Serikali yatangaza tenda ya ujenzi wa mwendokasi kutoka Maktaba ya Taifa Posta- Mwenge- Ubungo-Tegeta

Tajiri Kichwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2017
Posts
9,021
Reaction score
22,016
Nimeona katika gazeti Serikali inatafuta kampuni ya ujenzi wa barabara ya mwendokasi pamoja na vituo vyake.

Kutoka maktaba ya taifa to Mwenge/Ubungo 13.5 km utakuwa na vituo visivyopungua 20

Kutoka Mwenge to Tegeta Dawasa 15.63 km itakua na vituo visivyopungua 19.

fa28ef8e-891f-4fa0-90eb-6cdd7bec9486.jpg

Ujenzi wa phase 4 katika jiji la Dar es Salaam unasimamiwa Na tanroads. Ngoja tuone pindi utakapokamilika.

Ila ingewafaa wasitumie yule mkandarasi wa Mbagala to Kariakoo na Mbagala tu Magomeni. Naona design na ujenzi huko chini kidogo ya viwango tofauti na hii phase one ya mwendokasi tunayotumia.
 
Barabara ya Mwenge tunaenda kuijenga mara ya tatu sasa ndani ya kipindi kifupi. Tulijenga kwa pesa za maadhimisho ya Uhuru, tukaijenga tena kwa ufadhili wa Japan, tunaenda tena kuijenga kwa pesa za mkopo. Ukosefu wa mipango na watu kutafuta asilimia zao.
 
Barabara ya Mwenge tunaenda kuijenga mara ya tatu sasa ndani ya kipindi kifupi. Tulijenga kwa pesa za maadhimisho ya Uhuru, tukaijenga tena kwa ufadhili wa Japan, tunaenda tena kuijenga kwa pesa za mkopo... Ukosefu wa mipango na watu kutafuta asilimia zao...
Huoni Kati kati tayari kuna nafasi ya mwendokasi
 
Wamrudishe strabag zaidi ya hapo ni upigaji tu, na kwanini tuhangaike wakati tunatakiwa kujifunza kwa walioendelea. Ujerumani ndio nchi inayoongoza kwa miundombinu mizuri duniani. Lakini kwa kuwa watu wanaangalia percent zao utaona anapewa Mchina.

Hii nchi inahitaji kuongozwa na mtu mwenye kichwa kama changu. Halafu kwa nini wanahangaika wakati hii miradi mingine haijaisha bado. Pia ni wakati wa kuangalia mbadala wa petrol, mwendokasi waweke za kutumia umeme au gesi.
 
Barabara ya Mwenge tunaenda kuijenga mara ya tatu sasa ndani ya kipindi kifupi. Tulijenga kwa pesa za maadhimisho ya Uhuru, tukaijenga tena kwa ufadhili wa Japan, tunaenda tena kuijenga kwa pesa za mkopo... Ukosefu wa mipango na watu kutafuta asilimia zao...

Ili nalo linashangaza. Au teyari walikua wameshachora mchoro. Maana kuna space katikati walikua wanaacha.
 
Kwa moyo mweupe kabisa waachane na haya makitu, tumalize miradi iliyopo! Nguvu kubwa itumike kuwaingiza Watanzania katika kilimo cha kisasa, kwa kutayarisha miundo mbinu ya kilimo yaani rural roads zote, makambi ya ajira za wakulima,ili vijana waende huko kuendesha kilimo chini ya usimamizi fulani hata wa makaburu, huku tukialika agro-industry companies, kubwa kubwa.
 
Barabara ya Mwenge tunaenda kuijenga mara ya tatu sasa ndani ya kipindi kifupi. Tulijenga kwa pesa za maadhimisho ya Uhuru, tukaijenga tena kwa ufadhili wa Japan, tunaenda tena kuijenga kwa pesa za mkopo... Ukosefu wa mipango na watu kutafuta asilimia zao...

Pia barabara ya tegeta kwenda mwenge kulikua na ujenzi wa service road hivi karibuni. Mfano maeneo ya makonde, goig, africana ambazo nahisi zitabomolewa tena.
 
Nimeona katika gazeti Serikali inatafuta kampuni ya ujenzi wa barabara ya mwendokasi pamoja na vituo vyake.

Kutoka maktaba ya taifa to Mwenge/Ubungo 13.5 km utakuwa na vituo visivyopungua 20

Kutoka Mwenge to Tegeta Dawasa 15.63 km itakua na vituo visivyopungua 19.

View attachment 2363211

Ujenzi wa phase 4 katika jiji la Dar es Salaam unasimamiwa Na tanroads. Ngoja tuone pindi utakapokamilika.

Ila ingewafaa wasitumie yule mkandarasi wa Mbagala to Kariakoo na Mbagala tu Magomeni. Naona design na ujenzi huko chini kidogo ya viwango tofauti na hii phase one ya mwendokasi tunayotumia
Mshana Jr, hebu tufanye application ya hii kandarasi aisee.

Wacha tuanze kuomba miradi mikubwamikubwa
 
Barabara ya Mwenge tunaenda kuijenga mara ya tatu sasa ndani ya kipindi kifupi. Tulijenga kwa pesa za maadhimisho ya Uhuru, tukaijenga tena kwa ufadhili wa Japan, tunaenda tena kuijenga kwa pesa za mkopo... Ukosefu wa mipango na watu kutafuta asilimia zao...
Wacha utilatila na wewe! Wanakwambia ni mwendokasi wewe unafanya reference ya barabara ya kawaida? Watu wengine mkoje?
 
Nimeona katika gazeti Serikali inatafuta kampuni ya ujenzi wa barabara ya mwendokasi pamoja na vituo vyake.

Kutoka maktaba ya taifa to Mwenge/Ubungo 13.5 km utakuwa na vituo visivyopungua 20

Kutoka Mwenge to Tegeta Dawasa 15.63 km itakua na vituo visivyopungua 19.

View attachment 2363211

Ujenzi wa phase 4 katika jiji la Dar es Salaam unasimamiwa Na tanroads. Ngoja tuone pindi utakapokamilika.

Ila ingewafaa wasitumie yule mkandarasi wa Mbagala to Kariakoo na Mbagala tu Magomeni. Naona design na ujenzi huko chini kidogo ya viwango tofauti na hii phase one ya mwendokasi tunayotumia
Kwahiyo kipande cha Morocco Mwenge kitavunjwa kwa mara nyingine
  • Wakati wa JK kilivunjwa kikaongezwa lane ya 3
  • Mwendazake akavunja na kujenga kwa fedha ya Uhuru
  • Majuzi majuzi kilivunjwa na kuwekwa mitaro mipana chini ya ardhi
  • Na sasa kinavunjwa kuweka miundombinu ya mwendokasi
 
Back
Top Bottom