Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Haya mipango ishakamilika... anayetaka kusaidia niandikie PM na nitakupa "password" na jibu lake. Na ukituma wasiliana nami ili niweze kucoordinate michango hiyo. Pesa zitatumwa kwa Bashiri Ramadhani (ndio kiongozi wa wanafunzi na ndiye ambaye amezungumza na Ubalozi wa UK) Kwa vile utaweka jina lako unapotuma na ili kulinda "kutojulikana kwa wanachama" basi ukishaatuma wasiliana nami kwa Email Yangu ambayo ni mwanakijiji@jamboforums.com na kunipa info:

- Kiasi ulichotuma
- Confirmation number
- na Jina

Mimi nitajumlisha taarifa za wote mliotuma na kuwapa jumla. Halafu kesho at the earliest au Jumapili nitazungumza na vijana na kuwapa jumla.

Bashiri hatakuwa na password na jibu lake. Ni nyinyi mliotuma tu ndo mtajua na nitakapowasiliana nao.. Bashiri atapewa idadi ya fedha zilizotumwa na majina. Mwanafunzi mwingine atapewa password na mwingine atapewa jibu ili wakienda kuchukua wote watatu wawepo. Kabla ya kuwapa taarifa hizo nitazungumza na wanafunzi wote kwa spika phone na kuwaambia kiasi kilichotumwa na wanichagulie mtu atakayepewa password na jibu.
 
Nina himiza mshimano na JF ifanye kweli kuonyesha kwamnba hatusemi tu bali tunaweza kutenda pia .Tafadhalini tujitokeze kwa wingu wetu.Toa chochote tuwasaidi hawa maana ndiyo mapambano yenyewe.
 
Kabla sijajivuta!
Kwa hiyo tukisha tuma ndio ktuwasiane na wewe!... ama unatupa kwanza hiyo password wewe?
 
anayetaka kutuma..nitampatia password hiyo na jibu lake... so nitajua nani ametuma kiasi gani.. na nikiwaambia basi wataelewa. Kumbuka kutuma fedha huhitaji kutumia jina lako halisi.. ...
 
Kiev: Wanafunzi bado wapo Ubalozini hawaendi popote na wako tayari kukaa hapo weekend nzima. Kwa mujibu wa Afisa wa ngazi za juu za ubalozi huo niliyezungumza naye, wao hawana matatizo na vijana kuwa hapo kwani wameomba hiyo hifadhi.

Dar-es-Salaam: Ubalozi wa Uingereza Ukraine umekuwa na mawasiliano na Ubalozi wao Tanzania ambao kutwa nzima ya leo wamekuwa wakiwasiliana na viongozi wa serikali ya Tanzania kwani hili la wanafunzi kupiga kambi ubalozini limeishtua serikali.

Michango:
Kuna mtu ameshauri kutumia paypal account ya KLH News, hata hivyo nimecheki na Paypal inahitaji niwe na account nao angalau siku 60 kabla hatujaweza kutoa fedha kwenye account hiyo, na hadi leo tuna siku 51!!

Kwa ushauri wa Afisa huyo njia pekee ya kuwafikishia misaada vijana hao kwa haraka ni kupitia Western Union. Nimezungumza na vijana wote na wao wamekubali kutumia jina la mtu mmoja. Ninachotaka kufanya ni kutumia mtindo wa collective check and balance.

: Jina analotumiwa ni la mmoja
: Swali la usalama (anapewa mwingine)
: Jibu anapewa mwingine
: Wale wanaotaka kutuma wawasiliane na mimi nitawapa jina, swali na jibu. Wakishatuma waconfirm na mimi. Na mimi sitawaambia Kiev zilizotumwa hadi baadaye jioni ya leo au kesho asubuhi (nikijumlisha).

I'm open for any other suggestions, lakini tusipoteze muda kukosoa tu tuje na suluhisho linalowezekana kwani kule ni jioni ni giza linaingia...
Hivyo wanafunzi angalau watatu wanashiriki katika kuzichukua fedha hizo: That is the best I can come up with right now.
Tafadhali naomba nielimishwe yafuatayo:
1)Nini hasa lilikuwa lengo lao hao vijana kwenda kujisalimisha hapo Ubalozi?
2)Na kama ubalozi wa Uingereza umekubali kuwapokea nini nafasi ya hii michango tunayohamasishana sasa?Na nini nafasi ya ubalozi wa uingereza ktk kukubali kwao kwa mujibu wa ofisa uliyezungumza naye na kwa mujibu wa vijana wanaohusika na saga hili?
3)Hawa vijana wapo 29,je tunahakika gani hiyo michango itawafikia wote.
4)Je hao watatu hawawezi wakakatiana wao na kuwaacha wenzao kwenye mataa?
 
KNKCU,

a. Lengo la wao kwenda hapo ni kutaka attention ya Taifa lao na viongozi wao. Kwa vile hatuna Ubalozi Ukraine, taratibu zinawataka wajisalimishe kwa nchi ya Jumuiya ya Madola.. na Uingereza ndio mama yao. Hawakwenda kuomba ukimbizi.

b. Ubalozi umekubali kuwasikiliza na kuwaacha wakae hapo kwenye uwanja wa Ubalozi. Hadi hivi sasa ubalozi haujatoa chochote zaidi ya kujaribu kuwasiliana na Tanzania na Ubalozi wa UK Tanzania. Ubalozi ulishatoa ofa kwa serikali ya Tanzania kuwa wawaruhusu wao Ubalozi watoe fedha za matumizi n.k kwa vijana kwa ahadi kwamba serikali ya TZ itairudishia Uingereza pesa hizo, serikali yetu imekataa (haikutoa jibu). So Ubalozi wa Uingereza hauna lolote lile la kufanya.

