Serikali yatoa siku 3 FCC itoe ripoti kwanini bei za Soda zimepanda, pia imetoa siku 7 ijulishwe kwanini Vifaa vya Ujenzi vimepanda Bei

Ujenzi wa madarasa nchi nzima walitegemea vifaa vitoke wapi? Hii surge in demand, kwani kulikuwa na surge in production?
 
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara ameitaka tume ya ushindani FCC kutoa ripoti kwa Serikali ikieleza kwanini Vinywaji baridi na Vifaa vya ujenzi vimepanda bei...
TASAC kuwa regulator na player wanachelewesha mizigo ya wateja wao. Kazi ya kusimamia wameiacha wanafanya kazi ya clearing. Unawezaje kuwa referee na hapohapo mchezaji? Watenganishe majukumu wawe Regulators tu.
 
Na wakishatoa sababu zikawa zinakubalika
Itakuweje?
Tutabakia hapo hapo au tutaongeza vipasenti kidogo
 


Waziri aache utapeli wa kijinga.
 
Tanzania watu wameridhika.. mtu akishapata chakula hana shida ya kupambania sijui umeme, maji ya bomba safi, elimu nzuri nk. Hio haitabadilika leo sababu chakula nchi hii kipo kingi sana.. Tungekuwa jangwa kama Somalia , CCM wangeisoma namba
Hawajaridhika shida hawana cha kufanya maana hawezi badirisha chochote zaidi ya kelele tu
 
Nashangaa waziri anaanza kuchukua reaction leo wakati vifaa vya ujenzi vimepanda mda mfano tu bati la kawaida lililokuwa linauzwa 265000 mpaka 270000 saizi 430000,atajibalagiza tu
 
Ripoti ya kuungua Kariakoo iko wapi.

Leo wanaokuja wajinga walewale wanakwambia tunaunda tume kuchunguza moto soko la karume.

Halafu baada ya hapo ndiyo limepita hivyo. Mtabaki mnasubiri ripoti ambayo haiwezi kumsaidia mfanyabiashara aliyeunguliwa bidhaa zake.

Huwezi kuwasikia wakisema tutawasaidia hiki au kile, kwa njia hii au ile ili kuwapunguzia machungu .

Leo mwingine anasema bei ya soda, wenye viwanda watakaa naye atapewa mgawo wake hutamsikia Tena , utashangaa atageuka mtetezi wa bei ya soda kupanda.
 
Kwa hiyo waziri mzima wa biashara na viwanda hajui kinachoendelea ulimwenguni kwa sasa?
 
Mkuu mbona exemption zipo sana tuu
Fwatilia wazabuni wengi wanafaidika na hili

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
asihoji bei ya nyama, mchele, unga,.....mbolea. anahoji bei ya soda kitu ambacho with reqular consumption kinaharibu afya
 
Nilijua Fanta na Mirinda zimedoda kwa kuwa zinatumika kama mbadala
 
Kinamuuma nini? Soda ni luxury. Bei ya mafuta mbona hauulizi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…