Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Ok labda hatukuelewa na nimakosa yangu.
wacha tujui nini tutafanya kw a hawa watoto kwanza,baadae tutaomba tafsiri ya neno hilo.
 
Hivi hii serikali si huwa inapenda sifa kupokea na kuwalea wakimbizi wasio na idadi wa rwanda, burundi na kongo n.k. Na iliwahi kuwahifadhi na kuwafadhili wapigania uhuru wasio na idadi wa afrika kusini, angola, msumbiji n.k. Mbona linapokuja suala la wakimbizi wake wenyewe (vijana 29 waliopo ukraine) inapata kigugumizi cha kuwalipia nauli ya kuwarudisha nyumbani kama kweli imeshindwa kuwalipia ada.

Haya sasa hivi tumesikia wameshambuliwa, jamani inatia uchungu sana kwa sababu suala la hao vijana ni la muda mrefu sana lakini hakuna hatua zilizochukuliwa. Hivi haya maisha bora kwa kila mtanzania hayawahusu hawa vijana.

Inawezekana kabisa hii ndio ikawa serikali ya kwanza duniani kuwatelekeza raia wake walio katika nchi ya watu. Hivi hawaoni mataifa mengine yanavyohangaika usiku na mchana inapotokea raia wake hata mmoja tu ametekwa na waasi kwenye nchi zenye vita japokuwa unaweza kuta huyo raia kajipeleka mwenyewe katika mazingira hatari kama hayo. Kama hayo mataifa mengine yanafanya hivyo vipi viongozi wetu kwa hao vijana walioenda kutafuta elimu ili kuja kuwasaidia wao na taifa kwa ujumla?
 
Unajua LOWASA KUSEMA KUWA ANASIKIA NJAA ANENDA KULA KATIKA INTERVIEW YA MWANAKIJIJI NI AIBU TUPU

JAMAA IS SO ARROGANT NA AMEONYESHA JINSI GANI ALIVYO MBINAFSI NA ANAFIKIRIA CHAKULA CHAKE

ZAIDI YA HAYO STILL NAONA JK BADO NI MUUNGWANA MAANA KWA HAKUKATA SIMU NA PILI ALIKUBALI KUZUNGUMZA SASA TATIZO NI HUYO MSOLA KUGOMA KUSEMA KITU NA HUYO LOWASA KUONA TUMBO LAKE NI BORA ZAIDI

JAMANI HAWA WATU NI WASHENZI TUUU NA HAWANAMAANA HATA KIDOGO NA NDO WALO MZUNGUKA RAIS

KAZI IPO BASI
 
Nawapa Pole sana ,Hivi hao walinzi wa hizo balozi walikuwa wanafanya nini wakati vijana wanashambuliwa?Kwani tuliwahi kuelezwa hapa kwamba vijana wapo kwenye hali ya usalama hasa ukizingatia ulipo Ubalozi wa UK vile upo Ubalozi wa USA.Sasa nini kimejiri tena?


KNKCU, vijana walikuwa wanaondoka hapo kurudi vyuoni, walikuwa mbali na maeneo ya Ubalozi. Hata walipokuwa hapo ubalozini wale skinheads walikuwa wanawasumbua kwa maneno lakini hawakuweza kufanya lolote. Inaonekana walikuwa wanawapigia mahesabu.

Nitawapa taarifa zaidi kuhusu hali ya vijana kwani najaribu kuwasiliana hospitali walikopelekwa na familia zao nyumbani. Vijana wengine wameshawasili vyuoni kwao na huko wamekutana na maagizo ya vyuo kuwa kama hadi j'nne vyuo havijalipwa, vijana hao watafukuzwa mabwenini, na kushtakiwa! Kipigo kimetokea usiku wa kuamkia leo.

hata sijui nifanye nini? Wafadhili mnaowataja namba zao sina na nimeshajaribu mara mia moja kujaribu kuzipata namba hizo.
 
Ni habari za kusikitisha!

Tujiulize swali hili: kama Serikali yetu iliwapa masaa machache wanafunzi wa UDSM wkuondoka chuoni baada ya mgomo bila kufikiria kuwa wengine wanatoka Ngara na baadhi yao wakauza simu zao na vitu vingine vya thamani ili wapate nauli, sembuse hao walioko huko Ukraine?
 
KNKCU, vijana walikuwa wanaondoka hapo kurudi vyuoni, walikuwa mbali na maeneo ya Ubalozi. Hata walipokuwa hapo ubalozini wale skinheads walikuwa wanawasumbua kwa maneno lakini hawakuweza kufanya lolote. Inaonekana walikuwa wanawapigia mahesabu.

