Serikali yasalimu amri mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo, yakubali kusitisha kamatakamata ya TRA na kuleta mfumo mpya wa kodi

Serikali yasalimu amri mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo, yakubali kusitisha kamatakamata ya TRA na kuleta mfumo mpya wa kodi

Hiyo ndio Taarifa ya sasa baada ya mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo unaoendelea

=======

Serikali imesitisha zoezi la ukaguzi wa risiti za Kielekroniki (EFD) na ritani za kodi iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia mkoa wa kikodi wa Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, wakati ukiandaliwa utaratibu mzuri wa utekelezaji wa suala hilo katika Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo.

Hayo yamesemwa kwa niaba ya Serikali, jijini Dodoma, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, wakati akitoa maazimio ya kikao kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara Tanzania, Viongozi wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Taasisi zinazosimamia masuala ya wafanyabiashara, kikao ambacho kiliitishwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na kuhudhiriwa pia na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.

Pia, Soma=> Mgomo wa Wafanyabiashara: Biashara zafungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024
TRA waendelee na zoezi lao kwenye mikoa mingine ya kikodi.
 
Nani alikuambia udikteta uliwahi kufanya matokeo chanya?

Hao wote uliowataja ni vichaa ndio maana wao kila maamuzi walitumia/wanatumia nguvu pasina akili.

Mgomo bila vurugu ni haki kikatiba muwe mnaelewa vitu.

Hapo serikali imepoteza mapato ambayo ndio kodi mnazomsifia huyo malkia wa anga kuwa katoa mabilionj kwenye mradi fulani.
Asante kwa elimu nzuri.
 
Wanadekezwa hao na Samia Kwa sababu Kila kitu anawasikiliza.

Rais angekuwa Magu au Makonda au Mwigulu na PM Chalamila hakuna rangi wangeacha kuona

View: https://www.instagram.com/reel/C8mEzRNN7QA/?igsh=aDNoeDhzdTh2b3czView attachment 3024811

Nchi haiongozwi kwa ubabe.
Ikishaomgozwa kibabe imeshafeli kabla hata haijaanza.

Nchi inahitaji mazungumzo. Maelewano. Kila awasilishe maslahi na changamoto zake ili suluhu ijadiliwe inapatikanaje.

Lakini ubabe ubabe. Ni mbaya

Ubabe ni mzuri kwa wahalifu na wanaokiuka sheria kimakusudi
 
Unataka kusema Mwigulu siyo "Qualified for the post" na siyo "technocrat"?

Tatizo letu linawezekana linaanzia kwenye Elimu za vyuo vikuu vyetu " a fish rots from the head down".
Mwigulu ni economist sio accountant, uelewa wake wa maswala ya administration za kodi atakama anazitunga yeye bila ya mhasibu au mtaalamu wa maswala ya kodi kumuelezea utekelezaji wake lazima utampiga chenga.

Na it’s not rocket siasa huko wizarani huyo mshauri hayupo kutokana na majibu ya waziri bungeni anapoongelea maswala ya kodi anapwaya.

Na huyo anaejibu wafanyabiashara Kitila ndio kabisa clueless. Ukitaka kuona hilo hapo anasema TRA wawataarifu wafanyabiashara nyaraka za kuwa nazo wakati hivyo vitu vipo kwenye VAT na Income Tax acts wafanyabiashara wenyewe hawataki kujiongeza.
 
Nchi haiongozwi kwa ubabe.
Ikishaomgozwa kibabe imeshafeli kabla hata haijaanza.

Nchi inahitaji mazungumzo. Maelewano. Kila awasilishe maslahi na changamoto zake ili suluhu ijadiliwe inapatikanaje.

Lakini ubabe ubabe. Ni mbaya

Ubabe ni mzuri kwa wahalifu na wanaokiuka sheria kimakusudi
Wahusika wametumia ubabe
 
Mwigulu ni economists sio accountant, uelewa wake wa maswala ya administration ya kodi atakama anazitunga yeye bila ya mhasibu lazima utampiga chenga.

