Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
No, sisemi kwamba udogo wa bandari coz' hata kama ingekuwa ndogo si itapanuliwa. Ninachosema ni kwamba, biashara ya gas export ikichanganya, na kwa kuangalia ukubwa wa meli za mafuta na gas, basi kuna hatari pakawa busy sana na mara kwa mara pakawa occupied! Na zile meli zikianza kupakia mzigo, mnazisahau na ndio maana kwenye nchi nyingi kunakuwa na independent terminals kwa ajili ya meli za mafuta! Ujue hata hapa bandari ya Dar inatokea mara nyingi tu meli inaingia lakini inakuta gati ipo full occupied kwahiyo wanalazimika kusubiri!!Hapana, Dangote uamuzi wake haukutokana na udogo wa Bandari ya Mtwara, hata pale ilipo kwa sasa inaweza kuaccomodate 95% ya meli ya ukubwa wowote duniani,ingawa vifaa vya kupakulia siyo kama hivi vya Dar, ila kwa size ya meli ondoa shaka, ile bandari achana nayo, ni kuongeza tu urefu wa gati lakini meli kubwa uzionazo Dar zikifika Mtwara zinatua bila shida. Maboresho yakifanyika, hakuna sababu ya Bandari ya Dar kuelemewa!
Mfano wako ni mzuri. Obama alImchukua Chuck kwasababu ya kupata mtu anAyeweza kusimamia transition period kati ya Obama na Bush NCHI ikiwa vitani, ikiwemo hatua ya kumtafuta Osama.Huchoki na kampeni au ndiyo yale ya mvumilivu hula mbivu!
Uchaguzi umeisha au hufahamu kama kampeni za uchaguzi zimeisha!
Kwa kukusaidia hii ni serikali ya awamu ya tano inayojaribu kurekebisha pale ambapo serikali za awamu zilizopita hazikufanya suala lililotakiwa lifanywe au zilifanya kimakosa kutokana na mchanganuo wa priority kulingana na pato la taifa.
Kwani Rais Magufuli kuwepo kwenye kabineti ndiyo inamzuia kuchukua maamuzi ambayo ni tofauti na awamu zilizopita kulingana na mwelekeo wa serikali yake.
Mbona US Secretary of Defense, Chuck Hagel alifanya kazi katika awamu ya Bush na Obama ambao walikuwa na malengo/sera tofauti katika masuala ya ulinzi hasa kuhusu combat mission nchini Afghanistan. Baada ya kuingia Obama, Sera kuhusu ulinzi ilibadilika na Hagel akaendelea kuwa secretary of defense, kwa maana nyingine alichokuwa akikifanya wakati wa Bush Administration akaachana nacho.
Wake up man, hii ni awamu nyingine ya uongozi wa nchi na uchaguzi imamalizika siku ambayo Rais Magufuli aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania.
Mkuu amini nakwambia soon wataanikwa tu.au labda kwa heshima ya msoga anaweza kuwasitiri.Mkuu,kama ulikuwepo kwenye akili yangu.Nami nafikiri vivyo hivyo.
Kama kweli JPM yupo serious katika hili,basi ahakikishe wahusika wote wanachunguzwa na ikibainika kuna ufisadi,basi wachukuliwe hatua kali.
Inawezekana watu walipiga deal liwe hivi huku wao wakineemeka kwa mikataba kusitishwa,sasa ni wakati wa mamlaka husika kuwachunguza wote waliohusika na kuingia mikataba ya huu mradi.
Hii kitu tuliipigia kelele sana mwaka jana. Kama ni kweli basi Watanzania tuwashukuru viongozi walioweza kustopisha mradi huu hapo Bagamoyo kwani ulikuwa na mlengo wa kufilisi fedha ya Mtanzania. Hongera Magufuli, Hongera waziri na hongereni wote wenye kuirudisha heshima ya Tanzania kwa watanzania na nje pia. Kikwete akitaka Bandari akajenge yake binafsi kwa fedha zake.The Construction of the 10 billion (about Sh22 trillion) Bagamoyo Port has been suspended, The Citizen has learnt. The government wants to focus instead, on improving the capacity, performance and efficiency of the Mtwara and Dar es Salaam ports.
The Minister for Works, Transport and Communications, Prof. Makame Mbarawa, confirmed yesterday that the construction of what would be the largest port in Africa has been suspended, not shelved to pave way for upgrading berths 13 and 14 as well as developing the Mtwara Port depending on the availability of Funds. The activities would take years to complete, the minister said because the process has to start from finding funding.
