Serikali yaunda Kamati kuchunguza chanzo cha moto Soko Kuu Kariakoo. Waziri Mkuu asema hatua zitachukuliwa moja kwa moja ikijulikana kuna mkono wa mtu

Serikali yaunda Kamati kuchunguza chanzo cha moto Soko Kuu Kariakoo. Waziri Mkuu asema hatua zitachukuliwa moja kwa moja ikijulikana kuna mkono wa mtu

Na ameshafanya uchunguzi na kugundua ni hujuma!na wala sio electric fault au sababu nyingine,sasa nimeelewa why hatuhitaji idara ya forensic ndani ya idara zetu za kiusalaama
Hatari sana mkuu.
 
Hebu tuwekee ushahidi tuone hizo hujuma unazosema zimefanyika.
 
Wakati tukisubiri matokeo ya uchunguzi Kwa mtazamo wangu hasara itayopatikana ni kubwa.

Pia nishauri tuache waliopewa jukumu la uchunguzi walifanye.

Kuanza kuspeculate tunaharibu.
 
mama Samia anasukumwa kuwa mkatili!
Unapohujumu soko kuu nchini kama la kariakoo ni wazi unatenda tendo la kigaidi kwani mfumuko wa bei kariakoo ni mfumuko wa bei Tanzania.

iwapo ikithibitika kuna uhujumu lazima wahisika wachukuliwe hatua Kali
Wachina wanelitaka soko kwa muda mrefu bila mafanikio.

Kuna soko la Kisutu likaboreshwa kwa kujengwa la ghorofa...Sasa linahitaji wapangaji.

Machinga complex kuna ulazima wa kulitafutia wapangaji pia.
Soko kuu la Kariakoo likisimama kufanya kazi ni wazi hayo masoko mengine yatapata wateja na wapangaji pia... Na mchina atapata nafasi ya kulinyakua.

Je, tufanyeje ili Soko la kariakoo liache kufanya kazi kwa muda?
 
Serikali ya nini kuchunguza hapo, watamalizana na insurance company kama walikuwa nayo😁, can't believe soko kubwa kama hilo kukosa fire insurance, fukuza then prosecute management yote kama kweli no insurance, ajali za moto ni kawaida kitu ambacho si kawaida ni soko kama kariakoo kutokuwa na insurance
...fanya mfano hao
 
Majibu ya kamati ya uchunguzi,ukiwa tayari na wa kiuambia umma mni tag

Ova
 
Gaidi no 1 Mbowe ndio amelipua soko....wanahangaika nini ....si ndio akili zao mwisho hapo
 
Masoko yote makubwa huwa yanachomwa Ili kupisha ujenzi wa masoko ya kisasa au watu washalipa Sana bima hivyo utaka walipwe bima
 
Mpaka leo holaa

Nilishapoteza imani kwa huyu waziri mkuu, ni moja ya viongozi ambao siwaamini matamko yao.
Yaani alivodanganya ishu ya mwendazake macho makavu kabisa tena msikitini na yeye ni muislam.
 
Habari wakuu,

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akiwa Soko Kuu la Kariakoo, amesema serikali imeunda tume ya watu kumi kuchunguza na kupata ukweli wa chanzo cha moto na athari zilizopatikana ikiwemo mali zilizoteketea, pia amesema Waziri mkuu yuko njiani kuja kukagua na kuongea na wafanyabiashara na umma kwa ujumla.

Makalla amesema kamati itakuja na mapendekezo ya namna bora ya kufanya ili kuendelea kukabiliana na majanga ya aina hiyo.

Mkuu wa Mkoa amewaomba waathirika kuwa watulivu wakati Serikali inachukua hatua za kubaini chanzo na athari. Pia amewakaribisha Bima kuja kuona wateja wao(Ambao walikuwa wamekata bima).

=========

Amos Makalla: Mheshimiwa Waziri mkuu, sisi tuko hapa toka jana, tumelala hapa baada ya janga hili la moto.

Athari ya janga hili ni kubwa na tumechukua hatua mbalimbali kuhakikisha usalama wa watu isitkee vifo au ajali za watu lakini mali nyingi zimeharibika.

Waziri Mkuu: Ndugu wafanyabiashara, nimekuja kuleta salam za pole kutoka kwa Mheshimiwa Samia Suluhu. Kuja kwangu leo asubuhi ilikuwa ni moja ya maelekezo yake bna kuja kuona hali halisi ya kuungua kwa bidhaa mbalimbali ambazo ndizo zilizokuwa zinaipa hadhi ya eneo hili la Kariakoo.

Nimeona hali halisi na kwa namna ninavyojua soko la Kariakoo, hasara kubwa inatarajiwa kupatikana, kama ambavyo nimetangulia kuwapa pole, nirudie tena kuwapa pole kwa kupoteza mali, fedha lakini pia hata muelekeo wa kufanya shughuli zenu za kibiashara hapo baadae.

Eneo hilo kwa sasa ni hatarishi kwasababu bado moto unafuka mwingi, hatujajua bado kuna maeneo yana milipuko kama vile mitungi ya gesi ambao wanatumia gesi lakini kuna nyaya nyingi sana za umeme, kuna mitambo mingi iliyokuwa inauzwa lakini pia ilikuwa inatumika ndio maana eneo hili sio salama.

Tumeelekeza vyombo vyetu vya ulinzi viendelee kuwa hapa kwa ajili ya kulinda usalama eneo zima lakini pia kuhakikisha moto huo hauendelei tena na watakuwa hapa mpaka utakapotulia kabisa.

Nawasihi sana wafanyabiashara wote muwe watulivu, kwasasa Serikali ipo na itaendelea kuwepo hapa mpaka tutakapojua nini chanzo cha moto huu, nani kisababishi cha moto huo ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa

Mkuu wa mkoa ameunda timu ya uchunguzi lakini bado haitoshi, hili soko ni la kimataifa. Itakuja timu ya kitaifa ambayo itaungana na timu ya mkuu wa mkoa.

Timu ya mkuu wa mkoa ni wale ambao walikuwa hapa kuanzia jana wakafanya kazi ya uokoaji na kusikia hiki na kile na kupata taarifa

Timu hii ya kitaifa kuchunguza moto itajumuisha wafuatao
  1. Ofisi ya RAS
  2. Ofisi ya Rais Ikulu na TAMISEMI
  3. Ofisi ya waziri mkuu-Mkurugenzi wa Maafa
  4. Vyombo vya ulinzi na usalama vinne(JWTZ, Polisi)
  5. TBA(Mhandisi wa majengo na Mhandisi wa umeme kwenye majengo)
  6. TANESCO
  7. Mwanasheria Mkuu
  8. Mkurugenzi wa Mashtaka
Kama nilivyosema awali, tubaini chanzo cha moto. Nini kimesababisha au nani kasababisha moto huu. Pili tunataka tujue angalau kutabiri tu kiwango cha mali zilizopotea.

Tatu tunataka tujue usalama wa jengo lenyewe baada ya moto, Je jengo bado linaweza kutumika?

Endapo itagundulika kuna mtu alihusika kwa namna moja au nyingine, ndio maana huko ndani kuna Mwanasheria Mkuu, mkurugenzi wa mashtaka, Polisi. Hatua zitachukuliwa moja kwa moja.

Ndugu wafanyabiashara, tunatambua mheshimiwa Rais alipotembelea hapa aliunda tume ya kufanya mapitia ya tuhuma mbalimbali ziliibuliwa, inawezekana pia sijui, labda tume hiyo ilianza kuwagusa. Kama kulikuwa na njama zozote zilizowahusu tume ile na hao waliokuwa wanaguswaguswa na wakigundulika, hatua kali zitachukuliwa
Hii kamati mbona kimya hatujapata mrejesho wowote!!!
 
Back
Top Bottom