiona Usukumani kipindi wanauwa vikongwe kwa kisingizio cha ushirikina
 
Kweli ww ni Dk.Mwehu
Kitima anapaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu/ kisheria. Ni nchi gani hapa duniani ambayo mapadre ndiyo watoa takwimu za corona? Hata huko Italy ambako ndiyo makao makuu ya kanisa katoliki hawajawahi na hawatawahi kufanya hivyo.

Sayansi haitambui uwepo wa Mungu. Science has never discovered the existance of any matter in this universe which has characteristics of being called God. Iweze padre huyu ashabikie sayansi badala ya God?
 
Huwezi kushindana na dola!! Vinginevyo uko tayari kutumia!
hiyo dola unayo iongelea wewe unayo iaminia kwamba ndio kila kitu basi nikwambie tu yoote inaisujudia ngome ya rome/rumi ila kwa vile hujui kitu sio kosa lako
 
Ujue Kitima Ni Katibu wa TEC kwa hiyo Yeye Ni Kipaza sauti wa Vikao vya Tec.
Kitima anafuata nyayo za mtangulizi wake Dr. Willbond Slaa. Hiyo nafasi ya Katibu wa TEC inapaswa kuangaliwa kwa umakini. Ilimujenga Dr Slaa kutimukia chadema hadi kuwa balozi. Kitima naye kaianza safari hiyo. Kila la heri Dr Kitima, unakaribishwa sana huku.
 
Ukificha habari watu watatafuta habari nje na habari hizo huenda zikawa nzuri au mbaya hivyo toeni habari
 
Hivi serikali hii haina kazi ya maana ya kufanya hadi inataka kubinafsisha utoaji wa habari wa ugonjwa na vifo? Dah, ama kweli mitano tena!
Ukishindwa kuwaletea watu maendeleo, lazima ujiongeze kuwachanganya na stories za mabeberu na wasaliti.

Ama sivyo watakustukia umeshindwa mwenyewe.
 
Seikali ya maonyo na maagizo. Kila siku lazima utasikia waziri mkuu au waziri yoyote anatoa maagizo kwa wakuu wa mikoa na viongozi wengine wafanye hiki. Huwa najiuliza haya maagizo yalivyo mengi hivi hawayasahau kweli.?
 
Nilisema hata jana na ninarudia tena ngome ya rome /catholic inanguvu na ni nzito kuliko hata hiyo serikali ya jiwe hivyo serikali isiingie kichwa kichwa.
Mi nataka tu nikujulishe dini zinazoogopwa na serikali huwa ni waislamu. Maana wale wakimezeshana sumu huwa wanafanya kweli ndo maana serikali inawakumbatia na kuwasikiliza sana.
 


Msemaji mkuu wa Serikali ya Tanzania, Dk Hassan Abbas ametoa onyo kwa vyombo vya habari na watu binafsi kutoa taarifa za maradhi, vifo au wagonjwa bila kuzingatia misingi ya utoaji wa taarifa kwa sababu Serikali ina utaratibu wake wa kutoa taarifa.

Dk Abbas ameyasema hayo leo Alhamisi Machi 4, 2021 wakati akizungumza na Maelezo TV kuhusu tabia aliyoiona hivi karibuni ya vyombo vya habari na baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii kutoa taarifa zinazoihusu Serikali wakati kuna mamlaka husika za kufanya hivyo.

Amesema hata kwenye magonjwa ya kuambukiza na a ya mlipuko, zipo taratibu kwenye sheria za huduma ya jamii zinazoeleza ni kiongozi wa ngazi gani anapaswa kutoa taarifa kwa umma.

“Mtakumbuka mwaka jana Tanzania ilipopata janga la corona mheshimiwa Rais alitoa itifaki ya viongozi ambao watasemea maradhi haya ambapo ukiondoa viongozi wakuu wa kitaifa, viongozi wengine waliopewa jukumu hilo ni Waziri wa Afya na mimi Msemaji Mkuu wa Serikali,” amesema.

Amesema baadhi ya watu wameanza kujitokeza kutoa takwimu za maradhi mbalimbali, vifo au wagonjwa kwamba hilo siyo sahihi na ameviomba vyombo vya habari kuachana na watu wa namna hiyo.

Dk Abbas amesema kila mwanajamii wakiwemo viongozi wa dini anapaswa kushiriki kwa maana ya kutoa elimu, kusisitiza hatua za kuchukua, kushiriki katika kuitoa jamii hofu na kusisitiza mambo ambayo yapo kwenye miongozo.

“Utoaji wa takwimu na masuala mengine ya kisera kwenye maeneo haya yanapaswa kubaki kwa wasemaji rasmi na wataalamu ambao wana dhamana ya kufanya hivyo,” amesema Dk Abbas.

Dk Abbas ambaye pia ni katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, amesema mpaka sasa nchi inakwenda vizuri, wamefanikiwa kuiondoa jamii hofu na watu wanafanya kazi na kushiriki burudani na maisha yanaendelea.

Chanzo: Serikali ya Tanzania yaonya utoaji taarifa za maradhi, vifo
Yaani mwanangu afariki kwa koroona nikae kimya hadi Abasi aje aseme?
 
Back
Top Bottom