Serikali yawataka watalii waliopanga kuja nchini kuahirisha safari hadi hapo Corona itakapodhibitiwa

Serikali yawataka watalii waliopanga kuja nchini kuahirisha safari hadi hapo Corona itakapodhibitiwa

Viongozi wengi TZ, wanamaajabu. Polepole anasema utalii hautazuiwa, huyu naye eti anawashauri wasi cancel bali waahirishe.

Jee anajua hao watalii ni wafanyikazi huko kwao, na hupanga livu zao miaka miwili kabla na ku save pesa za safari.

Jee anajua kuwa kama Tanzania haikufunga mipaka au kusema hatutapokea wasafiri kutoka nchi kadha, mojawapo ikiwa hiyo ya hao tourist, basi ajue kuwa hawatarudishiwa pesa ya ticket na malipo ya hoteli, kwa sababu itakuwa kavunja safari mwenyewe.

Tangazeni lock down , watalii wengi watalipwa pesa zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa hazina maana ya upumbavu.
Ni makosa makubwa sana kufikiria kuwa siasa inahusika na udanganyifu, ujinga, uongo na upumbavu.
Kwa wanaccm siasa ni uongo ndo maana kwa zaidi ya miaka 58 ya Uhuru chini ya utawala wa ccm ujinga,umasikini na maradhi bado Tanzania ni nyumbani kwao huku chama kikitumia robots zinazolipwa mshahara Kati ya laki mbili na milioni mbili kusalia madarakani
 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh Kanyasu amewataka watalii waliopanga kutembelea Tanzania kuahirisha safari zao hadi pale ugonjwa wa Corona utakapokuwa umedhibitiwa.

Mh Kanyasu amewataka watalii hao kutofuta safari zao bali waahirishe kupisha hili janga linaloisumbua Dunia kwa sasa.

Source: ITV habari!
Kiufupi Serikali bora ingeongozwa na Mzee Mgaya.....hii ya awamu ya tano haiko seriously kupambana na Korona..



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh Kanyasu amewataka watalii waliopanga kutembelea Tanzania kuahirisha safari zao hadi pale ugonjwa wa Corona utakapokuwa umedhibitiwa.

Mh Kanyasu amewataka watalii hao kutofuta safari zao bali waahirishe kupisha hili janga linaloisumbua Dunia kwa sasa.

Source: ITV habari!
Asante sana. Tulisema tangu awali ila serikali ikatia pamba masikioni. Jana Polepole anajigamba kuwa Corona tutapambana nayo kwa kutumia vyombo vya dola kama tulivyoidhibiti CHADEMA.

Serikali ina tatizo mahali. Hasa kwenye communications na kufanya maamuzi.
 
Naomba kujua ametamka kupongeza juhudi za JPM!? Vinginevyo ni kinyume na mtazamo wa mkuu kutumia fursa ya majanga wengine kupiga hela, rejea maelezo yake kwa wahanga mafutiko Lindi, ... wakati wa mabondeni wanafurika nyie limeni mje muwauzie chakula kwa bei yenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serekali ya matahira! Badala ya kufunga mipaka wanaomba watalii kuhairisha kuja?!
 
Naona wengi hapa mnachanganya mambo, alichoongea polepole na waziri havina tofauti.
Polepole alisema mipaka isifingwe uchumi utayumba.
Ila Naibu waziri kasema wale wageni waliopanga kuja wasi cancel safari zao bali wa postpone mpaka hali itakapoimarika. Maana wageni walokuwa mpaka wamelipia wanadai total refund so waziri anawasihi waahirishe wasirudishiwe hela zao.
Ukitizama kauli za hawa wote hakuna tofauti kabisa,... wote wanawaza hela tu.
Huyu anaogopa wakifunga mpaka watakosa watalii, na huyu anaogopa watalii wako cancel watarudishiwa hela zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilishawahi kuleta post humu ya huyu naibu waziri Constantine John Kanyasu kuwa ni mtu humble mtakuwa mmemuona mliokuwa mnasema hamfahamu.
 
Kana mtindio wa Ubongo kare achaneni nako, kadumacuuu

Don't make a promise you can't fulfill...
 
Nimeona naibu waziri akiomba wasisitishe safari(cancel) bali wasogeze mbele kama hawana mpango wa kuja sasa.

Watalii wengi wanacancel safari na kuomba refund, sasa huyo alipata hela yake kuja tena ni probability. Bora waombwe kusogeza mbele safari kuliko kuahirisha. Wakiahirisha madhara yake ni makubwa sana.
 
Back
Top Bottom