Serikali yatangaza bei ya kikomo ya Sukari; ipo kati ya Tsh. 2,600 na Tsh. 3,200 kwa kilo kutegemea na Mkoa

Serikali imetangaza bei ya ukomo ya Sukari kwa rejareja katika Mikoa yote nchini, ambapo kwa Dar es Salaam itauzwa kwa Shilingi 2,600 kwa Kg 1, Mbeya 3,000, Mwanza, Dodoma na Shinyanga 2,900, Kigoma 3,200, Arusha na Kilimanjaro ni 2,700, Kagera na Mara ni 3,000.

Aidha kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara, Sukari itauzwa kwa Sh.2,800, Rukwa, Katavi, Ruvuma itauzwa kwa Sh 3,200. Njombe, Geita, Tabora, Singida, Iringa na Simiyu itauzwa kwa Sh.2900 na kwa Manyara, Tanga, Pwani na Morogoro itauzwa kwa Sh 2,700 na Songwe ni Sh.3,000.
Kwa maana hiyo serikali imepandisha bei ya sukari rasmi .

Duh aliyetuletea hii serikali Mungu anamuona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri wa kilimo mh Hasunga ametangaza bei elekezi ya sukai kwa mikoa yote hapa nchini na kwamba mfanyabiashara yoyote atakayepandisha bei hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Bei ya kilo moja ya sukari kwa mkoa wa Dsm ni sh 2600 na Kigoma sh 3200.

Source ITV habari
 
Kwa naneno mepesi serikali imeondoa ruzuku ili sukari iwe bei moja nchi nzima..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kulikuwa hakuna sababu ya kuwa na bei tofauti kwa kila mkoa. Mbona viwanda vikizalisha bei inakuwa sawa kote. Serikali inaumiza walaji na kuwanufaisha wazalishaji.
 
Serikali imetangaza bei ya ukomo ya Sukari kwa rejareja katika Mikoa yote nchini, ambapo kwa Dar es Salaam itauzwa kwa Shilingi 2,600 kwa Kg 1, Mbeya 3,000, Mwanza, Dodoma na Shinyanga 2,900, Kigoma 3,200, Arusha na Kilimanjaro ni 2,700, Kagera na Mara ni 3,000.

Aidha kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara, Sukari itauzwa kwa Sh.2,800, Rukwa, Katavi, Ruvuma itauzwa kwa Sh 3,200. Njombe, Geita, Tabora, Singida, Iringa na Simiyu itauzwa kwa Sh.2900 na kwa Manyara, Tanga, Pwani na Morogoro itauzwa kwa Sh 2,700 na Songwe ni Sh.3,000.
Sisi tunaokaa mwishoni mwa Tanzania tunduma tunajua sukari ukiletewa nyumban kg 1 ni sh 2000 ukifuata dukani sh1750 kwa kg1 mnaokaa makao makuu endeleeni kununua ndo bei yake hiyo msilalamike

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom