Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Status
Not open for further replies.
No, sisemi kwamba udogo wa bandari coz' hata kama ingekuwa ndogo si itapanuliwa. Ninachosema ni kwamba, biashara ya gas export ikichanganya, na kwa kuangalia ukubwa wa meli za mafuta na gas, basi kuna hatari pakawa busy sana na mara kwa mara pakawa occupied! Na zile meli zikianza kupakia mzigo, mnazisahau na ndio maana kwenye nchi nyingi kunakuwa na independent terminals kwa ajili ya meli za mafuta! Ujue hata hapa bandari ya Dar inatokea mara nyingi tu meli inaingia lakini inakuta gati ipo full occupied kwahiyo wanalazimika kusubiri!!
 
Mfano wako ni mzuri. Obama alImchukua Chuck kwasababu ya kupata mtu anAyeweza kusimamia transition period kati ya Obama na Bush NCHI ikiwa vitani, ikiwemo hatua ya kumtafuta Osama.

Ilionekana habari za OBL alizijua vema na kumwacha ilikuwa kuharibu mission.
Ndio maana baada ya tu ya kuuawa Chuck akawa amekamilisha mission pamoja na mengine

Sera ya Marekani kuhusu mambo ya kitaifa haibadiliki ni nadra sana .
Ndiyo maana suala la middle east limekwama licha ya Obama kuja na mtazamo mpya.

Kinachokwamisha ni ile sera ya kutowaacha Waisrael. Obama na Bibi Nyau wana bifu, ikifika security council Marekani wata veto azimio lolote kuhusu Israel. Kinachobadilika ni namna ya kutekeleza

Sera za Tanzania zinategemea nani yupo madarakani. Leo waziri anahoji elimu, hivi haumuoni tatizo hapo?
Hili la Bagamoyo halikuwa sera ilikuwa maoni tu ya mtu au watu kulingana na wakati

Msichotaka kusikia waliopo madarakani ndio walioujadili mradi , wengi walihoji,hawakusikilizwa, leo tukisema wao ni sehemu ya tatizo mnaingiza hoja za uchaguzi

Uchaguzi ulikwisha Rais amepatikana na serikali ipo. Kilichopo mbele yetu ni je wana maono gani kuhusu nchi tofauti na maono yaliotufikisha hapa? Mna haki ya kuishi kwa matumaini sisi tunaishi kwa ukweli.

Hamjibu hoja kuwa walikuwa katika cabinet, hawakufanya lolote kuhusu haya mauza uza ! Ni ukweli hata kama hamtaki kuusikia.

Leo mnataka tushangilie hatua tulizowahi kusema miaka mingi iliyopita, huu mradi haukufanyiwa tathmini. Hawakutusikiliza

Wanaweza kuchukua hatua zozote kulingana na sera zao, lakini ni wakati tuhoji kwanini mradi umefeli na wanatarajia nini tofauti.

Tukiendelea kushangilia haya mambo hayataisha.
Wanajua walikuwemo, watuambie kwanini mradi umefeli na tunaelekea kufanya nini. Hiyo ndio vision na mission si kuitikia tu.

Tukae chini tuwe na sera za kitaifa za pamoja kuhusu nchi yetu ikiwemo uchumi. Si muda wa reja reja hiyo ndiyo hoja kuu
Tutengeneze mfumo utakaozuia maoni ya watu kuwa yetu, mfumo utakaongozwa na utaalam na wataalam na si kubahatisha na siasa

Tusiambiwe tu mradi umefutwa, tuelezwe kwanini umefutwa, tatizo ni nini na kipi kinatarajiwa kufanyika tofauti
 
Mkuu amini nakwambia soon wataanikwa tu.au labda kwa heshima ya msoga anaweza kuwasitiri.
 
Hii kitu tuliipigia kelele sana mwaka jana. Kama ni kweli basi Watanzania tuwashukuru viongozi walioweza kustopisha mradi huu hapo Bagamoyo kwani ulikuwa na mlengo wa kufilisi fedha ya Mtanzania. Hongera Magufuli, Hongera waziri na hongereni wote wenye kuirudisha heshima ya Tanzania kwa watanzania na nje pia. Kikwete akitaka Bandari akajenge yake binafsi kwa fedha zake.
 
Hapo wawekezaji walioingia mikataba watakula fedha ya bure kama hii habari ni ya ukweli.
Jk Mwenyewe alikuja kustukia kaingizwa Mkenge ndio maana akaupotezea.... na kama angekuwa hajaupotezea ungekuwa kitambo walishaanza na pia pale Ufukweni karibu kuna Hoteli yake so ingebidi ivunjwe ipishe Bandari na watu wa bagamoyo walishachukia kuondolewa kwenye miradi yao ya pwani.... ila kama ndumba basi watu wa bagamoyo wanapiga mji mbaya sana wa bagamoyo nadhani pataendelea kuwa kama ulivyo mji wa kale kamwe hauwezi endelea kama bwana msoga kakaa miaka kumi bila kuendeleza mji na mkoa mzima
 
Ujenzi wake ulifikia hatua ipi? Mwenye picha yake tafadhali.
Kipindi kile niliweza tembelea Bagamoyo kuona mji ulivyo dah nilishangazwa kuoneshwa patakapojengwa hiyo Bandari yaani vilimwagwa vifusi kama kumi tu na mapande ya majabari kama sita hivi tu ndio kwisha habari jambo jema kama pesa hiyo tajwa haikutumika... ilikuwa njia ya kujipatia pesa bila jasho...
 
