Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

na Nasra Abdallah (Tanzania Daima)



UMOJA wa vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na TLP, umeitaka serikali kueleza wazi juu ya hatima ya wanafunzi wa Kitanzania wapatao 29, ambao walikuwa wanasoma nchini Ukraine na kufukuzwa kwa kushindwa kulipa ada.
Viongozi wa vyama hivyo, walitoa kauli ya pamoja mwishoni mwa wiki iliyopita, wakati walipokuwa wanazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Habari zilizopatikana mwishoni mwa wiki iliyopita, zilikuwa zinaeleza kuwa, kutokana na hali mbaya kifedha inayowakabili, wanafunzi hao waliamua kujisalimisha katika ubalozi wa Uingereza uliopo nchini humo.

Ubalozi huo, nao ulikubali kuchukua mzigo wa kuwahudumia wanafunzi hao wakati matatizo yao yanatafutiwa ufumbuzi.

Vyama hivyo vimetaka kujua msimamo wa serikali, baada ya wanafunzi hao kutelekezwa na kuamua kuomba hifadhi kwenye ubalozi wa Uingereza jijini Kiev, huku serikali ikiwa imeendelea kukaa kimya bila ya kusema lolote.

Wakizungumza kwa masikitiko, viongozi wa vyama hivyo walisema tukio hilo ni la aibu kwa taifa, kwani kwa kushindwa kuwalipia ada, serikali imewafanya raia wake waishi nchi za ugenini kama watu wasiokuwa na nchi.

Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, alisema ameshamuandikia Rais Jakaya Kikwete barua kuhusu suala hilo zaidi ya mara tatu, lakini hadi leo hajajibiwa hata barua moja.

Mrema alisema wazazi wa wanafunzi hao wamekuwa wakienda ofisini kwake mara kwa mara, kumuomba awasaidie ili watoto hao waweze kuendelea na masomo.

"Hata jana (juzi) wazazi hao walifika ofisini kwangu huku wakiwa wanalia, ikabidi nitume barua nyingine kwa rais kama kumkumbushia, lakini mpaka ninavyoongea na nyie hivi sasa, sijajibiwa chochote, sasa sijui ni kudharauliwa kwa viongozi wa vyama vya upinzani au wanaona kama tunajitafutia umaarufu kupitia wananchi wanyonge, ambao wamekuwa wakiumizwa kupitia kodi zao," alisema.

Alisema serikali ina wajibu wa kuwalipia wanafunzi hao ada ili waweze kuendelea na shule.

Mrema alidai kuwa ana vielelezo vyote alivyopatiwa na wazazi wa wanafunzi hao vinavyoonyesha kuwa serikali iliahidi kuwalipia ada.

Naye Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James mbatia, alisema kukaa kimya kwa serikali ni kuwadharau wananchi ambao ndio wamewaweka madarakani, kwani fedha zinazodaiwa si nyingi kiasi cha serikali kushindwa kulipa.

"Fedha zinazotakiwa ili wanafunzi hao waweze kuendelea na masomo ni sh bilioni 6, lakini tunashangaa serikali imeendelea kuwapuuza wananchi wake ambao kodi zao ndizo zinazotumika kununulia mashangingi wanayotembelea," alisema Mbatia.
 
"Fedha zinazotakiwa ili wanafunzi hao waweze kuendelea na masomo ni sh bilioni 6, lakini tunashangaa serikali imeendelea kuwapuuza wananchi wake ambao kodi zao ndizo zinazotumika kununulia mashangingi wanayotembelea," alisema Mbatia.

Hivi hii amount ni kweli au? manake Bilioni sita sio masihara ndugu zangu...
 
Nafikiri tuendelee kupigia kelele hili jambo kwani hawa jamaa wakiona jambo linawatoa nje na wananchi wanapata awareness huwa wanarudi nyuma na kutoa majibu vinginevyo.

Lets shout,
 
"Fedha zinazotakiwa ili wanafunzi hao waweze kuendelea na masomo ni sh bilioni 6, lakini tunashangaa serikali imeendelea kuwapuuza wananchi wake ambao kodi zao ndizo zinazotumika kununulia mashangingi wanayotembelea," alisema Mbatia.