Nitawapa taarifa zaidi kuhusu hali ya vijana kwani najaribu kuwasiliana hospitali walikopelekwa na familia zao nyumbani. Vijana wengine wameshawasili vyuoni kwao na huko wamekutana na maagizo ya vyuo kuwa kama hadi j'nne vyuo havijalipwa, vijana hao watafukuzwa mabwenini, na kushtakiwa! Kipigo kimetokea usiku wa kuamkia leo.

hata sijui nifanye nini? Wafadhili mnaowataja namba zao sina na nimeshajaribu mara mia moja kujaribu kuzipata namba hizo.


Wafadhili,Wafadhili gani?
Wafadhili wa kwanza ni sisi wan JF wote kama tutaweza kwa umoja wetu kununu hat Ticket ya wawili kati ya hao vijana na tutaonekana tumeweza kufanya hilo wengine kwa kutaka sifa watafanya kwa sasbabu hapo litaonekana kama swala la kitaifa kwani hat viongozi wataingia.You will see
 
Wenye namba za Mengi, Manji, Bakhresa,Malinzi ,Mama Kikwete, Mkapa,Mama Mkapa,Mwinyi, Malecela wampe mwanakijiji
Lengo letu sasa hivi tulielekeze ktk kuomba msaada wakuwarudisha vijana nyumbani angalau na afya zao.Kama kusoma waanze upya taratibu za kutafuta elimu kwani kujikwaa si kuanguka.Kama kuna wanabodi humu wenye uwezo wa kuwanunulia tiketi vijana wajitokeze.Maana Charity inaanzia nyumbani na nyumba yetu ya kwanza ni JF.
 
jamani naomba mniwekee article toka mwananchi kuhusu wanafunzi hawa, siwezi kuiona online....
 
Mi naona kuwa hii kiburi ya viongozi kwenye hili suala imechangiwa sana na ukimya wa vyombo vya habari. Suala la Kiev lingepewa uzito kama lile la Mh AC na mumewe, au lile la Manji na mengi, leo hao wanafunzi wasingekuwepo pale; hawa wasanii wanapenda publicity sana, siku wameona wanahabari wannawasakama noi lazima wasitishe mara moja kwa kujisafisha ili public profile yao isichafuke..Kwa hili nawatupia lawama kubwa sana wanahabari wa nyumbani..what a shame..Majuzi mmeandika habari za unyumba wa watu asubuhi mchana na jioni, kama dozi ya panadol, leo watoto wanafia ugenini wamechukulia kama jambo la kawaida, leo kwao kesho kwenu ndugu zangu, there is no limit to what these wasaniis can do...haya we!
 
Mtumwitu,
Nasikia Sauti ya Amerika imemhoji msemaji wa wanafunzi hao. Nitasikiliza.
 
Mi naona kuwa hii kiburi ya viongozi kwenye hili suala imechangiwa sana na ukimya wa vyombo vya habari. Suala la Kiev lingepewa uzito kama lile la Mh AC na mumewe, au lile la Manji na mengi, leo hao wanafunzi wasingekuwepo pale; hawa wasanii wanapenda publicity sana, siku wameona wanahabari wannawasakama noi lazima wasitishe mara moja kwa kujisafisha ili public profile yao isichafuke..Kwa hili nawatupia lawama kubwa sana wanahabari wa nyumbani..what a shame..Majuzi mmeandika habari za unyumba wa watu asubuhi mchana na jioni, kama dozi ya panadol, leo watoto wanafia ugenini wamechukulia kama jambo la kawaida, leo kwao kesho kwenu ndugu zangu, there is no limit to what these wasaniis can do...haya we!


Kutoka Ukraine kuja Dar unapita ROUTE ipi? Mimi nadhani wadhamini/wafadhili wazuri wanaweza kuwa AIRLINE mojawapo inayo ply kwenye hiyo ROUTE! Dar kuna akina Manji wanamwaga fedha pale Yanga kama hawana akili nzuri vile! Mwanakijiji umejaribu pia kushirikisha redio za Tanzania? Inawezekana kabisa hamasa ya kupata huo ufhadhili ikawa ni ndogo.........Watu huwa wanachangia mambo mengi tu kama uchunguzi wa saratani ya matiti, yatima na kadhalika pale wanapohamasishwa!

Wasiliana na ITV na Redio One, Clouds FM kupitia kipindi chao cha Powebreakfast cha asubuhi asubuhi ni watu wenye ushawishi mkubwa katika jamii na unaweza kushangaa pesa zikapatikana za kutosha kabisa kuwarudishwa wote.
 