Yule jamaa wa Ms.oga alituingiza mkenge mambo mengi sana. Afadhali sana serikali imesitisha.
 
Kikwete alikuwa ananunua TV wakati hata nguzo ya umeme nyumbani kwake hakuna..!! Kama alivyo changia member mwingine. Huu ulikuwa uhuni wa kula fedha ya kusaini mkataba au labda ilikuwa ni muendelezo wa deal akijua kwamba mradi ule ungempa nafasi ya kuendelea kujipiga unene endapo Membe angekuwa Rais, ama ni ile miradi kivuli ya kuziba midomo kwa safari za Rais ikionekana kama vile alikuwa anasafiri kwa faida ya kuingiza wawekezaji. Dada yangu Faiza atakuwa na jibu zuri huenda akatusaidia.
 
Yule jamaa wa Ms.oga alituingiza mkenge mambo mengi sana. Afadhali sana serikali imesitisha.
Tumepoteza miaka 10, alitulostisha miaka 10. Inabidi tuimarishe taasisi zetu za kuisimamia na kuipinga serikali na kumpinga Rais, yani Bunge na Mahakama. Isiwe rahisi kwa mtu mmoja kuamua kutujengea li bandari la mabilioni karibu na kwao wakati halina tija.

....aseeee mkwere atakufa kwa presha, mpaka jpm aondokee !! ipo kazi....
right, haya mambo yameanza kumsumbua Kikwete personally. Alipanda jukwaani kukanusha madudu ya ukwepaji kodi wakati wa utawala wake. Nadhani ameshaanza kuona kwamba Magufuli hamfagilii sana, ndio maana juzi ikabidi aende yeye Ikulu badala ya Magufuli kumfata yeye Msoga kama mzee mstaafu.
 
Hiyo Bagamoyo yenyewe ni land locked, lazima ujenge reli kutoa mzigo!!
Mtwara port na Tanga strategicaly ziko well placed kuhudumia majilani zetu vizuri!!
 
Mkuu majibu ykuhusu ushiriki wa Magufuli, kuelewa mradi na kuutumia katika kampeni yanapatika bandiko 410 la mkuu JokaKuu au unaweza kusikiliza kupitia link hii

magufuli akemea uchochezi - YouTube

Mkuu Cabinet ndicho kikao kiuu cha ushauri cha Rais na serikali.
Mawaziri wakila kiapo wanaapa kutunza siri za vikao... Hakuna excuse fulani alikuwa wizara hii na yule ile, uamuzi wao ni wa pamoja 'collective responsibility''

Kama unanisoma vema na mabandiko yapo wazi kwa reference, kiongzi anyefanya vema Nampa big up, akiboronga Nampa failure. No more no less

Nafanya hivyo kwasababu naamini katika Taifa si mtu au vyama

Unapouliza Magufuli na Lowassa nani alifaa kuwa Rais, kwanini usiulize Dovutwa na Kuga Mziray wa TPP Maendeleo?

Unajaribu kuhamisha mjadala u-fit theory zako na si ukweli ulivyo.
Hapa nitakupa ukweli kwasababu nimeandika sana na rekodi zipo

Nimesema, nchi haiondoki ilipo ichini ya CCM. CCM si chama imegeuka genge. Nikaendelea, kama Dovutwa au Kuga Mzira wataiondoa CCM hilo ni heri.

Nilisema, haina maana ni viongozi wazuri, bali kuondoa CCM ni jambo muhimu kuliko jingine. lolote . Genge lililotufikisha hapa linageukaje kutuongoza tena?

Ushahidi wa miaka 10 ni haya tunayoyaona. Waliosadia kutufikisha hapa ndio hao waliounda serikali. Kamati kuu ya CCM na NEC ni ile ile iliyopitia mradi wa Bagamoyo kama chama tawala

Mh Nape Nnauye katibu mwenezi wa CCM, na waziri wa habari na maelezo amethibitisha maneno yangu. Ametamka nchi ilifikia mahali pa baya, hadharani

Ni huyu aliyetuambia nchi inaendelea vema chini ya CCM miaka 10, leo anaona alichokuwa hakijui akiwa ngazi za juu, iweje wengine muendelee na'' mgomo ''

Hoja hapa si Magufuli, ni jinsi nchi isivyo na mifumo ya kuweka maendeleo endelevu. Miradi ni kazi za kitaalamu si kisiasa.