Hivi hii amount ni kweli au? manake Bilioni sita sio masihara ndugu zangu...
 
Mwanakijiji,
kama hiyo figure ni kwa wanafunzi wote wanaochukua masomo vyuo vya juu, nafikiri serikali inaweza, lakini kama hiyo figure ni kwa ajili ya wanafunzi hao 29 tu, then lets think twice.
 
Mafuchila haiwezakani kuwa ni kwa hao 29 tu kwani mikopo yao ilikuwa ni ya kama dola 3000 hivi kwa kila mmoja sawa na dola 87,000 sawa na gari moja lililonunuliwa na ofisi ya Waziri Mkuu!!
 
Duh! Nimekupata Mwanakijiji...basi naona kwenye gazeti wamemnukuu vibaya Bw. Mbatia kuwa kiasi cha Billion 6 zinahitajika ili vijana warudi shuleni. Binafsi hata mimi nikasita kuendelea kupiga upatu, lakini kwa figure ulizotoa swadakta. Umenivunja mbavu na huo mfano wako wa gari.
 
si ndo hapo.. kwanini wasiliulize hilo gari wakawalipia hawa vijana.. na lile gari jingine waliuze ili kuwapa fedha za ziada kutokana na usumbufu?

Kiev: Nimezungumza na afisa wa Ubalozi wa Uingereza pale Kiev, ni kweli vijana wako nje na wamelala nje siku hizi zote na amenihakikishia wako Salama kwani walipo pia ni eneo la Ubalozi wa Marekani na maafisa Usalama na walinzi wanawaangalia kuhakikisha usalama wao. Hata hivyo hadi leo, Ubalozi haujasikia lolote kutoka Tanzania.

Dar-es-Salaam: Kama hadi kesho Jumanne serikali haitafanya lolote au kutoa tamko linaloeleweka nitalichukua jambo hili a step higher... I'm a master magician, and I always have an extra trick from my hat!!
 
Wanabodi,
Nafikiri kama Mbatia kapewa hizo figure za bil 6. Inabidi Chadema waanze ku-question pia hizo figure maanake kuna wanafunzi wengine wanasoma huko Urusi hatufahamu ni kiasi gani kinatumiwa. Isije kuwa kweli serikali wanatumia mabillioni ya fedha kiujanja ujanja maanake hiyo figure mshikaji hata huku ktk shule zilizo ghali haiwezi kufika. Na kibaya zaidi kulikuwepo na option ya kuwasomesha nyumbani ambayo ilitangulia safari yao hawa vijana pamoja na wengine wote wanaodaiwa kuondoka kihalali. Ikiwa 29 inagharimu bil 6, je hao wengine walioko nje (urusi) hivi kweli inatughalimu kiasi gani?
Nafikiri umefika wakati kuchunguza nafasi za wanafunzi wote waliopo nje wakisomeshwa na serikali maanake nina hakika wapo wengi wanaosomeshwa kwa kodi za wananchi na sio halali kama inavyodaiwa kwa hawa vijana. hao watoto wa vigogo - Kabuntas! ambao miaka neda rudi (over 10yrs) wamekuwa vyuoni hawafuzu masomo yao. Ni kiasi gani cha fedha serikali hutumia na hao wasomi wetu wote wangapi wamepitia milango ya nyuma!.
 
Mkandara... tukiamua kulichunguza hili kweli utakuwa kuwa tunafungua kisandukuru cha pandora.. sidhani serikali iko tayari kuchunguza kweli malipo ya wanafunzi nje ya nchi..!!
 
Halafu kila siku nasikia hawa hawa wa Eastern Europe, sijawahi kusikia wa USA, UK au Canada wanaosomeshwa na serikali wakigoma hivi ni kwa nini?
 
Hii hesabu ya billion sita imetolewa na nani?

Tshs 6 000 000 000 . 00 / 29 = 206 896 551 . 70 kwa kila mwanafunzi.

