Serikali yapiga Marufuku Uhamisho wa Watumishi

Serikali yapiga Marufuku Uhamisho wa Watumishi

Kwamba Serikali imekosa Kwa kupeleka hela Hadi wajenge Barabara za lami Kijijini? Mengine yote yapo na wanaotakiwa kwenda kutoa Huduma huko kwenye mahospitali ndio nyie mnaotaka uhamisho
Wewe hutaki Tanzania iendelee, comment zako nyingi zinaonesha unafurahia jinsi nchi ilivyo nyuma kimiundombinu, unaona sawa tu
Kwa hiyo vijijini lami haihitajiki, sio? Unakosa hata chembe ya uzalendo na ni nchi yako hii unayoiongelea hivyo. Bure kabisa!
 
Serikali Haina pesa za kuchezea kiasi kwamba ipeleke lami Vijijini wakati hadi Leo hii hakuna lami za Mkoa na Mkoa.

Barabara ni uwekezaji sio jambo la kujifurahisha.

Hutaki kwenda Kijijini acha kazi
 
Nyie wajinga badala ya kuachia halmashauri husika ziajiri watu mmejilimbikizia madaraka mnafanya uajiri wa wafanyakazu wa Nkasi, Tandahimba na Tukuyu huko Dodoma na Dar, upuuzi mtupu.
Mtaenda tuu huko Tandahimba hutaki acha kazi.

Pili Serikali iliamua hivyo kuondoa upendeleo lakini pia Bado hata ukifanya hivyo Kuna watu watatoka Dar watakuja kupata kazi huko na wataomba uhamisho.

Ukitaka Kila Halmashauri iajiri manake ziwe na mamlaka Yao ya ndani ya kujitegemea.
 
Tatizo serikali haipeleki maendeleo baadhi ya sehemu, kama wanataka watu wasihame at least waboreshe miundombinu na huduma za kijamii kila sehemu ili watu wasipakimbie
Taizo hawatakiwa watu wahame na miundombinu haiboreshwi
 
Watakutana na rungu la mwajiri wakiwa huko huko ikiwemo kufukuzwa kazi
Hayo ni maneno matupu, mbona sijawaji kusikia mwalimu amefukuzwa kazi kwa ufanyaji mbovu wa kazi ilihali ukizunguka vijijini unakutana na walimu wengi wazembe na wavivu.
 
Hayo ni maneno matupu, mbona sijawaji kusikia mwalimu amefukuzwa kazi kwa ufanyaji mbovu wa kazi ilihali ukizunguka vijijini unakutana na walimu wengi wazembe na wavivu.
Kuna kazi za viongozi kuzozana na Watumishi sio walimu.

Ualimu sio kazi ni wito na walimu ndio wanatumikishwa zaidi Kwa Kila kitu na Serikali ni watiiifu.
 
Taizo hawatakiwa watu wahame na miundombinu haiboreshwi
Shida ndio inaanzia hapa. Unapeleka watu wakafanye kazi sehemu haina maji, haina umeme, barabara ni vumbi tupu, zahanati ni moja tu tena ni below average na unajua hawawezi kukataa kwa sababu wanahitaji kazi.
Serikali inapaswa iweke focus kubwa vijijini na wilayani sasahivi, wanaoishi kule ni Watanzania pia. Haiwezekani nchi ijengwe nusu nusu
 
Wanajikuta wanalazimika kusign lakini madhara yake ni kwamba hawatakuwa productive kazini. Kazi watazifanya bora liende, kitu kinachopelekea huduma za serikali kuendelea kuwa duni siku hadi siku.

Hiyo ndo picha kubwa ambayo wanaoshangilia jambo hili, ikiwemo waziri, na kitatange (ChoiceVariable ) huwa hawaioni.

Na impact ya watu kufanya kazi bora liende ni kubwa sana.
Au sio, Wanafanya kazi wakisubiri tu Uhakika mshahara lakini ufanisi/efficiency 10%
 
Back
Top Bottom