Kiev: Vijana bado wapo. Wamewaruhusu dada zao (3) kurudi vyuoni kwani hali ya hewa si nzuri. Usiku wa kuamkia leo wamenyeshewa na mvua lakini bado wapo nje ya Ubalozi wakisubiri majibu labda kesho asubuhi.
Moskow: Ubalozi bado haujasema lolote na jitihada za kuwapata hazikuzaa matunda.
Dar: Msimamo wa serikali wa kutowatambua na kushindwa kutafuta utatuzi wa suala hili bado ni ule ule. Hakuna kiongozi anayejisikia haja ya kulizungumzia jambo hilo. Vyombo vya habari vya nyumbani licha ya kujua kuhusu suala hili bado wako kimya na hawajaanza kulifanyia kazi.
Michango:
Hadi hivi sasa ni watu wanne tu wamechanga karibu dola 300 hivi ambazo zimetumwa na zimepokelewa leo. Nashukuru wote mliojitokeza kusaidia na kwa niaba yao Mnyezi Mungu awabariki na kuwazidishia.
Kwa sababu ni vigumu kuamini kuwa nchi (taifa) linaweza kutowajali raia zake kiasi hiki.
Halafu, pamoja na yote hayo, ubalozi walikokimbilia wakidhani kuwa labda watapewa msaada, nao unakosa hata ule ubinaadam tu wa kawaida. Hivi kweli inawezekana, watu wakafika nyumbani kwako, hata kujikinga mvua tu, halafu wewe ukawaambia wakae huko nje kibarazani huku wewe ukiendelea kujitanua ndani? Ni ubinaadam gani huo?
Mkjj, tafadhari bwana tupe ukweli - hao vijana wamekaa nje ya ubalozi kwa siku hizi nne sasa, bila hata ya kupewa msaada hata wa chakula na maji? Ni kweli hiyo, au na wewe unatufumba macho kwa sababu unayoifahamu mwenyewe? Mbona ni vigumu hasa kuamini kuwa watu wanaojiita waliostaarabika kama hao Waingereza waweze kutenda hivyo? Mali zote zile walizosomba wakati walipotutawala, yaani hata kuwapa vijana hawa maji tu ya kunywa hakuna? Siamini.
Kioja kingine nisichokielewa kuhusu jambo hili ni ukimya wa vyombo vya habari, sio vile vya nyumbani tu pekee, lakini hata hivyo vya Uingereza na kwingineko. Watu zaidi ya ishirini wawe katika eneo la ubalozi hata pasiwe na habari yoyote iliyoandikwa au kutangazwa katika chombo chochote?
Nilisikiliza mahojiano yako (KHLNews) na hawa vijana na yale uliyowafanyia wazazi wao. Nadhani kuna jambo lililofichika kidogo, lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya serikali yetu kuwa na msimamo huu unaotutia aibu kama taifa.