Ambayo ni sawa na £ 82 758 . 62

Vyuo vingi vya UK kwa degree ya kwanza kwa wanafunzi kutoka TZ = £8 000 Fees kabla ya malazi na chakula kwa mwaka lets say £ 10 000 kwa mwaka. (Kuna nafuu ya £ 1000 . 00 kwa wanafunzi wa commonwealth na wakati mwingine ikilipwa yote kuna 5% discount) Sasa hawa wamekwenda Ukraine tena sidhani hicho chuo hata kinaweza kushindana na vyuo vya UK. Degree ya miaka 3 au 4 UK plus 1 or 2.5 percent inflation haiwezi kuzidi £ 35 000 na £ 45 000 respectively. Sasa hii figure ya almost £ 83 000 inatoka wapi? Au ndio jinsi wanavyokula pesa ya walalahoi?
 
Halafu kila siku nasikia hawa hawa wa Eastern Europe, sijawahi kusikia wa USA, UK au Canada wanaosomeshwa na serikali wakigoma hivi ni kwa nini?

Nafikiri hao wa eastern countries hakuna kazi za ziada kwa hiyo wanategemea hiyo wanayopewa na serikali. UK na USA watafanya kazi za ziada na kupata vijisenti.
 
Dua,

Kinachoshangaza zaidi nakumbuka kulikuwa na ubishi wa kuthibitisha credibility ya hivyo vyuo kama vinatambulika nchini. Hii ina maana ni vyuo vya kawaida kabisa!...hizi gharama zinatoka wapi?... ama ndio mbinu ya serikali kutaka kuepa jukumu lake kwa kisingizio ambacho hakina ukweli.
 
Nashukuru kuwa "Tanzania Daima" na "Mwananchi" wamepick habari hii.. natumaini vyombo vya serikali na vingine vitalichukua jambo hili:

Na Abdallah Bawazir

WAZAZI wa wanafunzi 29 wa Tanzania waliojisalimisha katika ubalozi wa Uingereza nchini Ukraine, wamemuomba Rais Jakaya Kikwete, kuingilia kati suala la watoto wao na kuwachukulia hatua maafisa wa Wizara ya Sayansi, Teknknolojia na Elimu ya Juu, waliowakana wanafunzi hao.

Wakizungumza muda mfupi baada ya kikao chao kilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, kujadili matatizo yaliyowapata watoto wao, wazazi hao, huku wakiwa na wasiwasi juu ya maisha ya watoto wao ugenini, walisema wameshangazwa na hatua yawizara hiyo kuwakana wanafunzi hao, wakati waliondoka nchini kwa baraka zote za wizara na ahadi kuwa watalipiwa masomo yao.

Mmoja wa wazazi hao, Sheikh Waziri Omar Nyello, akizungumza kwa niaba ya wenzake, alimuomba Rais Kikwete, awaokoe vijana hao kwani walikwenda Ukraine kwa ajili ya masomo kwa idhini ya Serikali.

Alisema kabla ya kuondoka nchini, vijana hao walifuata taratibu zote zinazotakiwa ikiwa ni pamoja na kuomba mikopo kwenye Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na kukubaliwa.

Sheikh Wazir alifafanua kuwa wanafunzi hao walikwenda Ukraine Septemba mwaka jana baada ya kukubaliwa kupewa mikopo na Bodi ya Mikopo kwa ajili ya kuanzia muhula wa masomo wa 2005/06 lakini kutoka na sababu mbalimbali zilizo nje ya uwezo wao, walishindwa kwenda Ukraine mwaka huo na kuomba mikopo hiyo waanze kupewa muhula wa masomo wa 2006/07.

Walisema kabla ya wanafunzi hao kuondoka, walikubaliana na Bodi ya Mikopo pamoja na Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kuwa mikopo yao itaanza kutolewa muhula huo wa 2006/07.

Sheikh Waziri alisema kabla ya kuondoka nchini wanafunzi hao walipewa sharti la kujinunulia wenyewe tiketi za ndege na kuahidiwa kuwa fedha zao za mikopo zitatumwa wakishafika huko.

