Habari wanajamvi,
Nimekaa nikafikiri sana, nimekosa majibu!
Hebu tusaidiane kidogo hivi, je ni busara serikali yetu kuendelea kuruhusu wasafiri kutoka mashariki ya mbali ASIA na ULAYA kwa kigezo cha utalii tu?
Maana kwa Habari zisizo rasmi kirusi hiki si rafiki wa joto (hawasurvive kwenye joto)
Naliona wimbi la watu wakija Africa hata Wale waliohathilika na COVID 19.
Sasa je ni busara kwa nchi yetu kuendelea kuruhusu safari za nje ya nchi kuingia au kutoka.
Wakati hatuna taarifa rasmi ya kuhusu tabia za kirusi.
Na je pesa ya utalii ni bora kuliko maisha ya watu?
Tatu je kuna hatua gani serikali imechukua kama taadhali kuhusu hivi virusi, au bado tunasikilizia?
- Kwanini serikali isitoe mwongozo kama ilivyo kuwa kwa virusi vya Ebola.
Mashuleni, vyuoni na vyombo vya habari, mabandiko mbalimbali yalikuwa yakielimisha watu kama kinga ili watu wawe na uelewa kidogo.
Je kwanini serikali isifunge mipaka kwa Muda. Kwasababu taarifa zisizo rasmi Bado airport zetu zinatumika kuingia na kutoka bila kujali msafiri anaenda au anatoka wapi.
La mwisho Serikali haijifunzi kwa irani ambao msafiri mmoja amesababisha maambukizo ya mamia na vifo vya makumi. Na kama inajifunza inachukua hatua gani?
Sent using
Jamii Forums mobile app