Serikali yatoa siku 3 FCC itoe ripoti kwanini bei za Soda zimepanda, pia imetoa siku 7 ijulishwe kwanini Vifaa vya Ujenzi vimepanda Bei

Serikali yatoa siku 3 FCC itoe ripoti kwanini bei za Soda zimepanda, pia imetoa siku 7 ijulishwe kwanini Vifaa vya Ujenzi vimepanda Bei

Ujenzi wa madarasa nchi nzima walitegemea vifaa vitoke wapi? Hii surge in demand, kwani kulikuwa na surge in production?
 
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara ameitaka tume ya ushindani FCC kutoa ripoti kwa Serikali ikieleza kwanini Vinywaji baridi na Vifaa vya ujenzi vimepanda bei...
TASAC kuwa regulator na player wanachelewesha mizigo ya wateja wao. Kazi ya kusimamia wameiacha wanafanya kazi ya clearing. Unawezaje kuwa referee na hapohapo mchezaji? Watenganishe majukumu wawe Regulators tu.
 
Na wakishatoa sababu zikawa zinakubalika
Itakuweje?
Tutabakia hapo hapo au tutaongeza vipasenti kidogo
 
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara ameitaka tume ya ushindani FCC kutoa ripoti kwa Serikali ikieleza kwanini Vinywaji baridi na Vifaa vya ujenzi vimepanda bei.

Waziri ametoa siku 3 kwa ripoti ya Soda na siku 7 kwa vifaa vya ujenzi ziwe zimemfikia kwani inashangaza kusikia Soda zimeadimika ghafla soda zimerudi na bei iko juu.
===
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mh. Ashatu Kijaji ametoa siku tatu kwa Tume ya Ushindani (FCC) kutoa sababu ya kupanda kwa bei za vinywaji baridi nchini ambapo pia ametoa siku saba kwa Tume hiyo kueleza sababu za kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi sambamba na hatua ambayo Tume hiyo imechukua kuhusiana na kupanda kwa bei hizo.

Chanzo: ITV habari
View attachment 2085855

Waziri aache utapeli wa kijinga.
 
Tanzania watu wameridhika.. mtu akishapata chakula hana shida ya kupambania sijui umeme, maji ya bomba safi, elimu nzuri nk. Hio haitabadilika leo sababu chakula nchi hii kipo kingi sana.. Tungekuwa jangwa kama Somalia , CCM wangeisoma namba
Hawajaridhika shida hawana cha kufanya maana hawezi badirisha chochote zaidi ya kelele tu
 
Nashangaa waziri anaanza kuchukua reaction leo wakati vifaa vya ujenzi vimepanda mda mfano tu bati la kawaida lililokuwa linauzwa 265000 mpaka 270000 saizi 430000,atajibalagiza tu
 
Ripoti ya kuungua Kariakoo iko wapi.

Leo wanaokuja wajinga walewale wanakwambia tunaunda tume kuchunguza moto soko la karume.

Halafu baada ya hapo ndiyo limepita hivyo. Mtabaki mnasubiri ripoti ambayo haiwezi kumsaidia mfanyabiashara aliyeunguliwa bidhaa zake.

Huwezi kuwasikia wakisema tutawasaidia hiki au kile, kwa njia hii au ile ili kuwapunguzia machungu .

Leo mwingine anasema bei ya soda, wenye viwanda watakaa naye atapewa mgawo wake hutamsikia Tena , utashangaa atageuka mtetezi wa bei ya soda kupanda.
 
Kupanda kwa vifaa vya Ujenzi kumechangiwa na kutokuwepo kwa msamaha wa kodi kwenye miradi mingi ya Kiserikali inayotekelezwa nchi nzima.
Sababu nyingine ni kutokuwepo kwa bei elekezi ya vifaa vya Ujenzi hasa Nondo, Saruji, Vioo,bati,vyuma/pipes/n.k,Aluminium profiles, vigae, rangi, vifaa vya umeme,sanitaries/bomba na mbao kulingana na ubora.
Ikiwezekana FCC itumie agizo la Mh. Waziri kufanya review ya bei za bidhaa kwa kushirikiana na AQRB/Quantity Surveyors ili kuweka uzani wa bei kulingana na ubora, upatikanaji wake na jiographia ya nchi.
Mkuu mbona exemption zipo sana tuu
Fwatilia wazabuni wengi wanafaidika na hili

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
asihoji bei ya nyama, mchele, unga,.....mbolea. anahoji bei ya soda kitu ambacho with reqular consumption kinaharibu afya
 
Nilijua Fanta na Mirinda zimedoda kwa kuwa zinatumika kama mbadala
 
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara ameitaka tume ya ushindani FCC kutoa ripoti kwa Serikali ikieleza kwanini Vinywaji baridi na Vifaa vya ujenzi vimepanda bei.

Waziri ametoa siku 3 kwa ripoti ya Soda na siku 7 kwa vifaa vya ujenzi ziwe zimemfikia kwani inashangaza kusikia Soda zimeadimika ghafla soda zimerudi na bei iko juu.
===
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mh. Ashatu Kijaji ametoa siku tatu kwa Tume ya Ushindani (FCC) kutoa sababu ya kupanda kwa bei za vinywaji baridi nchini ambapo pia ametoa siku saba kwa Tume hiyo kueleza sababu za kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi sambamba na hatua ambayo Tume hiyo imechukua kuhusiana na kupanda kwa bei hizo.

Chanzo: ITV habari
View attachment 2085855
Kinamuuma nini? Soda ni luxury. Bei ya mafuta mbona hauulizi?
 
Back
Top Bottom