Serikali yaunda Kamati kuchunguza chanzo cha moto Soko Kuu Kariakoo. Waziri Mkuu asema hatua zitachukuliwa moja kwa moja ikijulikana kuna mkono wa mtu

Kwa nini badala ya kamati vyombo tofauti visichunguze? Kwa nini lazima iwe ni KAMATI?
Hapa inatakiwa TISS waonyeshe weledi wao. Na kama ni hujuma wahusika watolewe mfano maana hili halikubaliki.
 
Inshu ya zimamoto inahitaji preparation kubwa unaweza kwenda na maji yamejaa kumbe Moto unahitaji dry chemical Powder , au sand au carbon , Moto hauzimwi tu unazimwa kutokana na chanzo cha Moto , zaidi ukijua fire classes itakusaidia kwamba sio kila kitu ni zima Moto Bali watoa taarifa kuhusu chanzo cha moto
Zimamoto: Tulilazimika kufuata maji Air port kwa sababu Kariakoo hakuna matoleo ya maji
 
Inshu ya zimamoto inahitaji preparation kubwa unaweza kwenda na maji yamejaa kumbe Moto unahitaji dry chemical Powder , au sand au carbon , Moto hauzimwi tu unazimwa kutokana na chanzo cha Moto , zaidi ukijua fire classes itakusaidia kwamba sio kila kitu ni zima Moto Bali watoa taarifa kuhusu chanzo cha moto
 
1626002605334.png
 
Huyo waziri Mkuu aache utapeli wa kujifanya anaunda tume zisizo na tija. Aseme taarifa ya ile tume ya moto wa lori la mafuta iliishia wapi. Kama kweli hizo tume zina tija kwenye hayo majanga, mbona alificha taarifa ya lile janga la moto ya lori la mafuta Morogoro, hata baada ya kusema hiyo ripoti itawekwa wazi? Wafanyabishara huyo waziri Mkuu hana jipya hapo, bali anaweletea usanii tu lakini hana msaada wowote.
Kuna tume iliyochunguza ubadhirifu wa BOT kati ya January-March, hakuna kilichotokea.
 
Pia waangalie transaction za pesa iwe bank au mpesa za viongozi hao waliofukuzwa kazi,kama ni hujuma,lazima kuna waliopewa pesa kufanya hiyo kazi,
safi sana jambo la msingi ni kusaidia kutoa taarifa kama kuna dalili ya kuhusika kwa mtu yeyote ktk hujuma hii lazima washughulikiwe kikamikifu.
viongozi wetu ktk vitengo mbalimbali nawashauri waongeze ukali, vinginevyo kuna watu wataisumbua sana serikali yetu.
hatuwezi kupelekana kwa kuleana leana tu, lazima viongozi wetu wawe imara, watu hawafanani Lazima tujifunze namana ya kudili na kila aina ya watu.

asilimia kubwa ya sisi watanzania tunapenda kushurutishwa, hatuna tabia wala mazoea ya kutii bila shuruti, bila mjeledi kamwe hatusongi mbele.
mjeledi ukitumika wahusika wote watafahamika.
bana mbavu kidogo.
serikali siyo ya kuchezewa na wahuni wachache....haiwezekani.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inamaana vyoo , bar, migahawa na maduka na fremu zote kariakoo hamna hata iliyokua na koki ya maji?

Wameshindwa hata kuchukua maji misikiti yote ya hapo kariakoo?
Huwa sehemu kama ile kunakuwa na horse pipes zenye high pressure. Sasa mpaka hasara itokee ndiyo wataalmu wanakumbuka notes zao.

Maana yake Health and Safety ni 0 sokoni.
 
Habari wakuu,

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akiwa soko kuu la Kariakoo, amesema serikali imeunda tume ya watu kumi kuchunguza na kupata ukweli wa chanzo cha moto na athari zilizopatikana ikiwemo mali zilizoteketea, pia amesema Waziri mkuu yuko njiani kuja kukagua na kuongea na wafanyabiashara na umma kwa ujumla.

Makalla amesema kamati itakuja na mapendekezo ya namna bora ya kufanya ili kuendelea kukabiliana na majanga ya aina hiyo.

Mkuu wa Mkoa amewaomba waathirika kuwa watulivu wakati Serikali inachukua hatua za kubaini chanzo na athari. Pia amewakaribisha Bima kuja kuona wateja wao(Ambao walikuwa wamekata bima).

=========

Amos Makalla: Mheshimiwa Waziri mkuu, sisi tuko hapa toka jana, tumelala hapa baada ya janga hili la moto.

Athari ya janga hili ni kubwa na tumechukua hatua mbalimbali kuhakikisha usalama wa watu isitkee vifo au ajali za watu lakini mali nyingi zimeharibika.

Waziri Mkuu: Ndugu wafanyabiashara, nimekuja kuleta salam za pole kutoka kwa Mheshimiwa Samia Suluhu. Kuja kwangu leo asubuhi ilikuwa ni moja ya maelekezo yake bna kuja kuona hali halisi ya kuungua kwa bidhaa mbalimbali ambazo ndizo zilizokuwa zinaipa hadhi ya eneo hili la Kariakoo.