Source: THE CITIZEN
View attachment 315504
Jk Mwenyewe alikuja kustukia kaingizwa Mkenge ndio maana akaupotezea.... na kama angekuwa hajaupotezea ungekuwa kitambo walishaanza na pia pale Ufukweni karibu kuna Hoteli yake so ingebidi ivunjwe ipishe Bandari na watu wa bagamoyo walishachukia kuondolewa kwenye miradi yao ya pwani.... ila kama ndumba basi watu wa bagamoyo wanapiga mji mbaya sana wa bagamoyo nadhani pataendelea kuwa kama ulivyo mji wa kale kamwe hauwezi endelea kama bwana msoga kakaa miaka kumi bila kuendeleza mji na mkoa mzimaHapo wawekezaji walioingia mikataba watakula fedha ya bure kama hii habari ni ya ukweli.
Kipindi kile niliweza tembelea Bagamoyo kuona mji ulivyo dah nilishangazwa kuoneshwa patakapojengwa hiyo Bandari yaani vilimwagwa vifusi kama kumi tu na mapande ya majabari kama sita hivi tu ndio kwisha habari jambo jema kama pesa hiyo tajwa haikutumika... ilikuwa njia ya kujipatia pesa bila jasho...Ujenzi wake ulifikia hatua ipi? Mwenye picha yake tafadhali.
Kikwete alikuwa ananunua TV wakati hata nguzo ya umeme nyumbani kwake hakuna..!! Kama alivyo changia member mwingine. Huu ulikuwa uhuni wa kula fedha ya kusaini mkataba au labda ilikuwa ni muendelezo wa deal akijua kwamba mradi ule ungempa nafasi ya kuendelea kujipiga unene endapo Membe angekuwa Rais, ama ni ile miradi kivuli ya kuziba midomo kwa safari za Rais ikionekana kama vile alikuwa anasafiri kwa faida ya kuingiza wawekezaji. Dada yangu Faiza atakuwa na jibu zuri huenda akatusaidia.Mimi nimekwambia siwezi kuongelea mambo ya Kenya kwa maana sina uelewa sana ila kwa hapa kwetu Bandari ya Bagamoyo ni white elephant project yaani kupoteza tu fedha, fedha ambazo tungeweza kuzitumia kuboresha kwanza hizi zilizopo kabla ya kujenga Bandari mpya yaani kwanza Reli ijengwe upya ya kuunganisha Dar na Kigoma/Mwanza; Tanga- Moshi -Arusha mpaka Musoma na Mtwara corridor ambapo reli ya kutoka MT mpaka Ziwa Nyasa hivyo vifanyike kwanza, Maziwa yetu yote yapate Bandari kwanza, tayari zipo ni kukarabati tu kama vile Kigoma, Mwanza, Musoma, Bukoba na Nyasa na kama tukitumia hiyo bilioni 10 tutafanya mengi sana kwenye hilo baada ya hapo sasa baada ya kila kitu kuwa exhausted ndiyo kama kuna haja ya kujenga Bandari nyingine from scratch basi tufanye hivyo lkn siyo kinyume chake, huko ni kupoteza fedha!
Tumepoteza miaka 10, alitulostisha miaka 10. Inabidi tuimarishe taasisi zetu za kuisimamia na kuipinga serikali na kumpinga Rais, yani Bunge na Mahakama. Isiwe rahisi kwa mtu mmoja kuamua kutujengea li bandari la mabilioni karibu na kwao wakati halina tija.Yule jamaa wa Ms.oga alituingiza mkenge mambo mengi sana. Afadhali sana serikali imesitisha.
right, haya mambo yameanza kumsumbua Kikwete personally. Alipanda jukwaani kukanusha madudu ya ukwepaji kodi wakati wa utawala wake. Nadhani ameshaanza kuona kwamba Magufuli hamfagilii sana, ndio maana juzi ikabidi aende yeye Ikulu badala ya Magufuli kumfata yeye Msoga kama mzee mstaafu.....aseeee mkwere atakufa kwa presha, mpaka jpm aondokee !! ipo kazi....
Mkuu majibu ykuhusu ushiriki wa Magufuli, kuelewa mradi na kuutumia katika kampeni yanapatika bandiko 410 la mkuu JokaKuu au unaweza kusikiliza kupitia link hiiSina tatizo na ulichoandika kwa kiasi kikubwa, shida ni pale unapojenga hoja ya uwepo wa Magufuli kwenye cabinet ya Kikwete katika 'contetx' inayoashiria angeweza kukataa wakati mradi wa Bagamoyo unapitishwa! Nadhani hapa utakuwa unamuonea Magufuli kwa sababu kwanza hatujui kama huo mradi ulijadiliwa kwa kiwango gani kwenye cabinet wakati wa JK, pili, hatujui kama Magufuli alisema ndio au hapana na kama jibu lolote alilotoa (kama alitoa) lilikuwa na nguvu ya kubadili uamuzi wa utawala wa wakati huo, na tatu Bandari ilikuwa chini ya wizara nyingine ambayo Magufuli alikuwa hausiki nayo, unadhani ni wapi Magufuli alikosea?
