City train ndio ingekuwa suluhisho la usafiri Jijini Dar, haya mabasi hayawezi kabisa kutatua kero ya usafiri Dar..
Njia nzote hizi za mwendo kasi ingetakiwa iwe train zote, usingeona foleni au watu wamejazana katika vituo kusubiria usafiri..
Majiji yote makubwa duniani, city train ndio suluhisho la usafiri wa majiji hayo, mfano kwa Africa, Addis Ababa, Ethiopia, au Joburg, S.A, ila Ulaya nchi nzima ni train, US train ndio kila kitu na ujenzi wake usingekuwa tofauti na huu wa mwendokasi, tena kuna train za majiji zinabeba watu 2000 kwa mkupuo, yaani Tegeta asubuhi unapeleka 3 tu kwenda na kurudi, Mbagala 3 tu kwenda na kurudi, Kibaha Posta unapeleka 4 tu kwenda na kurudi foleni ya watu kwishaa kwa asubuhi, jioni zinarudia hivyo, maana train 3 kwa route moja inabeba karibia watu 6,000 zikirudi second round watu 12,000..
Yaani haya mabasi hayana msaada kulinganisha na investments inayofanywa, foleni, watu kubanana, watu kukosa usafiri, haijapungua
Train za mijini kama ile ya Mwakyembe, inabeba watu hadi 3,000 kwa mkupuo, tokea Pugu, Gongo la Mboto to Posta.. Ikirudi mara ya pili foleni ya watu imeisha, sasa je tungeweka train kama 15 hapa mjini za aina ile, wala usingeona shida za usafiri during peak hours, asubuhi au njioni