Serikali yatoa siku 3 FCC itoe ripoti kwanini bei za Soda zimepanda, pia imetoa siku 7 ijulishwe kwanini Vifaa vya Ujenzi vimepanda Bei

Serikali yatoa siku 3 FCC itoe ripoti kwanini bei za Soda zimepanda, pia imetoa siku 7 ijulishwe kwanini Vifaa vya Ujenzi vimepanda Bei

Ndio athari za kujifungia ndani Corona hizo. Supply chain imeharibika, na viwanda vilifungwa hivyo demand ni kubwa sana. Na ongezeka la gharama za usafirishaji.

Hakuna haja ya ramli hapo. Ikiwapendeza watoe ruzuku kama wanatuonea huruma sana. Au wapunguze ushuru ili bei ibakie ya awali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu waziri Ni mgeni Tanzania?
Huyu waziri amesomea Nini?
 
Kupotezeana wakati.
Huyo waziri anajamba halafu anaongeza sauti ya headphone zake ili wengine wasisikie. Jinga kubwa.

Haiwezekani serikali ipandishe gharama za umeme, mafuta na kukusanya kodi halafu bei za bidhaa zisipande.
 
Siku hiz wengi wanaogopa majuice ya viwandani.maji yananyweka zaidi.

Hata wangefunga kabisa hayo majuice masoda yenye misukari ya kuokoteza.inaongezea serkali gharama za matibabu
😀 😀 😀 Huko ndio wanakookotezea kodi mkuu, wakifunga watatujazia matozo mpaka tukimbilie Burundi.
 
Kwani waziri anashindwa kwenda viwandani moja kwa moja kujionea uhalisia mpaka aunde tume,hizi tume hazina maana yoyote na huwa hazina jipya kwa taifa,rejea tume alizowahi unda wazir mkuu,zaid wanatengenezea watu ulaji tu.kila kitu kimepanda na viongozi wapo wanaona watu wanaumia
 
Sababu ni hizi..
1. Uhaba wa maji
2. Mgao wa umeme.
3. Kupanda kwa bei za nishati (gesi na petrol)
4. Kodi, ushuru na tozo.
Sijui akipewa hizi sababu atasemaje! Wanaamuru utadhani hawajui mazingira ya uzalishaji nchini.
 
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara ameitaka tume ya ushindani FCC kutoa ripoti kwa serikali ikieleza kwanini Vinywaji baridi na Vifaa vya ujenzi vimepanda bei...

Watanzania watashangilia, Ujinga huu!
 
Huyo waziri ni mzembe wa fikra.

Ningekuwa rais ningemtumbua usiku huu huu tu.

Yaani hajui kuwa bei za vifaa vya ujenzi ilipanda bei toka mwaka jana?!
 
Back
Top Bottom