Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hiyo huu uachwe uharibike?
Hauko sawa mkuu, ikiwa uwanja ulijengwa 2007, unahitaji ukarabati mkubwa sana
Hutashuhudia kwaya wala matamasha mule baada ya marekebisho hata Simba na Yanga zitakutana pale kama zinacheza kati yao tuKwani sasa umeharibika?.. matengezo sio kwa kila kilocho haribika ata kuboresha ni matengenezo.
Ule uwanja ubakize matukio muhimu, itapunguza maintenance na itaongeza ubora. Wewe uwanja hadi kwaya zinajimwaga humo, mihadhara, vilabu
huwezi karabati uwanja ule kwa bil 30, nyingi mnooooKo tujenge kingine ule wa mkapa tuutelekeze?
fuatilia ule uwanja wa azam wamejenga kwa sh ngap utashangaa.......kuwa serious Mkuu.... "VILE VYA AZAM VIWILI HADI VITATU...."
Unge bid hio tenderhuwezi karabati uwanja ule kwa bil 30, nyingi mnoooo
Hutashuhudia kwaya wala matamasha mule baada ya marekebisho hata Simba na Yanga zitakutana pale kama zinacheza kati yao tu
Hii sehemu ya kuchezea si imetoka kutifuliwa juzi tuVitu vyote hivyo vinavyofanyiwa ukarabati bado unasema upigaji mkubwa!?..ile tv ya matokeo na mifumo yake Bei gani!?..watifue sehemu ya kuchezea,vitu vipya elfu 55,sehemu ya kukimbilia nk
Nimeikuta mahali!!!!!!!!!! Tukiamua tunaweza kuwa na viwanja vya kisasa!!!!!!!!!!!!Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Said Yakubu amesema Serikali ya [emoji1241] imetoa Tsh 30 𝘽𝙄𝙇𝙇𝙄𝙊𝙉 kwa ajili ya kuufanyia ukarabati uwanja wa Mkapa.
Amesema maboresho hayo yatafanyika katika maeneo ya kuchezea, vyumba vya wachezaji na kutoa viti vyote vya uwanja huo.
Uwanja wa Mkapa ulizindulwa rasmi mwaka (2007). Mpaka kukamilika uligharimu kiasi cha $ 56 Million sawa na Tsh 137+ 𝘽𝙄𝙇𝙇𝙄𝙊𝙉.
===
View attachment 2700662
View attachment 2700663
Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesaini mkataba wa makubaliano ya ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa na Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) ya China ambao utagharimu zaidi ya Sh. bilioni 31 hadi kukamilika Julai 2024.
Hayo yamesemwa Dar es Salaam Julai 27, 2023 na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Pindi Chana baada ya kusaini mkataba na kampuni BCEG ya China ambao pia ndio waliojenga uwanja huo.
Alisema lengo la kukarabati huo ni kufikia viwango vya Chama cha Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) Pamoja na Chama cha Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ili uendelee kuwa bora zaidi.
"Wito wangu kwa kampuni ya BCEG, hakikisheni kazi hii mnayoifanya iwe ya viwango vinavyowekwa iendane na ubora na viwango vya CAF na FIFA na ikamilike kwa wakati” amesema Dkt. Chana.
Naye Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bw. Said Yakubu amesema uwanja huo utafanyiwa marekebisho katika eneo la vyumba vya wachezaji, chumba cha waandishi wa Habari, eneo la watu mashuhuri (VVIP), kubadilisha viti vyote vya kukalia mashabiki uwanjani hapo, ubao wa kuonesha matokeo, kuweka mfumo mpya wa TEHAMA, kubadilisha eneo la kuchezea na seti mbili za magoli ambazo zitatumika uwanjani hapo.
Maeneo mengine ambayo yatafanyiwa ukarabati ni viti vya benchi la ufundi na wachezaji wa akiba, mfumo wa umeme, mfumo wa sauti, eneo la kukimbilia wanariadha, chumba cha VAR, lifti mbili mpya, mfumo wa taa, mfumo wa maji taka, mgahawa pamoja na vitu vingine ambavyo vimepita muda wa matumizi kwani vilitakiwa kutumika kwa muda wa miaka saba tu.
Aidha, Katibu Mkuu Yakubu ametoa wito kwa watumiaji wa uwanja huo wakiwemo mashabiki, kuhakikisha wanatunza miundombinu ya uwanja huo ili iendelee kutumika kadiri ilivyopangwa na kuendelea kuwa eneo la watanzania kupata burudani wakati wa kuangalia mechi mbalimbali na nchi jirani wanautumia kama uwanja wao wa nyumbani.
Katika kufanikisha ukarabati huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) watatoa viti vipya vitakavyotumiwa na benchi la ufundi pamoja na wachezaji wa akiba wakati mechi uwanjani hapo na Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) litagharimia matengenezo ya eneo la kuchezea mpira katika uwanja huo.
Hufuatilii kabisa mambo!Hii sehemu ya kuchezea si imetoka kutifuliwa juzi tu
Kivipi mkuuHufuatilii kabisa mambo!
