Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Kama nusu saa ijayo hivi nitawaletea maendeleo ya habari hii.... kutoka Kiev...
 

A very good philosophy: ANGUKA.

Nadhani mojawapo ya matatizo ya JK ni ya kujitakia. Wakati wa kampeini zake za kuwania uraisi kwa miaka kumi alijenga network kubwa sana ambayo ilikuwa inawaahidi wananchi kuwa akiingia madarakani neema itakuja nchini. Nakumbuku mke wake akiwa kwenye kampeini kule Lindi alisema "Lulu hiyo." Kwa jumla alijenga expectation kubwa sana ambayo ilikuwa nje ya uwezo wake. Mbaya zaidi wakati anatfanya kampeini za urais kwa miaka kumi hiyo, hakuwa anajifunza jinsi ya kuongoza na jinsi ya kutimiza anachoahidi. Sasa mambo yanamtokea puani. Uwezo wa kuwaadhibu waliomfanyoa kampeini hana, uwezo wa ku-deliver hana, sana sana baadhi ya wafuasi wake wanatumia mgongo wake kujiandalia kampeini za 2010 au 2015. Ndiyo hivyo sasa ana-ANGUKA.
 

....hii ndio maana yake,kama itafanywa kwa vitendo!

hongera kwa kuwa na mawazo kama haya!.pili mungu mjaa wa yote akubariki uweze kutenda mambo kama haya pale utakapohitajika!

asalaam aleykhum!.
 
Nakuambia Tanzania sasa imekuwa kama mtoto yatima aliyetelekezwa na jamii. Sasa hivi nchi inaenda kama hamna uongozi. Ujue watanzania wengi walileweshwa na tabasamu na ahadi za Maisha bora kwa kila mtanzania bila kutathimini kunastrategy gani ya kuwezesha maisha bora. Nawaambia watu watakuja kukumbuka serikali ilyopita kuliko hii maana hii watu waliipkea kwa matumaini makubwa mmno. Muungwana alitoa ahadi ambazo hazitekelezeki sasa nakuambia tunaelekea pabaya. Mbaya zaidi anajua pia hata 2010 atashinda kwa kishindo kama kawa. Sisi tutegemee kuona mengi zaidi. Hapa sauti ya umma inahitajika. Elimu ya uraia inahitajika kwa wanannchi wetu. Hii sauti ya umma ndio itawaondoa akina msola. Lakini jee watanzania wana mwamko huo? Je watanzania wanauwezo wakusema sasa tumechosha basi?
 
Jamani vijana wenu 20 bado wapo Ubalozini hawaondoki hapo hadi wapate jibu serikalini. Ubalozi umewasiliana na Tanzania na jibu ni lile lile "matatizo yao tunayashughulikia". Sasa hivi ubalozi umefungwa na vijana hawana chakula wala nini... niko tayari kujitolea chochote ili kuwasaidia hadi drama hii itakwisha... kama kuna mtu yuko tayari kuungana nami... wasiliana nami na nitawapeni namba ya vijana hawa Ukraine.. na mnaweza kuamua la kufanya...

Ubalozi wa UK umesema uko tayari kuwapa fedha za matumizi n.k endapo serikali ya Tanzania itakuwa tayari kuahidi kurudisha fedha hizo. Serikali yenu imekataa!!
 
hizi habari ni za masikitiko sana,hivi huyu tutayashughulikia yeye hana watoto kweli. Je nini msimamo wa hawa wanafunzi ?,ni kurudi nyumbani au nini,kama serikali itaendelea shikilia msimamo huo wa kutowatambua ni nini hatima yake.
Naomba mzee mkjj uwaulize au naomba simu yao
 
Jamani, vijana hawaondoki hapo ubalozini, wanashindia mikate... na wako tayari kulala nje leo... anayetaka kuwasaidia wasiliana na mimi PM...
 

....watoto wake wanafahamika wanasoma wapi? maanake dah!
 
je kuna icha zozote au blog yenye piacha zoo hapo ubalozi wa uk london?

Je waandishi mahiri kama akian YAKUBU wamepata mawasiliano yoyote na FOREIGN AND COMMONWEALTH OFFICE?
 
Habari hii, iko karibu kulipuka na kuwa habari kubwa..... subirini kidogo...na tegeni masikio kwenye vyombo mbalimbali vya habari.. vya nyumbani na kimataifa...
 