Na it’s not rocket siasa huko wizarani huyo mtu hayupo kutokana na majibu hata bungeni anapoongelea maswala ya kodi anapwaya. Na huyo anaejibu wafanyabiashara kitila ndio kabisa clueless.
Mwigulu ni mpiga dili kama wengine
 
Lunatic wewe. Majeshi yetu yana kazi nyingi za muhimu kushinda huo upuuzi mliokua mnataka kuwambia wafanye ...hio list kuukaribia hata uwaziri mkuu sahau, mmoja ashakufa hapo. Ubabe hausaidii. Kalisha mapumbu hapo nyuma ya keyboard ukisubiria hizo rangi ambazo wataona wafanyabiashara
Ukiona hivyo ujue hajawahi kufanya biashara yoyote
 
Chalamila anapenda kulichafua Jeshi letu kwa kulihusisha na operesheni zake za kindezi. Wakati wa maandamano ya Chadema alitaka kulitumia Jeshi kuwatishia, leo tena anataka kulitumianJeshi kuwatishia wafanyabiashara wa Kariakoo, akome kabisa kulidhalilisha Jeshi letu kana kwamba halina kazi maalumu ya kufanya.
Akili ake haina akili
 
Hiyo ndio Taarifa ya sasa baada ya mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo unaoendelea

=======

Waziri wa Viwanda na Biashara, Kitila Mkumbo amesema wamekutana na wafanyabiashara wa Kariakoo na kutoka sehemu nyingine Tanzania wakiongozwa na mwenyekiti wa wafanyabiashara Kariakoo, Majid Mbwana.

Waziri Kitila amesema changamoto zilizofanya wafanyabiashara kutaka kufunga biashara zao zipo katika maeneo matano
  1. Changamoto ya ukosefu wa nyaraka hususan bandarini inayosababisha makadirio ya kodi yasiyo sahihi.
  2. Changamoto ya ukokotoaji ya kiwango cha kodi ambacho wanalipa.
  3. Suala la uwepo wa machinga katika maduka ambayo wanauza
  4. Suala la kamatakamata ambalo limekuwa likiendeshwa na mamlaka ya mapato(TRA)
  5. Changamoto kwenye sheria ya muswada wa fedha(Finance Bill)
Baada ya majadiliano ya kina Serikali imekubaliana mambo yafuatayo
  1. Kuanzia Julai 1, 2024 mamlaka ya mapato Tanzania itakuwa na mfumo mpya wa nyaraka ambao utatumika vizuri zaidi katika kuhakikisha wafanyabiashara wanapata makadirio ambayo ni sahihi.
  2. Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) inasitisha operesheni zake maarufu kama kamatakamata mpaka itakapokamilisha utaratibu huu ili kuweka mfumo mzuri zaidi wa kukusanya mapato.
  3. Suala la ukokotoaji wa kodi ni suala la kisheria, Serikali imelichukua na inaendelea kuliangalia ili kuboresha zaidi mfumo wa ukokotoaji wa kodi hususani bandarini.
  4. Kuendelea kuwapanga wamachinga kama ambavyo Rais aliagiza ili wakae katika maendeo sahihi ambayo hayaingilii biashara za watu wenye maduka ili kila mtu aweze kufaidika, wamachinga na wenye maduka katika eneo la Kariakoo.
  5. Serikali imewataarifu wafanyabiashara kuwa muswada wa sheria ya fedha(Finance Bill) ya mwaka 2024 bado haujapitishwa na sasa uko katika majadiliano bungeni na kamati ya bunge la bajeti imeita wananchi wote waweze kutoa maoni ikiwemo wafanyabiashara hivyo imewaalika yale maoni ambayo wanayo wayapeleke kwenye kamati ya Bunge na wabunge watazingatia maoni yao kabla sheria haijapitishwa.

Pia, Soma=> Mgomo wa Wafanyabiashara: Biashara zafungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024
Kitila Mkumbo ni waziri wa mipango na uwekezaji na siyo viwanda na biashara.Ashatu Kijaji ni waziri wa viwanda na biashara.
 
Imeisha hiyo kirahisi tu bila bughudha maduka yanafunguliwa

Back
Top Bottom