Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
haha wageni wanafiki!!Hapa sawa. Na aliyetoa amri ya kujengwa bandari hiyo ashitakiwe kwa matumizi mabaya ya ofisi na ubadhirifu wa mali ya umma. fedha nyingi sana ya walipa kodi imeshapotea kwenye ujinga huo.
Naanza kuona sababu za wageni wanafiki kutokukauka kwa Magufuli.
Haha aliyepita anaubora wake Na huyu piaKama itakuwa habari hizi ni za Uhakika, basi nitaamini kuwa sasa Tanzania tumepata Rais bora na siyo BORA Rais kama aliyepita.
Asisahau na kimeo chake cha MV DAR ES SALAAM. nacho ni kijipu uchungu japo sijui atakitumbuaje
Mikataba inaweza kupitiwa upya ili kuhamishia nguvu Mtwara na Tanga, labda gharama kidogo ya usumbufu kuliko gharama ya kuendelea ambayo nchi ingeingiaHapo wawekezaji walioingia mikataba watakula fedha ya bure kama hii habari ni ya ukweli.
Tatizo sio kujenga bandari mpya ya kisasa bandari hiyo inajengwa wapi...suala ni kuangalia vipaumbeleKujengwa banadari mpya na ya kisasa kupisha bandari ya dar ambayo haina nafasi ni uharibifu?
Hakika shule mlienda kusomea ujinga.
Bado sijaona hoja au mantiki ya kusitisha(kama habari hii sio udaku)
Kama issue ni fedha...basi tukusanye kodi kwa ajili ya ujenzi wa Bagamoyo port ambayo itakuwa ya kisasa kuliko zote katika pwani ya EAC na pia tukusanye fedha kwa ajili ya kuboresha hizo za MTWARA NA TANGA.
Kwa nini basi tujisifu tunakusanya kodi ikiwa tunaogopa kuwekeza??
Nakumbuka Mkapa alijenga uwanja wa Taifa mpya pembeni tu ya uwanja wa Uhuru ambao nao uliboreshwa na sikusikia mtu akisema Uwanja huo ukajengwe Mtwara au Moshi.
Tupo pamoja kwenye hili, nawe ni Mtanzania bila shaka! swali ni je, tungeendelea hasara yake ingekuwaje ukilinganisha na kutoendelea? na madhara yake ki- ecolojia, mazingira na factors zingine. Ninaamini kwa kutamka uboreshaji wa Mtwara na DSM, basi mikataba hiyo itarekebishwa ili kukidhi mahitaji hayo... Hatujapoteza kitu sana.Ni kweli haukuwa na mantiki yoyote. Lakini mmeshasaini mtaweza kuwalipa hao wawekezaji fidia ya kuvunja mkataba?
Nadhani ni bilion dola si ml dolaTunakataa mradi wa 10 M usd? , kama tatizo ni location basi upelekwe tanga, sio kusema tumeachana na huu mradi wa bagamoyo tukarabati tanga na mtwara, mbona tunachekesha, nilitegemea awaite wadau/wahisani wa bagamoyo port wafanye survey tanga na mtwara n bagamoyo then wachague wenyewe kimya kimya then waseme kama wamehamisha kwenda sehemu hizo na mradi utaanza mwezi kazaa kama ulivyopangwa , Hakuna nchi duniani kote wanaweza kataa mradi kama huu.
Unafikiri Ikulu watu wanaenda tu wapendapo? Mbona wewe hatukuoni kwenda?
Fikiri japo kiduchu ewe punguani.
Mradi wa Bagamoyo haukuwa na tija yoyote zaidi ya matakwa ya mtawala asiyeambilika.
Priority ya bandari za Tanzania ni:-
1. Dar 2. Tanga 3. Mtwara then zinafuata nyingine
Bandari ya Dar haijawa exploied to the maximum na tatizo la kuondoa na kuhifadhi containers lina ufumbuzi ambao haujafanyiwa kazi kwa makusudi ya watawala na wenza wao wafanyabiashara wanaotaka kuchuma fedha bila kufikiria.
