Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Status
Not open for further replies.


Mimi nimekwambia siwezi kuongelea mambo ya Kenya kwa maana sina uelewa sana ila kwa hapa kwetu Bandari ya Bagamoyo ni white elephant project yaani kupoteza tu fedha, fedha ambazo tungeweza kuzitumia kuboresha kwanza hizi zilizopo kabla ya kujenga Bandari mpya yaani kwanza Reli ijengwe upya ya kuunganisha Dar na Kigoma/Mwanza; Tanga- Moshi -Arusha mpaka Musoma na Mtwara corridor ambapo reli ya kutoka MT mpaka Ziwa Nyasa hivyo vifanyike kwanza, Maziwa yetu yote yapate Bandari kwanza, tayari zipo ni kukarabati tu kama vile Kigoma, Mwanza, Musoma, Bukoba na Nyasa na kama tukitumia hiyo bilioni 10 tutafanya mengi sana kwenye hilo baada ya hapo sasa baada ya kila kitu kuwa exhausted ndiyo kama kuna haja ya kujenga Bandari nyingine from scratch basi tufanye hivyo lkn siyo kinyume chake, huko ni kupoteza fedha!
 
Last edited:

Sina tatizo na ulichoandika kwa kiasi kikubwa, shida ni pale unapojenga hoja ya uwepo wa Magufuli kwenye cabinet ya Kikwete katika 'contetx' inayoashiria angeweza kukataa wakati mradi wa Bagamoyo unapitishwa! Nadhani hapa utakuwa unamuonea Magufuli kwa sababu kwanza hatujui kama huo mradi ulijadiliwa kwa kiwango gani kwenye cabinet wakati wa JK, pili, hatujui kama Magufuli alisema ndio au hapana na kama jibu lolote alilotoa (kama alitoa) lilikuwa na nguvu ya kubadili uamuzi wa utawala wa wakati huo, na tatu Bandari ilikuwa chini ya wizara nyingine ambayo Magufuli alikuwa hausiki nayo, unadhani ni wapi Magufuli alikosea?

Baada ya kusema hayo, sasa narudi tena kwenye maelezo yako hapo juu, ni hatua gani sahihi ulitaka RAIS Magufuli achukue dhidi ya Bandari ya Bagamoyo kwa kuzingatia uwepo wa Bandari zingine kama Dar, Tanga etc?

Kwenye red: Kama nimekuelewa vizuri ni kwamba unasema wakati wa Kampeni Magufuli alitumia Bandari ya Bagamoyo kama kauli mbiu ya kampeni. Bado unasimamia hii hoja?

Na pengine ningekuuliza jambo moja (na hii ni kutokana na threads zako nyingi hapa jamvini hasa wakati na baada ya kampeni, 2015) unadhani nani alifaa kuwa rais kati ya Magufuli na Lowassa? Uwe mkweli.
 
Kujengwa banadari mpya na ya kisasa kupisha bandari ya dar ambayo haina nafasi ni uharibifu?

Hakika shule mlienda kusomea ujinga.
Kama walienda kusomea ujinga basi wew ndo uliye kuwa mwalim wao. Maana naona unashindwa kuelewa kuwa ghalama za kuijenga hyo bandari ni kubwa kuzidi hata bajeti yetu ya taifa. $10bill=22Tilion kwa pesa zetu za madafu. Dahh sijui alie propose hii project alidhani wote wanakili za madafu😵
 


Na yote hayo Uchina waje kuwafanyia WatanZania buuureeee kwa lipi hasa? Au kwa sababu mnaongea kwa kubana pua?
 
Kama Ni kweli basi tunasema Inalilah waina ilahi rajiun.....
Laiti serikali imetenga fedha zake wenyewe kujenga mradi huu basi hii point ya hapa kazi tu ingekua na maana . Lakini mrfadi wa Bagamoyo unajengwa kwa pamoja kati ya Mfuko wa Hifadhi Wa Oman na Serikali ya China..Tanzania haitoi kitu kwa sasa.
sasa unapo simamisha hizi fedha za wachina na Wa Oman ndio watakupa kuendeleza Dar ?
Serikali inatakiwa kuendelea na mradi huu na vile vile kufanya juhudi za kuendeleza bandari ya Dar.

Bqagamoyo imechaguliwa kwa sababu ina kina kirefu zaid na uwanda mkuu ambao utfanya meli kubwa zaidi kufika Tanzania, Na lengo jengine ni kupunguza foleni na kuzidiwa kwa bandari ya Dar es salaam ambayo kutokana na kuwa ndogo kwa eneo ndio sababu kubwa ya kuanzisha hizi ICD Ambazo zimeleta tafrani katika kukusanya kodi.
bandari ya bagamoyo ni kubwa hakutakua na sababu za kuanzisha ICD.
 
Soma vizuri ndugu-Nmeanza na neno "Zile gharama ZINGETUMIKA kujenga hiyo UHT, kwa maana hiyo hazikutumika kujenga hiyo UHT line!
 

Mkuu kula tano.