Maneno hayo ya Martin Luther King Junior miongo kadhaa iliyopita yana ukweli leo kuliko wakati mwingine wowote. Ndugu zetu wa kitanzania leo watalala nje na kushindia kula mikate kwa vile tu serikali yao haiko tayari kukubali makosa na kusahihisha. Binafsi, sina sababu hata chembe ya kufuatilia suala hili kwani sina maslahi yoyote nalo, sina ndugu, rafiki, jamaa n.k. Hata hivyo nina kifungo kimoja na ndugu zetu hawa kwamba sisi sote ni Watanzania na kama mazingira yangekuwa tofauti bila ya shaka tungeweza kukutana, kusoma pamoja, kucheza pamoja na hata kuoleana!!

Kiburi cha serikali kinaudhi na kinakera. Hata hivyo haitoshi kulalamika na kuwaonea huruma tukiwa tumeketi kwenye vyumba vyetu na sebule zetu huku tukipunga upepo wa starehe zetu. Binafsi nimejitolewa kuwasaidia kiasi kidogo nilichonacho kuwapa chakula cha uhakika kwa siku hizi watakazoketi ubalozini.

Bila ya shaka kuna baadhi ya wananchi wenzangu ambao nao wameguswa na stori hii. Kama unataka kupiga simu piga namba hii na uulize jinsi ya kuwasaidia. Namba 380-936 411476 na utazungumza na Bashiri (kiongozi wa msafara huo) na utaamua mwenyewe nini na jinsi utawasaidia.

Maneno na huruma peke yake haitoshi.. this is a call to action!!! Stand up and be counted! you sons and daughtrers of my beloved motherland, dare to act now! you visionaries of the new springtime of hope for Tanzania, you fellow Tanzanians, a breed of a new generation of courage and you who have desired greatness for your nation it is about time to rise! Stand up and act, speak and be heard! But as I always say, if you are a follower then wait, but if you have a spark of leadership in you, then lead!! It is about time.
 
Je kuna mweye kujua cost of living huko Ukraine ikoje. Yaani kwa njia nyepesi, $100 zinaweza kufanya nini?
 
mwanakijiji,
Lbbda tuwasiliane na amnesty international yaweza kuwasaidia ama redcross japo kwa chakula hapo walipo kwani kama ni watu waliokaa kwa muda mrefu wanaweza hata kufa kwa njaa .
Nina rafiki yangu yupo cossovo anafanya amnesty ngoja nijaribu kuchek naye kama waweza kusaidia japo kwa maji na mikate.
Struggle is a path to success.
 
Nimezungumza na waziri "wenu" mkuu.. na jibu lake limenifanya niombe kuondoka mapema shambani leo..!! ati hana muda anakimbilia "kula"
 
I was in Kiev three weeks ago. $100 inaweza kukupa mlo wa mchana na jioni + malazi with some incidentals. hizo ni kama UHV 500! Si haba one can survive for very few days. Ila in general hali ya maisha ni ngumu sana! Labda kwa sababu mimi nilikuwa mgeni, But since i started travelling its my worst country I have ever visited and I wouldnt wish to visit it in the future! ni nchi ya kibaguzi ni hakuna especially kwa mtu mweusi!!!!
 
Kwani ulimtegemea aseme anaenda wapi zaidi ya kwenda kula?
wanachokijua zaidi ya kula ni kuiba,so aliona aibu kukwambia kuwa anaenda kucheza dili.
 
MK.. jamani.. vijana wenu wanalala nje, wanashindia mikate na maji.. halafu anakimbilia kwenda kula tu?
 
Mzee MKJJ uko serious ? waziri Mkuun kasema anaenda kula ?
 
Mzee Mwanakijiji,
Kwa vile wewe uko karibu nao nakuomba anzisha account, Mimi nakuamini wewe nitawakilisha - Ka Mia kangu ka ngama ktk account pindi tu utakapo nipa details. Mengine tutazungumza nipigei simu zaidi.
Pili, bila kusahau Jerry Springer, Ohio (memorial day) vipi kuna haja ya kujimwaga wazee wazima?
Action brothers/sisters Action...tawadheni kabla hamjaingia msikitini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…