Serikali yapiga Marufuku Uhamisho wa Watumishi

Serikali yapiga Marufuku Uhamisho wa Watumishi

Viongozi wetu Bana, inachekesha Sana... Walioajiriwa na serikali wanapata tabu, kazi wamepata Kwa shida na hata walivyoajiriwa na maisha Yao pia ni shida Tu, sasa bwana waziri kijana Yuko let say Halmashauri kaona kazi zimetangazwa labda za TRA au mashirika ya serikali ina maana asiombe kazi hizo wakati ni Haki Yake maana akifaulu lazima ahame, hivyo asihame?? maana wengine hufuata maslahi regardless Yuko kijijini ilimradi ni sehemu inayolipa, hivi vitakuwa vichekesho sasa...Hiyo kauli ina mikanganyiko Sana, poleni sana waajiriwa.
 
Miundombinu ipo ,watu wa Dar ni muache kazi au muende kuhudumia watu Vijijini
Hapana, mimi nipo Mbeya huku nasoma. Ni jiji kabisa lakini miundombinu bado, na sio Mbeya tu miji mingi Tanzania miundombinu sio mizuri. Serikali ina kazi kubwa sana ya kufanya kuliko inavyofikiria
 
Hapana, mimi nipo Mbeya huku nasoma. Ni jiji kabisa lakini miundombinu bado, na sio Mbeya tu miji mingi Tanzania miundombinu sio mizuri. Serikali ina kazi kubwa sana ya kufanya kuliko inavyofikiria
Unataka kazi au miundombinu?
 
Sasa mbona unapoomba kazi wanakuambia uchague? Huyo anaesema chagua kituo cha kufanya kazi si ndo hajatumia akili??

Angepanga tu bila kuwaambia wati wachague.
Na kama umepangwa ambako hupataki Kwann unaenda na hadi mkataba unasign?
 
Back
Top Bottom