BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Serikali kupitia Wizara ya Afya imethibitisha uwepo wa Wagonjwa wa Kipindupindu muda mfupi baada ya Jamii Forums kuripoti uwepo taarifa za Ugonjwa huo katika Wilaya ya Ilala. Kwa mujibu wa Wizara ya Afya hadi sasa kuna Wagonjwa 10 waliobainika katika Wilaya ya Ilala ambapo 3 wapo Tabata, na wengine 7 wapo katika eneo la Kivule na Buguruni.
==================
==================