Magufuli hakuwa na jinsi maana Kikwete alikwishaamua bandari ijengwe Bagamoyo ingawa hata washauri walipendekeza kuboreshwa kwa bandari za Dar, Mtwara na Tanga.

Lakini pia wazo la kusitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo hata Edward Lowasa alikuwa nalo na hata kwenye kampeni alisema kwamba angesitisha ujenzi huo na kuelekeza fedha kwenye bandari hizo tatu ili kuziboresha.

Hivyo pia si mbaya kutumia uzoefu wa Edo kwenye baadhi ya mambo muhimu kwenye maslahi ya taifa.

Hivyo utaona kwamba tulikuwa na kiongozi aliekuwa amezungukwa na washauri wabovu.
 
Huchoki na kampeni au ndiyo yale ya mvumilivu hula mbivu!

Uchaguzi umeisha au hufahamu kama kampeni za uchaguzi zimeisha!

Kwa kukusaidia hii ni serikali ya awamu ya tano inayojaribu kurekebisha pale ambapo serikali za awamu zilizopita hazikufanya suala lililotakiwa lifanywe au zilifanya kimakosa kutokana na mchanganuo wa priority kulingana na pato la taifa.

Kwani Rais Magufuli kuwepo kwenye kabineti ndiyo inamzuia kuchukua maamuzi ambayo ni tofauti na awamu zilizopita kulingana na mwelekeo wa serikali yake.

Kama katiba inaruhusu Rais kushitakiwa na Rais Magufuli akaamua kumkamata na kumshitaki Rais Kikwete, utakuja hapa na kuanza kusema mbona anamkamata Rais ambaye maamuzi yake aliyoyafanya hata Rais Magufuli alikuwa waziri? Au ndiyo macho ya makengeza kihoja katika kampeni zako?

Kwa nini hupigi kelele kuhusu kukamatwa au kufukuzwa kazi kwa wafanyakazi waliokuwa chini ya utawala wa Rais Kikwete kama wale wa TAKUKURU,TRA na TPA ambao walifanya madudu lakini serikali ya Rais Kikwete haikuwafanya lolote. Kwa nini husemi Rais Magufuli awaache tu kwa vile hata yeye alikuwepo kwenye serikali ambayo ilichukua maamuzi ya kutowafanya chochote.

Mbona US Secretary of Defense, Robert Gates alifanya kazi katika awamu ya Bush na Obama ambao walikuwa na malengo/sera tofauti katika masuala ya ulinzi hasa kuhusu combat mission nchini Afghanistan. Baada ya kuingia Obama, Sera kuhusu ulinzi ilibadilika na Gates akaendelea kuwa secretary of defense, kwa maana nyingine alichokuwa akikifanya wakati wa Bush Administration akaachana nacho.

Wake up man, hii ni awamu nyingine ya uongozi wa nchi na uchaguzi imamalizika siku ambayo Rais Magufuli aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania.
 
Last edited:
Ningependa kuona andiko la mpango wa biashara wa bandari ya Bagamoyo, hata executive summary tu- au hizo ni siri?
 
Mkuu, kwa kifupi nchi yetu imepoteza miaka 10 kusikiliza masimulizi ya mkwere badala ya kuendelea na safari ya maendeleo.
 

Mkuu serikali haijakurupuka kusitisha mradi huu.

Mradi haujafutwa bali umesitishwa.

Pia fedha za mradi huo bado hajitatolewa zote na ni wachina ndio walianza kutoa kiasi kwa ajili ya hatua za mwanzo, ila hao wa Oman bado hawajatoa hata senti.

Hivyo paper zote zimepitiwa na pameonekana inawezekana kusitisha kisheria.

Msidhani hii serikali ya sasa ni kuchekeanachekeana, hayo yalikwisha siku raisi wa awamu ya tano JJPM alipoapishwa.
 
Mkuu, kwa kifupi nchi yetu imepoteza miaka 10 kusikiliza masimulizi ya mkwere badala ya kuendelea na safari ya maendeleo.

Na hata wenzetu wazungu waloendelea wanaamini kwamba mtoto akifika miaka 10 na ukaona kuna kasoro, yaani hasikii, basi ndio ataendelea kuwa hivyo hadi anakuwa mtu mzima.

Ndio maana akifika miaka 16 anahesabiwa anaweza kujitegemea na mzazi kama ulikuwa unamtunzia akaunti yake benki, basi ni benki haohao ndio wanamtumia kadi mpya ya benki na si ile ya kawaida wa saving account ambayo wewe ndie uliekuwa ukiitunza.

Sasa miaka 10 imepita na tumekuja kugundua aina ya mtoto atakaekuja kuwa mtu mzima ni lazima tujitahidi kumtengeneza mapema kabla hajafika miaka 20.
 
Last edited:

Nakubaliana na wewe kiasi kuhusu bandari ya Tanga, ilivyo inatofauti kubwa na hii ya Dar au ile ya Mtwara. Kwamba meli inakua mbali na baadae mzigo unabebwa hadi nchi kavu, happ kuna shida kidogo!

