Serikali yapiga marufuku nyimbo za ovyo kwenye magari ya shule

Watoto Wanaosoma shule za serikali hizi wanatumia usafiri wa uma. Wana gari zao maalum kabisa kwamba hawapandi zingine Hadi afike konda flani wa gari Fulani.

Watoto wakiingia humo garini wanatoka flash na kumpa dereva awawekee playlist Yao humo kwe gari kunakua kama club.

Sasa we mtu mzima jifanye unajua malezi uropoke utashambuliwa had utiwe aibu nimekiona hili kwe daladala nyingi za mbez temeke. Hiki kizazi sijui kitapona kwa dawa gani
 
Sio tu kwenye mabasi ya shule, hata kwenye dalaladala na mabasi ya abiria.
Kweli mkuu! Inaweza tokea uko kwenye daladala na mama Ako ikapigwa, inama nipachike rungu,nitereze kama nyoka pangoni.
 
Wanavyoagiza utadhani wizara ya elimu imetoa magari yakubeba wanafunzi.. Inamaana hawajui kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi wanapanda public transport (daladala)? Hiyo amri inawahusu hadi wamiliki wa daladala?
 
Kabla hawajaja na matamko wakusanye kwanza maoni kutoka kwa wananchi, kwanza miziki ya hovyo ni ipi? Kama ni ya hovyo kwa nini iruhusiwe kwa baadhi ya makundi, je nani anasimamia hayo makundi kutosambaza miziki hiyo kwa jamii, je ni miziki tu!!? Filamu zinazorushwa na stesheni mbalimbali haziwezi kuzuiwa? Je TCRA, BASATA wanatimiza wajibu wao vilivyo?

Hiyo miziki na filamu za hovyo hazipo kwenye mabasi ya shule tu, zipo kwenye mabasi makubwa ya safari ndefu na fupi, zipo majumbani migahawani na kila sehemu ya public, kupiga marufuku miziki kwenye magari ya shule ni kujidanganya, kuna watoto wa shule wanapanda bajaj, mabasi makubwa nk.

Nilidhani serikali ipige marufuku kiziki hiyo kwenye maeneo yote ya public na hasa yenye watoto, pili BASATA wazuie hiyo miziki, TCRA wazuie filamu za hovyo ili kukinusuru kizazi hiki, kwasasa kina hali mbaya
 
Sio tu kwenye mabasi ya shule, hata kwenye dalaladala na mabasi ya abiria.
  • Wakishapiga biti wanaenda kunywa mvinyo. Ndio imetoka hiyo!!!
  • Kwenye mabasi wamewahi piga mkwara, ila hali ni mbaya nahisi kuliko kabla ya mkwara.
  • Hakuna raha kusafiri kwa mabasi, inakwaza kweli hasa kama upo na familia.
  • Kuna minyimbo ya kishetani mithili ya pono.
  • Viongozi wapo zao kwenye usafiri wa umma (J, STK, ...) wa kifahari; hawataki kadhia ya kuzuia ushetani huko kwa maraia.
 
Tulipata kuwasilisha haya tukaambiwa tuna wivu na biashara za watu, lakini nilijifunza jambo wanaoshupalia yawepo ni vijana wasio na familia na wenye familia zilizopoteza mwelekeo
 
  • Nahisi hawataki mambo magumu yenye 'kuudhi' wasaidizi wao wa kampeni.
  • FREE MARKET IS NOT UNCONTROLLABLE MARKET!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…