Serikali yasema haiwatambui wanaofanya kazi za ndani Saudi Arabia

Serikali yasema haiwatambui wanaofanya kazi za ndani Saudi Arabia

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Ali Jabir Mwadini, amesema hakuna utaratibu unaowatambua Watanzania waliokwenda kufanya kazi za ndani nchini Saudi Arabia.

Balozi Mwadini alisema hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanywa kwa njia ya video moja kwa moja kutoka Riyadh, Saudi Arabia.

“Nifafanue hili, fursa za ajira hapa Saudi Arabia zipo, na zilizofunguliwa na serikali ya Tanzania kuridhia na kuwataka wananchi wazichangamkie ni za udereva, uhudumu wa migahawa na hoteli. Sasa tumefungua kwa wauguzi na sekta ya afya, ila tunataka watu wapitie Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (Taesa),” alisema Balozi Mwadini.

Alisema hakuna Watanzania wanaofanya kazi za ndani nchini Saudi Arabia waliokwenda kwa kutumia utaratibu rasmi wa kiserikali na kuwezesha ubalozi kuwa na taarifa zao bali wanaofanya kazi hizo wamekwenda kinyemela.

“Kazi za ndani hatukufungua vibali kwa Watanzania kwenda kufanya na wala hatuna mikataba hiyo na hata kampuni zinazofanya uwakala wa wafanyakazi wanafahamu hilo kuwa hatukutoa vibali kwa kazi hiyo, ila tunasikia wapo ambao wanafanya kinyemela, sasa wakipata changamoto ndio ubalozi unaambiwa huyo ni Mtanzania,” alisema Balozi Mwadini.

Aliwasihi Watanzania kuepuka kudanganywa na kampuni au watu binafsi kuwatafutia kazi za ndani nchini humo na kuwasafirisha kinyemela kwa kujaza madhumuni mengine ya safari, kwani wakipata changamoto ni vigumu kuwatafuta walipo.

“Tutumie njia sahihi, fursa za ajira za wenye taaluma zipo ila fuateni utaratibu kuziomba na pia hakikisheni kampuni mnazoambiwa zinawatafutia kazi, zihakikini Taesa ili kuwa na uhakika na wakati mwingine kampuni hizo ndizo zinawadanganya kuhusu maslahi, wakifika na kukuta tofauti utata unaanza. Lakini wengine wanaondoka vizuri wakifika huko wanabadilisha mawazo na kutaka kufanya mambo mengine,” alisema Balozi Mwadini.

“Niwaambie kwa ujumla mazingira ya Saudi Arabia ni bora kuliko maeneo mengi. Kwa bahati mbaya masikio yanasikiliza habari mbaya. Hata mimi nilikuwa mzito kufungua soko la ajira kwa Watanzania. Wapo Watanzania 13, nilikutana nao baada ya kusikia changamoto zao na nilifuatilia na baadhi yao walirudi nyumbani kwa sababu walikuwa chini ya viwango vya kazi,” alisema Balozi Mwadini.

Alisema hadi sasa wapo zaidi ya Watanzania 1,200 wanaofanya kazi nchini humo ambao wanatambuliwa rasmi na idadi hiyo itaongezeka hivi karibuni baada ya kusainiwa kwa mkataba mwingine.

“Niwatake Watanzania wasikubali kutumia njia zisizo rasmi kuja kufanya kazi huko, kwa kutumia njia hizo wanaweza kukutana na changamoto, ila wakitumia mfumo rasmi, taarifa zao tunakuwa nazo na tunafuatilia na wanakuwa salama zaidi, ila kufanya kazi kinyemela sio jambo jema,” alisema Balozi Mwadini.

Chanzo: Habai Leo
 
TAESA mbona huwa hawatangazi?
Mfano kazi za Qatar World Cup kimya. Nchi ngumu sana hii
 
Hiyo ni sababu tosha ya kumrudisha Tanzania. Watanzania wanateseka na yeye anasema hivyo? Sasa ubalozi wake ni wa nini?