Ama kuhusu Mtwara, iko vizuri sana tena sana. Kwa ufupi eneo kubwa la maji ya bahari kule Mtwara ni kina kirefu, achilia pale bandarini, ndiyo maana Mtwara siyo rafiki sana kuogelea. Hivyo kistratrjia, bandari ya Mtwara,Dar na Tanga kwa uchumi tulio nao, tungeanza kuziboresha kwanza. Na ndiyo ile ya Bagamoyo imesitishwa kwanza!
 
Soma vizuri ndugu-Nmeanza na neno "Zile gharama ZINGETUMIKA kujenga hiyo UHT, kwa maana hiyo hazikutumika kujenga hiyo UHT line!
Mimi nilishakuelewa na ndio maana nikasema kama zingetumika kwa UHT bado mahitataji ya ujenzi wa bomba la gas yangebaki pale pale... tungekwepa tu kwa muda lakini ungefika wakati lazima gas kama gas isafirishwe to commercial cities.
 

Ni kama vile rais wa awamu ya 4 allikua kwenye mashindano ya kimataifa ya kutafuta rahisi mbovu kuliko wote duniani, Wote tulijua hapa bagamoyo hakukuwa na sababu nyingine zaidi ya kuonekana mtoto wa mjini kafanya miracle, ndugu yetu katuletea, aibu sana sana sana na haya ni machache tu nasikia kama tungeyajua nusu ya hayo anayoyajua JPM na timu yake, tungetembea uchi barabarani kwa maandamano yasiyo na mwisho. Halafu kale katoto kake kashenzi kanathubutu kuita press conference eti kusema familia yao wanaandamwa, anadhani familia yao ni ya celebrity au mstaafu wakati ni ya mwizi mkuu na baba yake, Nisingeamini kama kuna mtu angeweza kulibetua jambo hili, huu ni mwanzo tuendeleeni kupeleka vijimambo vyote kama kawaida yetu, with detailed evidence, na zile roho za wote walioangamia kwa mateso yako, zikapige kelele mbele ya bwana
 
kukuonyesha jinsi gani watanzania wote isipokua wale walioko kwenye timu yako ya ufisadi iliyopigwa knock out na Rizwana na Ghalib Said Mohamed aliyebadili jina la Home Shopping Center kuwa GSM na Alosco ambapo serikali imekataa kwanza kabla ya kujitangaza mufilisi ngoja kwanza kunaendelea kupanga documents zetu za evidence, the whole country is overwhelmed with the Bagamoyo scandal, Msoga dance is now over,
 
Asante JPM unaona mbali sana bila kumuonea mtu yeyote aibu hata kama ni rais mstaafu kwa maamuzi yake mabovu.ilikuwa haiingii akilini hii hivi hakuwa na washauri au ni washauri wanafiki wa ndio mzee na kutomwambia ukweli bwana mkubwa aliyemaliza muda wake?haki ya Mungu wewe ni Rais bora utatuvusha na kutuondoa ktk aibu tuliyoanza kupata najuta kwanini sikukupa kura yangu.ushauri fanya kazi na wapinzani utajua mengi zaidi ya kuyafanyia kazi kurudisha heshima ya nchi hii.
 
Nashukuru kwa kuniondolea mashaka yangu kuhusu Tanga manake ile siku nilivyofika tu nikahisi hapa kuna shallow water! Kuhusu Mtwara, YES, ni natural habor!!

Hofu yangu kuhusu Mtwara ni moja tu! Kama zile cubic feet trillion kadhaa za gas ni kweli zipo Lindi na Mtwara basi biashara ya gas export ikichanganya ile bandari itakuwa busy sana! Na tusisahau, mimeli ya kusafirisha gas inakuwa mikubwa sana... sasa inaweza kuleta delays kwa meli zingine za kibiashara na nadhani inawezekana ndio sababu iliyomfanya Dangote kutaka kujenga bandari yake kwa kukwepa hizo hizo meli za mafuta!! Sasa kwa Mchina ambae lengo lake ni ku-speed up biashara zake ukanda huu halafu anakuja na mmeli wake; anakuta mimeli ya mafuta ime-cover... hawezi ku-favor sehemu kama hiyo hata siku moja.
 

Hapana, Dangote uamuzi wake haukutokana na udogo wa Bandari ya Mtwara, hata pale ilipo kwa sasa inaweza kuaccomodate 95% ya meli ya ukubwa wowote duniani,ingawa vifaa vya kupakulia siyo kama hivi vya Dar, ila kwa size ya meli ondoa shaka, ile bandari achana nayo, ni kuongeza tu urefu wa gati lakini meli kubwa uzionazo Dar zikifika Mtwara zinatua bila shida. Maboresho yakifanyika, hakuna sababu ya Bandari ya Dar kuelemewa!
 
Mnajaribu kila njia ku attack character lakini ikija kwenye issues za ukweli hamumuwezi.

Kikwete anadunda na ana rikodi ambayo mpaka sasa hakuna wa kabla yake aliyeifikia. Na ikitokea wa sasa akiifikia basi hilo pia ni chaguo lake, au mmesahau?
Jeshi la mtu mmoja. Kweli sikio la kufa halisikii dawa.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…