Serikali yatangaza tenda ya ujenzi wa mwendokasi kutoka Maktaba ya Taifa Posta- Mwenge- Ubungo-Tegeta

Serikali yatangaza tenda ya ujenzi wa mwendokasi kutoka Maktaba ya Taifa Posta- Mwenge- Ubungo-Tegeta

Kwahiyo kipande cha Morocco Mwenge kitavunjwa kwa mara nyingine
  • Wakati wa JK kilivunjwa kikaongezwa lane ya 3
  • Mwendazake akavunja na kujenga kwa fedha ya Uhuru
  • Majuzi majuzi kilivunjwa na kuwekwa mitaro mipana chini ya ardhi
  • Na sasa kinavunjwa kuweka miundombinu ya mwendokasi
Ng'ombe bado anatoa maziwa.
 
Nimeona katika gazeti Serikali inatafuta kampuni ya ujenzi wa barabara ya mwendokasi pamoja na vituo vyake.

Kutoka maktaba ya taifa to Mwenge/Ubungo 13.5 km utakuwa na vituo visivyopungua 20

Kutoka Mwenge to Tegeta Dawasa 15.63 km itakua na vituo visivyopungua 19.

View attachment 2363211

Ujenzi wa phase 4 katika jiji la Dar es Salaam unasimamiwa Na tanroads. Ngoja tuone pindi utakapokamilika.

Ila ingewafaa wasitumie yule mkandarasi wa Mbagala to Kariakoo na Mbagala tu Magomeni. Naona design na ujenzi huko chini kidogo ya viwango tofauti na hii phase one ya mwendokasi tunayotumia.
Hongera Rais Samia Suluhu kwa kusimamia maendeleo kikamilifu Tanzania ni salama na Samia
 
wale ndugu zetu waliojenga kunduchi mashomoni iatkuwaje sasa pale?
 
Inasikitisha sana ufujaji na upotevu wa fedha za umma uliopo nchi hii. Tatizo ni kubwa saaana.

Pia hii barabara ya Mwenge, hakuna haja ya mwendokasi kwa sasa. Kuna mabasi ya kutosha na foleni yake ni ya kawaida hasa kama taa za barabarani zitaheshimiwa maana kwa mtazamo wangu traffic police ndiyo wanaleta shida. Pia sehemu zinazoleta foleni kama pale Tegeta Kwa Ndevu ni kwa sababu ya soko holela lililoachwa likue pale, malori yanashusha mizigo barabarani, hakuna parking, haya yote yanaminya njia ya barabara. Na hapo sijaongelea wauza mahindi ya kuchoma, machungwa na bidhaa zingine ambao ikifika saa 12 jioni wanateka mji wao na kuleta jam sehemu za vituo.

Kutoka Bunju kuja Ubungo, hata saa 8 usiku unapata basi, je mwendokasi zitakuwepo muda huo? Kuna watu wana magari yao lakini wamekuwa wanatumia mabasi kuja mjini, lakini kutokana na usumbufu utakaokuja na huu mradi, wengine wataona bora waendeshe na tatizo la foleni litakuwa kubwa zaidi hata ya sasa hivi.
 
Nimeona katika gazeti Serikali inatafuta kampuni ya ujenzi wa barabara ya mwendokasi pamoja na vituo vyake.

Kutoka maktaba ya taifa to Mwenge/Ubungo 13.5 km utakuwa na vituo visivyopungua 20

Kutoka Mwenge to Tegeta Dawasa 15.63 km itakua na vituo visivyopungua 19.

View attachment 2363211

Ujenzi wa phase 4 katika jiji la Dar es Salaam unasimamiwa Na tanroads. Ngoja tuone pindi utakapokamilika.

Ila ingewafaa wasitumie yule mkandarasi wa Mbagala to Kariakoo na Mbagala tu Magomeni. Naona design na ujenzi huko chini kidogo ya viwango tofauti na hii phase one ya mwendokasi tunayotumia.
Mkandarasi wa kwanza alikuwa Strabag na alifanya vizuri sana. Ila wa pili mizinguo kweli.
 
Inaitwa tunakamilisha taratibu ila mwenye tenda yake tayari yupo
 
Mi nafikiri tunarudi nyuma. Serikali iwekeze kwenye haya madude - Electrical Trams gharama za kuendesha ziko chini hata nauli itakuwa chini vinginevyo tuweke mabasi ya umeme.
View attachment 2363279

Kwa umeme upi huo?

Hiyo SGR tu tunasuasua hadi sasa imepitiliza muda uliopaswa kuanza kazi...
 
Ukweli nashindwa kuelewa hii nchi inataka nini yaani barabara imeshamalizika mnakuja tena kuibomoa kwanini mwendokasi isipite barabara ya kawe
 
Mbagala ile barabara ni ya miaka ya 90 na haikuandaliwa kwa ajili ya mwendokasi.
Ila serikali iliyokabidhiwa Uhuru haikuwekeza katika upimaji wa ardhi...

Mf barabara ya Tabata kuanzia hapo Dampo hadi Kigogo, Dampo hadi Segerea
Buguruni kuelekea TChangombe
 
Barabara ya Mwenge tunaenda kuijenga mara ya tatu sasa ndani ya kipindi kifupi. Tulijenga kwa pesa za maadhimisho ya Uhuru, tukaijenga tena kwa ufadhili wa Japan, tunaenda tena kuijenga kwa pesa za mkopo. Ukosefu wa mipango na watu kutafuta asilimia zao.
Hivyo kabisa waTaalamu wa nchi hii
 
Omba tenda hiyo sio tu unashauri wasitumie mtu fulani, huo ni uchawi.
Siyo vizuri kumnyamazisha mtoa hoja asiyejitosa mwenyewe kuwa mbadala. Mtoa hoja amependekeza mtu mbadala kwa kuwa huyo mtu ameonyesha tayari uzuri wa kazi aliyoifanya. Mtoa hoja hawezi kujipendekeza mwenyewe kwa kuwa labda hana utaalamu huo. Hivyo anataja nani apewe kazi hiyo kutokana na yale aliyokwisha onyesha. Mbaya ingekuwa kukataa jambo bila kutoa mbadala.
 
Back
Top Bottom