John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Serikali imetangaza kuongeza mwaka mmoja mbele kabla ya kuanza kutumika sheria ya elimu kuanzia ngazi ya Stashahada kwa waandishi wa habari kwa mujibu wa Sheria ya Huduma ya Habari ya Mwaka 2016.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari na Mawasiliano ya Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alipokuwa akizungumza na wahariri wa Habari makao makuu ya TCRA, leo Alhamisi Februari 10, 2022.
“Mimi nikiwa Waziri, nilisimamia ile Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari, mazingira ya wakati kule na sasa ni tofauti, mwaka 2016 na 2022 ni tofauti.
“Hili la elimu tutoe mwaka mmoja ili tuone nini cha kufanya huko mbele.
“Niwaombe wanahabari tuaminiane, mimi mwandishi wa habari mwenzenu. Hiki ninachokieleza ndicho kipo kwenye moyo wa Rais Samia na uelekeo wa serikali ya awamu ya sita, tufanye kazi Pamoja.
“Tutatumia busara, tutashikamana kwa pamoja na nia ya Serikali ya awamu ya sita ni nzuri. Mimi najua tulikotoka, wakati mwingine safari ya mabadiliko ni ndefu. Tunaomba tuaminiane tutafika.”
Awali, sheria hiyo ilikuwa ianze kutumika Desemba mwaka 2021, kwa waandishi kuwa na elimu kuanzia ngazi ya stashahada.