“Tunahisi maafisa wa Wizara ya Elimu ya Juu na Bodi kabla ya kubalisha vigezo walisahau kuwa kuna wanafunzi wapo Ukraine na waliokubaliwa mikopo kwa vigezo vya zamani, sasa walipobaini wamefanya makosa wakaamua kuwageuzia kibao kuwa serikali haiwatambui ili kulinda kibarua chao,” alisema Sheikh Waziri.

Wakizungumza na Mwananchi toka Kiev, wanafunzi hao walisema Mwananchi kuwa walijisalimisha katika ubalozi wa Uingereza uliopo Kiev baada ya vyuo wanavyosoma kuwataka wawe wameondoka kufikia Jumatatu iliyopita na wawe wamelipa ada ama sivyo watakamatwa na kupelekwa polisi.

Pia walilalamika kuwa baada ya Serikali kushindwa kuwatumia fedha za ada pamoja na za mahitaji muhimu, wamekuwa wakiishi maisha ya mateso bila ya chakula huku, usalama wa maisha yao ukiwa hatarini.
 
Nafikiri hao wa eastern countries hakuna kazi za ziada kwa hiyo wanategemea hiyo wanayopewa na serikali. UK na USA watafanya kazi za ziada na kupata vijisenti.
Si hilo tu hao wanaosoma Nchi hizo fedha zao hazicheleweshi zinapelekwa kwa muda muafaka pamoja na kuwa wanaouwezo wa kupata hata vibarua Sababu kubwa wanazozitoa watendaji wa bodi na wizara ya elimu ya juu maisha ni ghali na wanatakiwa kulipa tuition kabla hata mhula haujaanza na hawana msalie, Lakini vile vile watoto wa vingunge wengi ndiyo wanaopata hizo nafasi za huko hivyo wanahakikisha wa huko wanapelekewa fedha kwanza.
 
Nimempata Prof. Msolla tena, na kwa mara nyingine, kapokea vizuri na nilipomuuliza kuhusu msimamo wa serikali kama umebadilika.. akakata simu tena!
 
Nimempata Prof. Msolla tena, na kwa mara nyingine, kapokea vizuri na nilipomuuliza kuhusu msimamo wa serikali kama umebadilika.. akakata simu tena!

Wakti Jeikei anaongea na viongozi huko mafichoni Ngurdoto moja ya mambo aliyowaambia ni kuhusu kuwakwepa waandishi wa habari; akisema kuwa kiongozi anayemkimbia mwandishi ana lake jambo, na kwa kumkwepa anampa mwandishi haki ya kuandika chochote atakacho....
hiyo ni kumbukumbu yangu; pengine Msolla hakuwepo, bado alikuwa kwenye solar space...sasa hivi anaishi kwenye outer space, ndo maana suala la Kiev halipandi...in the near future atakwenda kwenye lunar space..tutamwitaje sijui;
..maana yake ni kwamba anaishi kwenye dunia ingine kabisaaa
 
Kiev: Wanafunzi bado wamepiga kambi, na michango ambayo wachache tuliosaidia imewawezesha kufikia hapa. Wanashukuru sana na wazazi wao wanashukuru sana. Hawajaoga siku ya tano, na afya zao zinazidi kunyong'onyea. Mida hii Ubalozi wa UK unakutana kuona ni jinsi gani wanaweza kuwasaidia zaidi kwani hadi hivi sasa bado hawajapata jibu rasmi. Waliobakia vyuoni wanasubiri wenzao kurudi tu ndio watimuliwe kwenye mabweni.

Dar: Wazazi wa familia wameanza kupata mwanga wa matumaini kidogo baada ya kujaribu kuwahusisha wabunge kadhaa wa CCM. Na upande mwingine mazungumzo na wanasheria kadhaa yameanza kufanyika. Hilo limelazimisha kusubiri kidogo kabla hatujaongeza moto kwenye hoja.

Serikali: Bado kimya! Siku ya Sita!
 
Back
Top Bottom