Serikali yapokea msaada wa magari mawili kutoka Qatar kwa ajili ya kuhudumia viongozi wanaokuja nchini

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
๐—ช๐—ฎ๐˜‡๐—ถ๐—ฟ๐—ถ ๐—ž๐—ผ๐—บ๐—ฏ๐—ผ ๐—ฎ๐—ฝ๐—ผ๐—ธ๐—ฒ๐—ฎ ๐—บ๐—ฎ๐—ด๐—ฎ๐—ฟ๐—ถ ๐—บ๐—ฎ๐˜„๐—ถ๐—น๐—ถ ๐—ธ๐˜‚๐˜๐—ผ๐—ธ๐—ฎ ๐—ค๐—ฎ๐˜๐—ฎ๐—ฟ

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea magari mawili aina ya Land Cruiser Prado kutoka Taifa la Qatar kwa ajili ya kuhudumia viongozi wanaokuja kwa ziara za kitaifa na kikazi nchini.

Qatar kama mshirika wa maendeleo ya uchumi wa Tanzania alikubali ombi na ametoa magari hayo mapya kufuatia ombi la magari na pikikipiki za kuhudumia viongozi wa nje wawapo katika ziara nchini huku wakiendelea na mchakato wa kuleta pikipiki sita.

Akizungumza katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhiwa nyaraka za magari hayo, Mheshimiwa Waziri, Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) ameishukuru Qatar kwa kuwa mdau mkubwa wa maendeleo Tanzania na kuahidi kutumia vyema misaada hii ili kuweza kutatua changamoto zinazojitokeza katika kazi.

Akimkabidhi funguo za magari hayo Afisa Usafirishaji Mkuu, Bw. Maulid Mkenda, Mhe. Waziri Kombo amehimiza kuyatunza magari hayo ili yadumu na kuleta tija na ufanisi.

Qatar pia imekuwa ikitoa ushirikiano katika masuala ya ajira kwa vijana kwa kutoa nafasi za ajira kwa madereva wa Kitanzania nchini Qatar huku nafasi nyingine zikiendelea kuja na kutangazwa.

IMG-20251127-WA0124.jpg
IMG-20251127-WA0123.jpg
IMG-20251127-WA0119.jpg
IMG-20251127-WA0117.jpg
 
Yaaani magari 2 ndo anapokea Waziri?๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…

Kweli nchi imeshajifia hii. Hongera Samia kwa kuiangamiza Tanganyika.

Tumefika hatua kuita press kupewa msaada wa prado 2?? Kweli umetumalizia Taifa letu.

Baada ya kunyimwa mikopo na misaada ya Bilions of Money na Mataifa Makubwa sahivi tumeishiwa hadi tunaitisha Press kupokea prado 2??๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…
 
๐—ช๐—ฎ๐˜‡๐—ถ๐—ฟ๐—ถ ๐—ž๐—ผ๐—บ๐—ฏ๐—ผ ๐—ฎ๐—ฝ๐—ผ๐—ธ๐—ฒ๐—ฎ ๐—บ๐—ฎ๐—ด๐—ฎ๐—ฟ๐—ถ ๐—บ๐—ฎ๐˜„๐—ถ๐—น๐—ถ ๐—ธ๐˜‚๐˜๐—ผ๐—ธ๐—ฎ ๐—ค๐—ฎ๐˜๐—ฎ๐—ฟ

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea magari mawili aina ya Land Cruiser Prado kutoka Taifa la Qatar kwa ajili ya kuhudumia viongozi wanaokuja kwa ziara za kitaifa na kikazi nchini.

Qatar kama mshirika wa maendeleo ya uchumi wa Tanzania alikubali ombi na ametoa magari hayo mapya kufuatia ombi la magari na pikikipiki za kuhudumia viongozi wa nje wawapo katika ziara nchini huku wakiendelea na mchakato wa kuleta pikipiki sita.

Akizungumza katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhiwa nyaraka za magari hayo, Mheshimiwa Waziri, Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) ameishukuru Qatar kwa kuwa mdau mkubwa wa maendeleo Tanzania na kuahidi kutumia vyema misaada hii ili kuweza kutatua changamoto zinazojitokeza katika kazi.

Akimkabidhi funguo za magari hayo Afisa Usafirishaji Mkuu, Bw. Maulid Mkenda, Mhe. Waziri Kombo amehimiza kuyatunza magari hayo ili yadumu na kuleta tija na ufanisi.

Qatar pia imekuwa ikitoa ushirikiano katika masuala ya ajira kwa vijana kwa kutoa nafasi za ajira kwa madereva wa Kitanzania nchini Qatar huku nafasi nyingine zikiendelea kuja na kutangazwa.

This is seriously too much๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ
 
Halafu wao familia ya Qatar wamepewa kipande cha mbuga na vitalu vya kuwinda wanyamapori tujiandae jamii ya maasai kutimuliwa tena mahali.

Nani asiyefahamu hiyo royal family ya Qatar na matanuzi yao ya kifahari.

Hiyo familia ina ndege moja ya kisasa huwa msimu wa joto ukiwa mkali huko gulf wanahama na kwenda Hispania katika kisiwa kimoja kubadili hali ya hewa.
 
Back
Top Bottom