c. Michango kwa sasa inawalenga wale waliopiga kambi hapo Ubalozini 20 hivi siyo wote 29 wapo hapo wengine wanaangalia vitu huko vyuoni walikowaacha. Hivyo michango hii ya matumizi na kujikimu hadi serikali itakapotatua tatizo hilo ni kwa wale waliopiga kambi hapo. Hawaondoki Ubalozini hapo..! Hivyo ni kuhakikisha wanapata chakula, na mablanketi n.k..

d. Nimeshawaambia wanafunzi wote kwa pamoja (kutumia spika za simu) na kuzungumza nao mmoja mmoja kuwa tunajaribu kuwasaidia na nimewaeleza mpango wazi, so siyo mtu mmoja mwenye ujuzi wa michango hii. Na ndio maana badala ya kutuma mtu mmoja mmoja nataka nijue ni kiasi gani kimetumwa na nitakapowaambia waende kuchukua basi nitawaambia kwa pamoja (na kurekodi naweza kuwarekodi)!
 
Mzee Mwanakijiji, Nimeandika PM muda lakini sijapata jibu toka kwako.. - Ijumaa hii tena mjomba!
 
Nimekuelewa na ahsante kwa maelezo yako.
 
Mzee MKJJ
Tafadhali thibitisha kama umepata kamchango kangu ni kadopgo lakini tujitolee wandugu . Hawa vijana lazima tuwape moyo na msaada wa hali na mali . Shime mimi nimesha kapesa kangu watoto wamegawana na hawa ndugu lakini ndiyo utu kabisa .Tujitahidi tafadhali sana .
 
Mbona wengine kimya au hawaoni umuhimu wa hili?

SASA LEO NIMEONA UMUHIMU WA KUWA NA HIYO BRITISH PASSPORT na naona kwa nini walioko nje ya NCHI WANACHUKIWA
 
Sijui kwa nini machale yalinicheza aisee. Kuna mtoto wa ndugu yangu mmja alikuwa ameichangamkia skolaship hiyo nikamwambia tufanye maarifa kubadilisha mwelekeo; nashukuru alikubaliana nami.

Tatizo kubwa sana kwa sasa hivi ni kuwa Tanzania tunaelekea pabaya. Jinsi serikali inavyotendea wananchi wake, nina wasiwasi kuwa imani kwa serikali itapungua sana na hivyo kusababishwa viongozi waendeshe nchi kimabavu zaidi. Ni kawaida kuwa kiongozi akiwa hana support ya wananchi wake huwa anakuwa mbabe.
 
Kichuguu, maneno yako ni ya kweli. Katika kufuatilia jambo hili kuna mambo mengi nimegundua kuhusu watendaji wa serikali na viongozi wetu wa kisiasa. Kubwa nililoligundua naliandikia makala ya wiki ijayo. Hata hivyo madogo niliyogundua ni kwamba:

a. Hatujui kupanga kitu kwa upana wake na kimo chake. Tunapanga vitu kufikia kiwango cha chini kabisa siyo cha juu. Tunataka elimu nzuri, lakini badala ya kuhakikisha elimu inagharamika na kufikiwa na watu wengi zaidi, tunafanya kuwa bidhaa wenye kuimudu wachache. Kabla ya suala hili la Ukraine, nililetewa malalamiko ya shule moja ya Kiislamu pale Dar ambayo katika fomu zake za kusajiliwa zilisema wazi kuwa ada inalipwa mapema pindi mtoto akikubaliwa na endapo mtoto huyo na wazazi wake wakaamua kwenda shule nyingine basi hiyo ada hairejeshwi!! Walichofanya shule hiyo ni kufanya selection yao mapema kweli na hivyo kuwatia wazazi kihoro!! Mmoja wa maprofesa wa UDSM ni mmoja wa wanabodi wa shule hiyo!!! Hiyo ada yenyewe inalingana karibu na ya Chuo Kikuu!! Siyo shule hiyo tu, zipo shule nyingine za binafsi ambazo zimetapakaa kama uyoga na ambazo masharti yake siyo tofauti sana na hayo. Watanzania tumekubali kulipa hivyo, na wale wachache wenye kumudu ndio wanapeleka watoto wao huko.

b. Inapotokea nafasi za kwenda nje, wazazi na watoto hufurahia kwa sababu inakuwa ni kama ahueni kwa familia. Mzazi mmoja niliyezungumza naye leo (unaweza kumsikiiliza kwenye Tovuti) ana watoto karibu watano wako shule na anawasaidia wengine wa ndugu zake (siyo kitu cha ajabu TZ) kwani ni yeye aliyesoma zaidi katika familia. Alipopata nafasi ya mwanae kusomeshwa huko Ukraine alishukuru Mungu, lakini leo hii hana hili wala lile zaidi ya kuhofu juu ya mtoto wake huyo. Wale wanafunzi wa Urusi wanalipwa dola 200 kwa mwezi kwa matumizi yao yote, pesa hizo zikiisha lwao!! Serikali ilipanga bajeti vipi huko? Kama ilikuwa tayari kulipia dola 10,000 kwa wanafunzi wanaoenda Uchina na dola 3000 kwa wale wa Urusi na Ukraine.. wanaweza kuwaambia watu vigezo gani vilitumika? Kabla ya kumpeleka mtoto kwenye nchi nyingine angalau basi wabajeti hali halisi na siyo hali halisi ya chini kabisa!!

mengine nitayaandika zaidi...
 
Back
Top Bottom