Serikali yatangaza tenda ya ujenzi wa mwendokasi kutoka Maktaba ya Taifa Posta- Mwenge- Ubungo-Tegeta

Serikali yatangaza tenda ya ujenzi wa mwendokasi kutoka Maktaba ya Taifa Posta- Mwenge- Ubungo-Tegeta

Kwahiyo kipande cha Morocco Mwenge kitavunjwa kwa mara nyingine
  • Wakati wa JK kilivunjwa kikaongezwa lane ya 3
  • Mwendazake akavunja na kujenga kwa fedha ya Uhuru
  • Majuzi majuzi kilivunjwa na kuwekwa mitaro mipana chini ya ardhi
  • Na sasa kinavunjwa kuweka miundombinu ya mwendokasi
Ile nafasi kubwa katikati ulifikiri ni mapambo?
 
Barabara ya Mwenge tunaenda kuijenga mara ya tatu sasa ndani ya kipindi kifupi. Tulijenga kwa pesa za maadhimisho ya Uhuru, tukaijenga tena kwa ufadhili wa Japan, tunaenda tena kuijenga kwa pesa za mkopo... Ukosefu wa mipango na watu kutafuta asilimia zao...
Ni kweli tunakwenda kujenga kwa mara nyingine kwa pesa ya mkopo ila bila kuathiri ile tuliyojenga kwa fedha zilizotangulia.... itajengwa katikati bila kuvunja ile ya pembeni
 
Huu mradi unavyopuyanga hivi bado wanaendelea tu kuongeza sehemu zingine.Si bora watanue tu barabara ziwe nyingi lakini si BRT maana wameonesha ufanisi wao ni sifuri kabisa.kama serikali mnania ya kurahisisha usafiri Dsm ongezeni barabara ziwe sita au nane kama nafasi inaruhusu na siyo hiyo mi BRT ambayo imeonesha uendeshaji wake ulivyo wa ovyo.
 
Barabara ya Mwenge tunaenda kuijenga mara ya tatu sasa ndani ya kipindi kifupi.
Ukipita ile njia utaona kabisa kuwa mradi wa awali ulilenga njia za magari ya kawaida na kwa mpango wa mbele wakaacha nafasi ya ujenzi wa Barabara ya mwendokasi!
tuwe realistic tusibeze kila jambo, Mradi kama wa mwendokasi una mahitaji yake ya msingi ili ku- accomodate!
 
Madesa yamekuharibu unaamini kila kitu ni 'kusomea' tu, bure kabisa.
Ulipoudharau na kuubeza ushauri na kuutukuza uchawi nilikuona ni empty head...... ushauri ni elimu Na lazima uende shule, labda huo ushauri wenu wa fitna
 
Barabara ya Mwenge tunaenda kuijenga mara ya tatu sasa ndani ya kipindi kifupi. Tulijenga kwa pesa za maadhimisho ya Uhuru, tukaijenga tena kwa ufadhili wa Japan, tunaenda tena kuijenga kwa pesa za mkopo... Ukosefu wa mipango na watu kutafuta asilimia zao...
Replica hii habari imenishtua na kunishangaza

Serikali ya wapigaji kila wakati wanawaza fursa
 
Kwahiyo kipande cha Morocco Mwenge kitavunjwa kwa mara nyingine
  • Wakati wa JK kilivunjwa kikaongezwa lane ya 3
  • Mwendazake akavunja na kujenga kwa fedha ya Uhuru
  • Majuzi majuzi kilivunjwa na kuwekwa mitaro mipana chini ya ardhi
  • Na sasa kinavunjwa kuweka miundombinu ya mwendokasi
😅😅😅
 
Nimeona katika gazeti Serikali inatafuta kampuni ya ujenzi wa barabara ya mwendokasi pamoja na vituo vyake.

Kutoka maktaba ya taifa to Mwenge/Ubungo 13.5 km utakuwa na vituo visivyopungua 20

Kutoka Mwenge to Tegeta Dawasa 15.63 km itakua na vituo visivyopungua 19.

View attachment 2363211

Ujenzi wa phase 4 katika jiji la Dar es Salaam unasimamiwa Na tanroads. Ngoja tuone pindi utakapokamilika.

Ila ingewafaa wasitumie yule mkandarasi wa Mbagala to Kariakoo na Mbagala tu Magomeni. Naona design na ujenzi huko chini kidogo ya viwango tofauti na hii phase one ya mwendokasi tunayotumia
Hutaki wamtumie SINOHYDRO? hahaha Wakati ndio hao hao wamepewa na kile kipande kingine Cha Reli!! Sijui hawa jamaa wanatumia dawa Gani, Wana miradi mingi Tanza-nia ila yote haikosi kasoro
 
KWA MOYO MWEUPE KABISA WAACHANE NA HAYA MAKITU,TUMALIZE MIRADI ILIYOPO!,NGUVU KUBWA ITUMIKE KUWAINGIZA WATANZANIA KATIKA KILIMO CHA KISASA,KWA KUTAYARISHA MIUNDO MBINU YA KILIMO YAANI RURAL ROADS ZOTE,MAKAMBI YA AJIRA ZA WAKULIMA,ILI VIJANA WAENDE HUKO KUENDESHA KILIMO CHINI YA USIMAMIZI FULANI HATA WA MAKABURU,HUKU TUKIALIKA AGRO-INDUSTRY COMPANIES,KUBWA KUBWA.
Ccm hii hawatokaa wakusikie. Sio kipaumbele chao kuinua maisha ya wananchi.
 
Mi nafikiri tunarudi nyuma. Serikali iwekeze kwenye haya madude - Electrical Trams gharama za kuendesha ziko chini hata nauli itakuwa chini vinginevyo tuweke mabasi ya umeme.
1663741139842.png
 
Wamrudishe strabag zaidi ya hapo ni upigaji tu....na kwanini tuhangaike wakati tunatakiwa kujifunza kwa walioendelea....Ujerumani ndio nchi inayoongoza kwa miundombinu mizuri duniani. Lakini kwa kuwa watu wanaangalia percent zao utaona anapewa mchina.

Hii nchi inahitaji kuongozwa na mtu mwenye kichwa kama changu. Halafu kwa nini wanahangaika wakati hii miradi mingine haijaisha bado.... Pia ni wakati wa kuangalia mbadala wa petrol, mwendokasi waweke za kutumia umeme au gesi.
Sioni sababu kuanza mrad huu Sasa HV wangeanza by 2030

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Hutaki wamtumie SINOHYDRO? hahaha Wakati ndio hao hao wamepewa na kile kipande kingine Cha Reli!! Sijui hawa jamaa wanatumia dawa Gani, Wana miradi mingi Tanza-nia ila yote haikosi kasoro

Haha itakua ni wavumilivu tukiwa tunawalipa kidogo kidogo. Tunaweza kulaza deni.
 
Back
Top Bottom