Baada ya kusema hayo, sasa narudi tena kwenye maelezo yako hapo juu, ni hatua gani sahihi ulitaka RAIS Magufuli achukue dhidi ya Bandari ya Bagamoyo kwa kuzingatia uwepo wa Bandari zingine kama Dar, Tanga etc?
Kwenye red: Kama nimekuelewa vizuri ni kwamba unasema wakati wa Kampeni Magufuli alitumia Bandari ya Bagamoyo kama kauli mbiu ya kampeni. Bado unasimamia hii hoja?
Na pengine ningekuuliza jambo moja (na hii ni kutokana na threads zako nyingi hapa jamvini hasa wakati na baada ya kampeni, 2015) unadhani nani alifaa kuwa rais kati ya Magufuli na Lowassa? Uwe mkweli.
Mfano wako ni mzuri. Obama alImchukua Chuck kwasababu ya kupata mtu anAyeweza kusimamia transition period kati ya Obama na Bush NCHI ikiwa vitani, ikiwemo hatua ya kumtafuta Osama.
Ilionekana habari za OBL alizijua vema na kumwacha ilikuwa kuharibu mission.
Ndio maana baada ya tu ya kuuawa Chuck akawa amekamilisha mission pamoja na mengine
Sera ya Marekani kuhusu mambo ya kitaifa haibadiliki ni nadra sana .
Ndiyo maana suala la middle east limekwama licha ya Obama kuja na mtazamo mpya.
Kinachokwamisha ni ile sera ya kutowaacha Waisrael. Obama na Bibi Nyau wana bifu, ikifika security council Marekani wata veto azimio lolote kuhusu Israel. Kinachobadilika ni namna ya kutekeleza
Sera za Tanzania zinategemea nani yupo madarakani. Leo waziri anahoji elimu, hivi haumuoni tatizo hapo?
Hili la Bagamoyo halikuwa sera ilikuwa maoni tu ya mtu au watu kulingana na wakati
Msichotaka kusikia waliopo madarakani ndio walioujadili mradi , wengi walihoji,hawakusikilizwa, leo tukisema wao ni sehemu ya tatizo mnaingiza hoja za uchaguzi
Uchaguzi ulikwisha Rais amepatikana na serikali ipo. Kilichopo mbele yetu ni je wana maono gani kuhusu nchi tofauti na maono yaliotufikisha hapa? Mna haki ya kuishi kwa matumaini sisi tunaishi kwa ukweli.
Hamjibu hoja kuwa walikuwa katika cabinet, hawakufanya lolote kuhusu haya mauza uza ! Ni ukweli hata kama hamtaki kuusikia.
Leo mnataka tushangilie hatua tulizowahi kusema miaka mingi iliyopita, huu mradi haukufanyiwa tathmini. Hawakutusikiliza
Wanaweza kuchukua hatua zozote kulingana na sera zao, lakini ni wakati tuhoji kwanini mradi umefeli na wanatarajia nini tofauti.
Tukiendelea kushangilia haya mambo hayataisha.
Wanajua walikuwemo, watuambie kwanini mradi umefeli na tunaelekea kufanya nini. Hiyo ndio vision na mission si kuitikia tu.
Tukae chini tuwe na sera za kitaifa za pamoja kuhusu nchi yetu ikiwemo uchumi. Si muda wa reja reja hiyo ndiyo hoja kuu
Tutengeneze mfumo utakaozuia maoni ya watu kuwa yetu, mfumo utakaongozwa na utaalam na wataalam na si kubahatisha na siasa
Tusiambiwe tu mradi umefutwa, tuelezwe kwanini umefutwa, tatizo ni nini na kipi kinatarajiwa kufanyika tofauti
Thank you sirMmh....huyo kachanganya,Chuck Hegel hakuwemo ktk utawala wa Bush, yule alikuwa ni Roberts Gates.
Big Port Afrika itasafirisha bidhaa gani? hakuna Uchumi Tanzania wala nchi zinazotuzunguka za kuweza kuitumia Bandari kama hiyo, hiyo ingekuwa ni white elephant project!
Hapo wawekezaji walioingia mikataba watakula fedha ya bure kama hii habari ni ya ukweli.