Sent from my SM-N986B using JamiiForums mobile app
Exactly mkuu, yaani hawa politicians wamelewa madaraka kwa kiasi kikubwa, ni wajibu wake kufuatilia kila raia wake, ni wajibu wake yeye kutoka pale ofisini ni kuingia mitaani ili kujua raia wake wako wapi na wanafanya nini, mpuuzi sana huyu balozi, mabalozi wetu wengi wamepewa vyeo hivi kama ahsante yao kwa kuwalinda politicians hawajui kabisa wajibu wao, ona balozi wa kenya hapo Namibia anaingia mitaani kutafuta raia wake na huu ndio wajibu wao, hii ni craze
 
Balozi akitoa kauli hajielewi
Balozi akikaa kimya anae dharau
Balozi akiamua kudeal na mambo yake utasikia balozi hatufai
Balozi akirudi kimya kimya kama Dr. Cassava utasikia huyo ni mwanasiasa anataka cheo
Balozi akiamua kutulia kama slowslow utasikia ameishiwa mbinu au demotion
Balozi akichangia mawazo yake kama Kagasheki utasikia akili zimeanza kumrudia
Aiseh miruzi mingi humpoteza Mbwa
 
Miaka mitatu iliyopita kulikua na Kiongozi wa CCM nadhani wa Mkoa wa Dar, sikumbuki vyema, alikua na taasisi feki ya kuwatafutia kazi Watanzania huko Kwa Waarabu, dah nimeisahau lle story
 
Nchi kama philippines,nepal,india serikali zao ndio zinapambana kiwatafutia kazi nje raia wake,huko gulf na ulaya wamejaa house girls wa kifilipino n.k,hapa kwetu kwenye tatizo la ajira hawataki watu wao watoke nje ya nchi kujitafutia riziki!
 
Balozi kaeleza vizuri kabisa,
Watu wanaenda Nchi za Watu kinyemela bila Serikali yao kujua hadi wanapopata matatizo,

Ameshauri wanaotaka kwenda huko wapitie kwenye Taasisi rasmi ya Ajira za huko ili watambulike kiserikali ambapo itakua rahisi kuwafatilia,

Kosa liko wapi hapo?
 
Miaka mitatu iliyopita kulikua na Kiongozi wa CCM nadhani wa Mkoa wa Dar, sikumbuki vyema, alikua na taasisi feki ya kuwatafutia kazi Watanzania huko Kwa Waarabu, dah nimeisahau lle story
Na ni miaka hiyo hiyo kiongozi fulani wa mkoa aliamua kuwasumbua wajane eti atawasaidia wakati zile ni kesi za kimahakama (maintenance courts)sio politics, hizi mahakama ndio zenye uwezo wa kutoa garnish dhidi ya kipato cha mzazi asiyewajibika na malezi ya mtoto.
Miaka mitatu iliyopita kulikua na Kiongozi wa CCM nadhani wa Mkoa wa Dar, sikumbuki vyema, alikua na taasisi feki ya kuwatafutia kazi Watanzania huko Kwa Waarabu, dah nimeisahau lle story
 
Hao wapuuz WA Taesa Wana programs za kuwatafutia watu kazi nchi za nje ? , Kuna taasis nyingine ni upuuz Tu na kuburst na kufuja Kodi za walalahoi watz.
Na huyu kenge anayejiita balozi kazi yake ni nini hapo kwenye ubalozi ?
 
Balozi akitoa kauli hajielewi
Balozi akikaa kimya anae dharau
Balozi akiamua kudeal na mambo yake utasikia balozi hatufai
Balozi akirudi kimya kimya kama Dr. Cassava utasikia huyo ni mwanasiasa anataka cheo
Balozi akiamua kutulia kama slowslow utasikia ameishiwa mbinu au demotion
Balozi akichangia mawazo yake kama Kagasheki utasikia akili zimeanza kumrudia
Aiseh miruzi mingi humpoteza Mbwa
Ni kweli kabisa,,yaani kwakuwa tuna uwezo wa kuongea basi tunachonga tuu! Ovyoo kabisa.
 
Wanataka balozi eti aingie mtaani akatafute watu walipoenda kufanya kazi kinyemela? Yaani ameenda Kuwakilisha inchi Kwa AJILI ya upuuzi huo?
 
Back
Top Bottom