Tuliwaambia Bagamoyo ni white elephant. Hawakutusikiliza , leo wanasemwa ni ''mashujaa'' baada ya kuona felia! eti tusiseme.

Wengine hatukuwepo katika siasa tulisimama na Taifa wao walishiriki vikao

Wana dhima ya kutueleza nini kimetokea. Kwanini mradi walioamini magufuli akemea uchochezi - YouTube umefeli.

HaTutataki habari za gizani kama ulivyoletwa bali maelezio, si ''cheap politics''

Miradi ya Kitaifa lazima iwe mbali na siasa. Tuweke mfumo miradi hiyo iendeshwe kwa utaalamu na uwazi.

Tujue nini kinaendelea si kujificha nyuma ya miogongo,waombe radhi.

Kwa mfano ningalikuwa hakimu mka wa mahakama na kesi ya namna hii ikaja , ningeweka makundi mawili 'wahalifu' na accomplices

Tushirikiane kuwauliza, walishiriki kutupeleka 'porini' wameona nini mbele na wanataka twende wapi

Nchi haitabadilika kama hatubadli mind set za ndiyoo bila ku reason.

Mind set za kudhani criticism ni dhambi, uzalendo ni kuvaa njuga na manyanga.

Mindset zisizoweza kuangalia mbali bali kila jambo kwa mtizamo wa siasa.
 
Mmh....huyo kachanganya,Chuck Hegel hakuwemo ktk utawala wa Bush, yule alikuwa ni Roberts Gates.
 
Big Port Afrika itasafirisha bidhaa gani? hakuna Uchumi Tanzania wala nchi zinazotuzunguka za kuweza kuitumia Bandari kama hiyo, hiyo ingekuwa ni white elephant project!

Mkuu bidhaa ni nyingi sana za kusafirisha na kuleta hapa, kitu ambacho hukijui, meli nyingi kubwa hushusha mizigo ya tanzania either south africa au mombasa kutokana na udogo wa bandari zetu na facilities zake. Tanzania kuna mizigo mingi sana kuliko ujuavyo, bado kuna uhitaji mkubwa sana wa bandari kubwa kuliko ya dar es salaam, tunahudumia nchi nyingi sana hapa ambazo wakati mwingine mizigo lazima iende Mombasa wakati tanzania ndio shortcut yao, pili mchina alihitaji kuitumia hiyo bandari kwa project zake Africa, na wote tunafahamu ni nani mwenye project nyingi Africa, mchina mfano anamigodi Zambia ila mizigo yote mikubwa anashusha na kusafirishia south africa kisa bandari ya dar ni congested na ndogo, Migodi yote ya Congo hasa maeneo katanga huhudumiwa na port za southafrica..huku shortcut yao ikiwa tz, udogo wa bandari yetu ndio shida,,, hujiulizi kwa nini kila siku lazima ipanuliwe?? na eneo pale sasa likeshaisha..
 
Binafsi naona kuna haja ya serikali kuunda chombo maalamu cha wataalamu mbali na bunge watakaoweza kukaa kwa pamoja na kuandaa mpango Mkakati Mkubwa wa kuinusuru Nchi.

Yaani tuandae Mikakati maalumu ya kututoa hapa tulipo, tujue tunaanza na lipi na tumalize na lipi in thousand years to come, watu watumike vizuri kuinusuru Nchi maana hakuna anayeijua Tanzania zaidi ya Mtanzania Mwenyewe.

Hizi porojo humu ndani hazitatufikisha kokote hapa kama Raisi akawa Mungu.
 
Binafsi naona kuna haja ya serikali kuunda chombo maalamu cha wataalamu mbali na bunge watakaoweza kukaa kwa pamoja na kuandaa mpango Mkakati Mkubwa wa kuinusuru Nchi.

Yaani tuandae Mikakati maalumu ya kututoa hapa tulipo, tujue tunaanza na lipi na tumalize na lipi in thousand years to come, watu watumike vizuri kuinusuru Nchi maana hakuna anayeijua Tanzania zaidi ya Mtanzania Mwenyewe.

Hizi porojo humu ndani hazitatufikisha kokote hata kama Raisi akawa Mungu.
 
Hii system akija Juma Kuwa raisi na yeye anaweka la kwake na mke wake hatufiki kokote, Hii ni Nchi na sio Nyumba inayoendeshwa na mume na mke, hii Nchi ni lazima iendeshwe na wananchi wenyewe, tuweke Mikakati Madhubuti kwa kadiri itakavyoonekana kuwa na Manufaa kwa taifa halafu hawa wanasiasa wawe watekelezaji tu bila kuwapa Mandate ya kusitisha aina yeyote ya Mikakati yetu kama Nchi.

Yeye aje atekeleze kisha Asepe atuachie Nchi yetu. FULLSTOP.
 
Hapo wawekezaji walioingia mikataba watakula fedha ya bure kama hii habari ni ya ukweli.

Kweli dada. Ndio maana tunashauri punguani aliyeshauri mradi huo ashitakiwe kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…