Ngumu kuliko ugumu wenyewe, kubwa kuliko utasikia serikari imetoa pesa za kuukarabati uwanja wakati uwanja wenyewe ulikuwa unaingiza mapato, sasa si ujikarabati kwa pesa zakeHapo usikute kiasi halisi kinachohitajika ni Bilioni 5 tu. Nchi ngumu sana hii.
Ile tv tu na mifumo yake Bei gani!?..vitu uwanja mzima?!Hapo usikute kiasi halisi kinachohitajika ni Bilioni 5 tu. Nchi ngumu sana hii.
Kuna harufu ya kupigwaKatibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Said Yakubu amesema Serikali ya [emoji1241] imetoa Tsh 30 𝘽𝙄𝙇𝙇𝙄𝙊𝙉 kwa ajili ya kuufanyia ukarabati uwanja wa Mkapa.
Amesema maboresho hayo yatafanyika katika maeneo ya kuchezea, vyumba vya wachezaji na kutoa viti vyote vya uwanja huo.
Uwanja wa Mkapa ulizindulwa rasmi mwaka (2007). Mpaka kukamilika uligharimu kiasi cha $ 56 Million sawa na Tsh 137+ 𝘽𝙄𝙇𝙇𝙄𝙊𝙉.
===
View attachment 2700662
View attachment 2700663
Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesaini mkataba wa makubaliano ya ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa na Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) ya China ambao utagharimu zaidi ya Sh. bilioni 31 hadi kukamilika Julai 2024.
Hayo yamesemwa Dar es Salaam Julai 27, 2023 na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Pindi Chana baada ya kusaini mkataba na kampuni BCEG ya China ambao pia ndio waliojenga uwanja huo.
Alisema lengo la kukarabati huo ni kufikia viwango vya Chama cha Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) Pamoja na Chama cha Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ili uendelee kuwa bora zaidi.
"Wito wangu kwa kampuni ya BCEG, hakikisheni kazi hii mnayoifanya iwe ya viwango vinavyowekwa iendane na ubora na viwango vya CAF na FIFA na ikamilike kwa wakati” amesema Dkt. Chana.
Naye Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bw. Said Yakubu amesema uwanja huo utafanyiwa marekebisho katika eneo la vyumba vya wachezaji, chumba cha waandishi wa Habari, eneo la watu mashuhuri (VVIP), kubadilisha viti vyote vya kukalia mashabiki uwanjani hapo, ubao wa kuonesha matokeo, kuweka mfumo mpya wa TEHAMA, kubadilisha eneo la kuchezea na seti mbili za magoli ambazo zitatumika uwanjani hapo.
Maeneo mengine ambayo yatafanyiwa ukarabati ni viti vya benchi la ufundi na wachezaji wa akiba, mfumo wa umeme, mfumo wa sauti, eneo la kukimbilia wanariadha, chumba cha VAR, lifti mbili mpya, mfumo wa taa, mfumo wa maji taka, mgahawa pamoja na vitu vingine ambavyo vimepita muda wa matumizi kwani vilitakiwa kutumika kwa muda wa miaka saba tu.
Aidha, Katibu Mkuu Yakubu ametoa wito kwa watumiaji wa uwanja huo wakiwemo mashabiki, kuhakikisha wanatunza miundombinu ya uwanja huo ili iendelee kutumika kadiri ilivyopangwa na kuendelea kuwa eneo la watanzania kupata burudani wakati wa kuangalia mechi mbalimbali na nchi jirani wanautumia kama uwanja wao wa nyumbani.
Katika kufanikisha ukarabati huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) watatoa viti vipya vitakavyotumiwa na benchi la ufundi pamoja na wachezaji wa akiba wakati mechi uwanjani hapo na Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) litagharimia matengenezo ya eneo la kuchezea mpira katika uwanja huo.
Hivyo viti vina shida gani mpaka wavitoe? Ukarabati ulitakiwa kufanyika kwenye miundombinu ya maji, vyooni, kupaka rangi, na kuendelea kuiboresha pitch.Ile tv tu na mifumo yake Bei gani!?..vitu uwanja mzima?!
Vitu vyote vinafanana rangi,vile vilivyorudishiwa vinafanya uwanja unakua Kama nguo yenye viraka,tv huko nyuma tukiangalia Sana matangazo ya Serengeti na stars,na huwa inaonesha muda na matoleo ukiwa uwanjani,ile tv scoreboard inafika Hadi Dola laki Saba unusu,kumbuka uwanja una umri wa zaidi ya miaka 15 sasaHivyo viti vina shida gani mpaka wavitoe? Ukarabati ulitakiwa kufanyika kwenye miundombinu ya maji, vyooni, kupaka rangi, na kuendelea kuiboresha pitch.
Halafu hiyo TV iliwahi kufanya kazi tangu ilipofungwa? Na kwa nini walioiweka wasiwajibishwe kwa utapeli?