World Bank walifadhili study ya kutengeneza master plan ya bandari zote Tanzania na solution zote zipo.
Tatizo kubwa la Dar Port ni miundombinu ya kuingia na kutoka lakini ufumbuzi wake ni kujenga dry port Kisarawe ambapo kuna eneo la kutosha kati ya reli ya kati na Tazara. Containers zote ta transit zingepelekwa Kisarawe kwa kutumia reli hizo mbili ambayo ingeondoa tayari msongamano barabarani. Mizigo yote ya transit ingekuwa cleared kutokea Kisarawe ambayo ingeunganishwa na road network nje ya Dar.
Terminal na storage za mafuta zingejengwa nje ya Dar pia na kuunganishwa kwa pipeline hivyo tusingeona fuel tankers ndani ya mji.
Ukijumlisha matatizo yote ya nchi hii unarudi pale pale kwenye habari ya KATIBA.
Sasa hivi kila kiongozi anafanya mambo anavyojisikia na hakuna anayeweza kumgusa.
Tatizo pia ni kwamba nchi haina strategic planning ingawa tunaaminishwa kuwa kuna tume ya mipango na mipango inapangwa kumbe hakuna kitu, ni bure kabisa!
Nchi inatakiwa iwe na long term plans kama 30-50 years katika nyanja zote za kiuchumi na kijamii ambazo zinatekelezwa katika shorter terms za 5 years. Ndivyo nchi ambazo zipo serious zinafanya na sio huu utumbo unaondelea hapa.
Kama Rais Magufuli kweli ana vision na nchi hii kwanza ashughulikie swala la katiba wakati anaendelea na hizi emergency measures anazofanya sasa. Then ndiyo afikirie stategic planning ya kuikwamua na kuindeleza hii nchi. Vinginevyo anapoteza nguvu na muda bure.
Hapa kazi tu!!Hapo wawekezaji walioingia mikataba watakula fedha ya bure kama hii habari ni ya ukweli.
Wanashindwa kupiga hayo mahesabu ya bandari kuendeshwa na mwekezaji miaka hiyo yote na kukabidhiwa chuma chakavu.Hii ni habari nzuri sana mwaka huu ambayo nimeisoma. 22 trillion? Kujenga bandari mpya ambayo ingeendeshwa na wachina kwa miaka 50 kujilipa deni lao! Halafu kuna jinga moja linasupport huu mradi kisa?
Sijui watu huwa mnajengaje hoja? Hayo mabavu anayoyatumia Magufuli kufanya hayo anayoyafanya kayatoa wapi kama si kwenye katiba. Uchaguzi Mwaka Jana ulifanyika kwa sababu Magufuli alitaka ufanyike au kwa kuwa Kikwete alichoka kuwa Rais? Magufuli anapoteua watu au kuhamisha huwa anafanya hivyo kwa kutumia mamlaka ambayo kayapata toka wapi kama siyo kwenye Katiba? Kasome vizuri ujue ni kwa nini wanasema Uingereza haina Katiba iliyoandikwa.Katiba haina maana yoyote ile kwa nchi za Kiafrika... kwa kifupi Katiba siyo jibu la nchi za Kiafrika bali Kiongozi mwenye maono kama Magufuli na Elimu, ... lkn Katiba haiendelezi nchi hata siku moja,bali ni Jamii na utamduni wa watu kwenye nchi husika ndiyo huendeleza nchi usisahau Uingereza haina Katiba iliyoandikwa lkn mbona wansihi vizuri tu? Nchi kama Singapore wana Katiba kama ya TanZania 100% na imewatoa hiyo Katiba kma yetu ktk third world country na leo ni highly developed country ina kipato cha juu klk Western European countries nyingi tu!