Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Status
Not open for further replies.
Kwa wale ndugu zetu mlio nunua viwanja kwa Fujo na kwa Bei mbaya Poleni sana hii imesha kula kwenu, ila tumaini lililo baki ni kwa nyie kuomba Mungu Kawambwa au Rizione aje awe Raisi ili aje afufue ndoto zenu na ndoto za Mkwere.
 
haha wageni wanafiki!!
 
Bandari tulizonazo alishindwa kuzisimamia zimekutwa na madudu kama si wadudu halafa mtu yule yule aliyeshindwa kusimamia Bandari ya Dar anataka kuijenga bandari nyingine Bagamoyo ni uwendawazimu..................
 
Bandari ya abagamoyo ni Jipu, Asante Rais Pombe kwa kulitumbua.
Unataka kima 50km kuwe na bandari??? Huku zilizokuwepo ukiziua?
 
Hapo wawekezaji walioingia mikataba watakula fedha ya bure kama hii habari ni ya ukweli.
Mikataba inaweza kupitiwa upya ili kuhamishia nguvu Mtwara na Tanga, labda gharama kidogo ya usumbufu kuliko gharama ya kuendelea ambayo nchi ingeingia
 
Kujengwa banadari mpya na ya kisasa kupisha bandari ya dar ambayo haina nafasi ni uharibifu?

Hakika shule mlienda kusomea ujinga.
Tatizo sio kujenga bandari mpya ya kisasa bandari hiyo inajengwa wapi...suala ni kuangalia vipaumbele
 
Bagamoyo kuwa mji wa biashara ndo basi tena
 

Unahitaji strong doses of antibiotics given intravenously!!
 
Foleni ya malori siyo ishu kubwa kwa sababu kuna bandari Kavu nje ya Dar, hata hapo tu Chalinze, Moro pia kuna eneo limetengwa, so tutengeneze hizi bandari kavu na tuimarishe bandari za Dar, Mtwara na Tanga ili malori ya kaskazini yaishie Chalinze na Tanga, yale ya kusini na kanda ya kati yaishie Moro

Hiyo Bagamoyo kwa kweli haina umuhimu wowote, JK na kundi lake walikuwa na maslahi binafsi tu
 
Home

Pitia hiyo link hapo juu

Bandari ya Bagamoyo haikuwa na mkopo. Ni wawekezaji wanawekeza na wanakula faida au hasara kutokana na mradi uliopo. Sema ukiusitisha ndiyo umeamua kuwapa faida ukipenda usipende.
 
Ni kweli haukuwa na mantiki yoyote. Lakini mmeshasaini mtaweza kuwalipa hao wawekezaji fidia ya kuvunja mkataba?
Tupo pamoja kwenye hili, nawe ni Mtanzania bila shaka! swali ni je, tungeendelea hasara yake ingekuwaje ukilinganisha na kutoendelea? na madhara yake ki- ecolojia, mazingira na factors zingine. Ninaamini kwa kutamka uboreshaji wa Mtwara na DSM, basi mikataba hiyo itarekebishwa ili kukidhi mahitaji hayo... Hatujapoteza kitu sana.
 
Nadhani ni bilion dola si ml dola
 
Unafikiri Ikulu watu wanaenda tu wapendapo? Mbona wewe hatukuoni kwenda?

Fikiri japo kiduchu ewe punguani.

Ikulu wanakwenda watu, kutubu makosa yao au kuomba msaada. At present both applies to the former Ikulu resident.
 



Katiba haina maana yoyote ile kwa nchi za Kiafrika, kwani Rwanda hawana Katiba mbona Kagame ameigeuza kwa kutumia mbinu za referendum? Burundi kwani hawana Katiba mbona Nkurunzinza ameibadilisha hata Kenya nao wameandika katiba mpya lkn kila siku wanaimegua kumuongezea Raisi Uhuru Kenyata madaraka leo hii yale original yaliyokuwepo kwenye Katiba ya Kenya yameshabadilishwa ili kukidhi matakwa ya watawala, kwa kifupi Katiba siyo jibu la nchi za Kiafrika bali Kiongozi mwenye maono kama Magufuli na Elimu, kama tukiwekeza kwenye Elimu tutakuwa na Taifa ambalo watu hawatakubali kuchezewa na wanasiasa, lkn Katiba haiendelezi nchi hata siku moja,bali ni Jamii na utamduni wa watu kwenye nchi husika ndiyo huendeleza nchi usisahau Uingereza haina Katiba iliyoandikwa lkn mbona wansihi vizuri tu? Nchi kama Singapore wana Katiba kama ya TanZania 100% na imewatoa hiyo Katiba kma yetu ktk third world country na leo ni highly developed country ina kipato cha juu klk Western European countries nyingi tu!
 
Hii ni habari nzuri sana mwaka huu ambayo nimeisoma. 22 trillion? Kujenga bandari mpya ambayo ingeendeshwa na wachina kwa miaka 50 kujilipa deni lao! Halafu kuna jinga moja linasupport huu mradi kisa?
Wanashindwa kupiga hayo mahesabu ya bandari kuendeshwa na mwekezaji miaka hiyo yote na kukabidhiwa chuma chakavu.
 
Sijui watu huwa mnajengaje hoja? Hayo mabavu anayoyatumia Magufuli kufanya hayo anayoyafanya kayatoa wapi kama si kwenye katiba. Uchaguzi Mwaka Jana ulifanyika kwa sababu Magufuli alitaka ufanyike au kwa kuwa Kikwete alichoka kuwa Rais? Magufuli anapoteua watu au kuhamisha huwa anafanya hivyo kwa kutumia mamlaka ambayo kayapata toka wapi kama siyo kwenye Katiba? Kasome vizuri ujue ni kwa nini wanasema Uingereza haina Katiba iliyoandikwa.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…