Serikali yasaini Mkataba wa Ujenzi wa Barabara ya Njia Sita Dodoma–Chamwino Ikulu, Bilioni 241 kutumika

Serikali yasaini Mkataba wa Ujenzi wa Barabara ya Njia Sita Dodoma–Chamwino Ikulu, Bilioni 241 kutumika

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
WhatsApp Image 2026-05-18 at 19.42.07.jpeg
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ameshuhudia utiaji saini wa mkataba wa upanuzi wa barabara ya Dodoma Mjini–Chamwino Ikulu yenye urefu wa kilometa 32 kuwa ya njia sita, mradi utakaogharimu takribani shilingi bilioni 241 hadi kukamilika kwake.

Mkataba huo umesainiwa kati ya TANROADS kwa niaba ya Serikali na China Railway Construction Engineering Group (CRCEG) ya China, kwa lengo la kutekeleza upanuzi wa barabara hiyo kuwa ya njia sita.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini iliyofanyika katika Uwanja wa Mashujaa, jijini Dodoma leo Mei 18, 2026, Waziri Ulega ameuagiza TANROADS kuhakikisha inamsimamia mkandarasi huyo kwa karibu ili mradi huo ukamilike kwa viwango vya ubora vinavyolingana na hadhi ya jiji la Dodoma.
WhatsApp Image 2026-05-18 at 19.42.08.jpeg
WhatsApp Image 2026-05-18 at 19.42.11.jpeg
Ulega amesisitiza umuhimu wa kuwekwa kwa taa za kisasa, bustani, njia za watembea kwa miguu pamoja na miundombinu ya kuvutia, ili kuifanya Dodoma kuwa na sura ya jiji la kisasa.

“Tunataka mtu akipita usiku aione Dodoma inavyong’ara. Taa za barabarani lazima ziwe za viwango vya juu,” amesisitiza Waziri Ulega.

Aidha, amewataka wataalamu wa usanifu kuzingatia usalama wa watumiaji wa barabara kwa kuweka maeneo salama ya kuvuka, hatua itakayosaidia kupunguza ajali zinazotokea katika baadhi ya maeneo ya jiji.
WhatsApp Image 2026-05-18 at 19.42.13.jpeg
WhatsApp Image 2026-05-18 at 19.42.13 (1).jpeg
Vilevile, Ulega amebainisha kuwa sambamba na mradi wa DIST, Serikali tayari imesaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya mzunguko wa ndani wa Jiji la Dodoma yenye urefu wa kilometa 6.4, unaofadhiliwa na Serikali ya Japan kwa gharama ya yen bilioni 2.78.

“Lengo la mradi huo ni kupunguza msongamano wa magari katikati ya jiji na kurahisisha usafiri pamoja na shughuli za kijamii na kiuchumi katika makao makuu ya nchi,” amefafanua Ulega.

Kadhalika, ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika sekta ya miundombinu kupitia ujenzi wa barabara na madaraja, kwa lengo la kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha huduma za usafiri nchini.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jabir Shekimweri, ameishukuru Serikali kwa kutoa shilingi bilioni 19 kwa ajili ya fidia kwa wananchi watakaopisha utekelezaji wa mradi huo, huku akiahidi ushirikiano wa karibu kutoka kwa uongozi wa mkoa katika kipindi chote cha utekelezaji.

Shekimweri pia ameiomba Wizara kuzingatia zaidi usalama wa wananchi kwa kujenga vivuko vya juu au chini ya barabara, pamoja na kufunga kamera za usalama barabarani.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakoso, ameipongeza Serikali kwa utekelezaji wa mradi huo, huku akiishauri kuendelea kutoa kipaumbele kwa miradi viporo katika bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27.

Akitoa taarifa ya mradi huo, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mohamed Besta, amesema mradi huo utatekelezwa kwa utaratibu wa Sanifu na Jenga (Design and Build), na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 36, ikijumuisha miezi sita ya usanifu na miezi mitatu ya maandalizi ya awali.
 
Wa Tanzania baida ya miaka zaidi ya 60 ya uhuru ,hawawezi kujenga barabara ya njia SITA ?..

Kila kitu wanapewa wachina TU, ??

nyie Wana siasa na wa TZ muna haki ya kujitegemea kiuchumi ikiwemo kuwa na construction companys za kujenga hizo barabara na kupata faida, hakuna haja ya kujificha kwa wachina

Hii tabia ya kuwatumia wa china, ni zaidi ya uhujumu uchumi....
 
Back
Top Bottom