Serikali yapiga marufuku matumizi ya kuni na mkaa kulisha watu zaidi ya 100

Serikali yapiga marufuku matumizi ya kuni na mkaa kulisha watu zaidi ya 100

Serikali iweke sheria kali, izuie upakiaji wa mikaa, mkaa ukiwa ghali watu watatafuta mbadala wake
 
Makande ,ubwabwa wa matandu ,nyama ya chairfire watapikia kwenye mafuta au gesi? Wanajua madhara ya jiko la mafuta(mchina)? Mafuta yenyewe ya taa lita moja Tsh 4000 ,jiko la gesi la maana kuanzia laki na 20 ,mtungi wa gesi kuanzia 90 hadi 125k ,sasa ukikmataza kupikia kuni hizo bidhaa mabadala utamnunulia?
 
Wenzetu kabla ya kupiga marufuku kitu wanaangalia mbadala na kuhamasisha kwanza pia kuyengeneza kitu cha kuwa mbadala
Ila sisi tunakurupuka kwa kupiga marufuku ili waje na mafaini tu
Serikali iwekeze zaidi kwenye gas na umeme
Pia upandaji wa miti uwe kama zoezi endelevu kila mahali kwa lazima

Wachoma mikaa ndio balaa na pia wakulima wa Tumbaku
 
Ni jambo jema sana! Mazingira yameathirika vibaya sana na ukataji miti ovyo. Serikali kwa upande wake ihakikishe nishati mbadala inapatikana kwa wingi na kwa bei rahisi nchini kote.
Lakini serikali ingeandaa mazingira rafiki na mbadala badala ya kukurupuka kuzuia.
 
Lakini serikali ingeandaa mazingira rafiki na mbadala badala ya kukurupuka kuzuia.
Of course nishati mbadala ikipatikana kwa bei rafiki automatically wananchi wataachana na ukataji miti bila Serikali kutumia maguvu!

Matumizi ya maguvu ni dalili Serikali imeshindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwenye suala hili.
 
Hii nchi wana siasa badala ya kufanya kazi za kuwa tumikia wananchi wame amua kuwa wapiga debe wa makampuni ga biashara kwa manufaa yao.
Mungu hakuwa mjinga mutupa mapori.
Nature lazima ichukue nafasi yake.
Ita fika siku hawa hawa wana suasa wata kuwa wsfugaji wa kuku wa kisasa na samaki watupige marufumu kula ng'ombe na mbuzi wetu ili tununue vya kwao.
Tume ona mkigawa taifa gas nani asie jua ni kampuni ya jambazi namba moja wa nchi hii??
 
Nishati mbadala zinafaa pia kuandaa nyama choma na vyakula vingine vinavyoandaliwa kwa kuchoma.
Iliyochomwa kwenye moto ni tofauti, kwa mfano kuna baadhi ya maeneo wanaotumia gesi, mishikaki wanadumbukiza kwenye mafuta; sasa ile ladha ya uchomwaji inakuwa haipo.​
 
Iliyochomwa kwenye moto ni tofauti, kwa mfano kuna baadhi ya maeneo wanaotumia gesi, mishikaki wanadumbukiza kwenye mafuta; sasa ile ladha ya uchomwaji inakuwa haipo.​
Kwa maelezo yako hayo unazungumzia luxurious life.

Maisha ya anasa yana gharama zake; mkaa hautapigwa marufuku kabisa ila unaweza kuuzwa gunia sh laki tano ili watu wa class yako muendelee na maisha bila athari kubwa za kimazingira.
 
Itaathiri pia ajira za wengine
 
Back
Top Bottom