Nimeona hali halisi na kwa namna ninavyojua soko la Kariakoo, hasara kubwa inatarajiwa kupatikana, kama ambavyo nimetangulia kuwapa pole, nirudie tena kuwapa pole kwa kupoteza mali, fedha lakini pia hata muelekeo wa kufanya shughuli zenu za kibiashara hapo baadae.

Eneo hilo kwa sasa ni hatarishi kwasababu bado moto unafuka mwingi, hatujajua bado kuna maeneo yana milipuko kama vile mitungi ya gesi ambao wanatumia gesi lakini kuna nyaya nyingi sana za umeme, kuna mitambo mingi iliyokuwa inauzwa lakini pia ilikuwa inatumika ndio maana eneo hili sio salama.

Tumeelekeza vyombo vyetu vya ulinzi viendelee kuwa hapa kwa ajili ya kulinda usalama eneo zima lakini pia kuhakikisha moto huo hauendelei tena na watakuwa hapa mpaka utakapotulia kabisa.

Nawasihi sana wafanyabiashara wote muwe watulivu, kwasasa Serikali ipo na itaendelea kuwepo hapa mpaka tutakapojua nini chanzo cha moto huu, nani kisababishi cha moto huo ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa

Mkuu wa mkoa ameunda timu ya uchunguzi lakini bado haitoshi, hili soko ni la kimataifa. Itakuja timu ya kitaifa ambayo itaungana na timu ya mkuu wa mkoa.

Timu ya mkuu wa mkoa ni wale ambao walikuwa hapa kuanzia jana wakafanya kazi ya uokoaji na kusikia hiki na kile na kupata taarifa

Timu hii ya kitaifa kuchunguza moto itajumuisha wafuatao
  1. Ofisi ya RAS
  2. Ofisi ya Rais Ikulu na TAMISEMI
  3. Ofisi ya waziri mkuu-Mkurugenzi wa Maafa
  4. Vyombo vya ulinzi na usalama vinne(JWTZ, Polisi)
  5. TBA(Mhandisi wa majengo na Mhandisi wa umeme kwenye majengo)
  6. TANESCO
  7. Mwanasheria Mkuu
  8. Mkurugenzi wa Mashtaka
Kama nilivyosema awali, tubaini chanzo cha moto. Nini kimesababisha au nani kasababisha moto huu. Pili tunataka tujue angalau kutabiri tu kiwango cha mali zilizopotea.

Tatu tunataka tujue usalama wa jengo lenyewe baada ya moto, Je jengo bado linaweza kutumika?

Endapo itagundulika kuna mtu alihusika kwa namna moja au nyingine, ndio maana huko ndani kuna Mwanasheria Mkuu, mkurugenzi wa mashtaka, Polisi. Hatua zitachukuliwa moja kwa moja.

Ndugu wafanyabiashara, tunatambua mheshimiwa Rais alipotembelea hapa aliunda tume ya kufanya mapitia ya tuhuma mbalimbali ziliibuliwa, inawezekana pia sijui, labda tume hiyo ilianza kuwagusa. Kama kulikuwa na njama zozote zilizowahusu tume ile na hao waliokuwa wanaguswaguswa na wakigundulika, hatua kali zitachukuliwa
Kabla hizo kamati waziri mwenye dhamana atuachie vx yetu kwanza, pili mkuu wa jeshi la zima moto awe mahabusu kwa uzembe na team nzima, pumbavu mnanunua ma vx mapya mnapeana wakati ma Lori ya zima moto machakavu.
 
IMG-20210711-WA0030.jpg
 
wastage of time, kama tatizo lipo kwao wanawajibishwaje? Eti kinga kwa viongozi? nchi ya kiboya sana hii
 
Huwa sehemu kama ile kunakuwa na horse pipes zenye high pressure. Sasa mpaka hasara itokee ndiyo wataalmu wanakumbuka notes zao.

Maana yake Health and Safety ni 0 sokoni.
Okay,nmekuelewa.
Tunatatizo kubwa Kama taifa[emoji3525]
 
Sijui hivi na kamati ile ya naniii yakuchunguza ulaji pesa wizara ya fedha aliyotuambia PM, ilishatoa mrejesho?? Ngoja sie tuendelee kula mtoto, nyama tutazikuta chini...... Kazi iendelee.
Ni mtori mkuu siyo mtoto [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kwa taarifa ambazo sio RASMI zinasema kwamba moto wa KARIAKOO ni hujuma katika jitihada za kumuangusha Rais wetu pendwa, Suluhu Hassan.

Inasemekana kwamba ni mchongo uliosukwa na viongozi wa ndani ya soko kwa kushirikiana na viongozi wakubwa katika idara mbalimbali za nchi.

Nadhani mama anatakiwa sasa kupunguza maneno maneno ya kiunguja na aanze kuwa serious, watanzania hawahitaji huruma sana na wanajua kulamba ushuzi wa Rais hasa linapokuja suala la madaraka , lakini moyoni wakawa na nia ovu. Nadhani yeye anaona wale wote waliokuwa wanalamba ushuzi wa JPM , kwa sasa wanavyo ACT dhidi ya JPM.

Toa maoni yako juu ya moto wa kariakoo?

Kama ni hujuma, je ni tahadhari gani serikali ianze kuzifanyia kazi haraka iwezekanavyo ili kunusuru kitovu chetu cha biashara Tanzania dhidi ya visasi na uadui unaokuja kwa kasi?
 
Back
Top Bottom