Tunahitaji kupata idadi kamili ya hao wanafunzi
kisha sisi watu wa UK tunaweza kujiorganise tuwatumie michnago yetu
Kama waliopo huko Europe wakifanya michango hewala
Watu wa States najua mko bize kujiandaa na hiyo pati ya Columbus lakini hii ni immediate issue
Yakubu hebu angalia tunaweza kufanya nini...hebu liase na Mwana kijiji
Haiwezekani waTZ wenzetu wawe na hali walionayo na sisihuku matumbo yamejaa, kama serikali haiwezi kufanya kitu basi hata sisi tushindwe?
Mlio na Contacts za NGO za Kimataifa whatever ..fanyeni mipango jamaa tuwasaidie
Mimi nitaangalia mambo ya legality na mengineyo madogo madogo
time is running out na mnajua kuna dada zetu kule vile vile
MODS: hebu ifanyeni sticky lakini walau mpaka Jumamosi tuwe na tushapata solution
Maana naona serikali nhaina interest ya kuwasaidia na kama wanayo interest basi wawakilishi wa serikali yaani MABALOZI na WIZARA YA MAMBO YA NCHI ZA NJE pamoja na WIZARA YA ELIMU ya juu hazina mipango ya kuwasaidia hawa wanafunz ambao wamefikia HATUA YA KUOMBA UKIMBIZI UBALOZI WA UINGEREZA HUKO URUSI
hii ni aibu kwetu wote na huu si muda wa kutafuta lawama bali ni tuwasitiri wenzetu hawa kwani aibu yao ndio aibu yetu
na naombaParty politics tuziweke pembeni ...