Serikali yasitisha leseni ya kuchapisha na kusambaza Gazeti la Tanzania Daima kuanzia Juni 24, 2020

Serikali yasitisha leseni ya kuchapisha na kusambaza Gazeti la Tanzania Daima kuanzia Juni 24, 2020

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Serikali kupitia kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema kuwa kufuatia kusitishwa kwa lesini ya gazeti hilo, halitaruhusiwa kuchapishwa wala kusambazwa popote nchini au nje ya nchi

Serikali imebainisha kuwa uamuzi huo umetokana na kukithiri na kujirudia kwa makosa yanayokiuka sheria ya nchi na maadili ya uandishi wa habari na kuwa juhudi za kuwaonya na kuwaelekeza Wahariri wa gazeti hilo kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa hazijazaa matunda

Taarifa ya Serikali inasema Mkurugenzi wa wa Idara ya Habari, amefuta leseni ya gazeti hilo ikiwa ni baada ya kulionya kwa zaidi ya mara 10 huku gazeti lenyewe likilazimika kuomba radhi mara mbili kwa uvunjifu wa maadili ya Kitaaluma na Sheria za nchi ikiwemo kuchapisha habari za uongo, uchochozi na uzandiki

Aidha, Serikali imesema kwa mujibu wa Sheria Wachapishaji wa gazeti hilo wanayo fursa ya kuomba tena leseni kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari ili kuruhusiwa kurejea tena kuchapisha na kusambaza watakapoona wamejitafakari na kuwa tayari kufuata taratibu

3C5FA649-A028-4140-8893-4FB4781E30E2.jpeg


Soma pia > Gazeti la Tanzania Daima latoka kifungoni baada ya kufungiwa kwa siku 90
 
Back
Top Bottom