Vyombo vya habari vya Tanzania ni mamluki wa serikali. Kila siku ni kuisifia tuu huwezi kuona wameikosea. Mungu wangu sijui tunaelekea wapi sisi watanzania. Yaani EL anathamini chakula kuliko maisha ya watanzania? this is dangerous. Sasa tutafute namna ya kuwanusuru hawa jamaa? Kuna umoja wa watza UK, US, etc can we put our hands together kuwasaidia? Wenyeviti na makatibu wa vyama hivi watusaidie tusiwe na vyama vya kufanya serehe na kuwapokea viongozi tuu bali pia tuwasaidie vijana wetu. Balozi ya Russia inafanya kazi gani?
 
sawa mzee jasusi nimekusikia.. wanarusha saa ngapi hawa VOA...? saa za hapa kijijini?
 
ninachoweza kusema ni kwamba kama hawa vijana wataweza basi warudi nyumbani tz, maana sasa naona ishakuwa hatari baada ya kuambiwa serikali iwalipie ada itakuwa tutaambiwa tulipie michango ya kusafirisha miili ya waliokuwa wanafunzi ( siombei iwe hivyo ) lakini kutokana na maelezo ya vipigo vya hao skinheads or buttheads yaliyotolewa !kwa kweli inasikitisha. na sina la kuwaambia zaidi ya kutafuta means ya kurudi nyumbani tu !! najua elimu ni muhimu lakini why hatarisha maisha yako !! put safety first !
 
Mimi nafikiri hapa tulipofikia ni pabaya; the best cause now ni kutafuta utaratibu wa kuwarudisha hawa vijana nyumbani. Nionavyo mimi sasa, kama serikali itaendelea kuwakataa hawa vijana na wazazi wao watakuwa hawana uwezo wa kuwalipia katika masomo yao huko Ukraine, ni bora warudi nyumbani.

Tuombe Mungu hawa vijana waliovamiwa wapone salama; otherwise it is a huge embarrassment to our Government, more so to our beloved country!

Can this case trigger a beginning for Tanzanians to take issues of our political leadership with a pinch of seriousness!
 
Mzee Mwkjj,
Itakuwa kwenye internet pia. Saa saba mchana EST.
 
mwanasiasa.. yaani hii habari ilinifanya ninyong'onyee mapema leo... natamani ningepewa uwaziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu, just for two hours... I promise you hawa vijana wangekuwa shule wanasoma..!!
 
jamani naomba mniwekee article toka mwananchi kuhusu wanafunzi hawa, siwezi kuiona online....

Waliokwama Ukraine wasaidiwe

MAPEMA wiki hii vyombo vya habari viliandika habari za kukwama kwa wanafunzi wa Kitanzania waliokwenda nchini Ukraine katika bara la Ulaya kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu katika fani mbalimbali.

Safari hii, habari hizo zilihusu wanafunzi hao kujisalimisha katika ubalozi wa Uingereza katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev baada ya kuhangaika kwa zaidi ya miezi sita wakitafuta fedha kwa ajili ya kujikimu pamoja na kulipa ada katika vyuo wanavyosoma.

Hii si mara ya kwanza kwa vyombo vya habari kuripoti juu ya kukwama kwa wanafunzi hao, baada ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kuwakana, ikisema haina mkataba nao na kwamba walikwenda katika nchi hiyo bila kufikia makubaliano yoyote ao.

Lakini wanafunzi hao wamekuwa wakisisitiza kwamba waliondoka nchini kwenda Ukraine baada ya makubaliano na Bodi ya Mikopo pamoja na Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kwamba wangetumiwa fedha hizo baada ya kufika huko.

Wanafunzi hao wanadai kuwa ni kutokana na makubaliano hayo ndiyo maana waliamua hata kutumia nauli kutoka mfukoni mwao kwenda Ukraine kwa ajili ya kuwahi masomo, wakiamini kuwa huku nyuma, Bodi ya Mikopo ingeendelea kushughulikia mikopo yao na kisha kuwatumia fedha kupitia akaunti zao.

Vijana hao wa KItanzania wapatao 29, walipata kibali cha kukopeshwa fedha za masomo nchini Ukraine katika mwaka 2005/2006, lakini kutokana na matatizo yaliyokuwapo wakati ule, walishindwa kwenda katika vyuo walivyoomba na kupata nafasi.

Wao wanadai kuwa baada ya kukosa masomo katika muhula huo, waliwasiliana na Bodi ya Mikopo na wakakubaliana kuwa waanze masomo katika muhula wa mwaka 2006/2007 kwa kuwa maombi yao ya mikopo yalikwisha kukubaliwa na Bodi ya Mikopo na kwamba wangetumiwa fedha zao mara baada ya kufika huko.

Lakini Bodi ya Mikopo imewakana kabisa wanafunzi hao ikisema kuwa kila mwaka, Bodi hiyo imekuwa ikiingia mikataba mipya na wanafunzi wanaoomba kwenda kuanza masomo ya elimu ya juu katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Bodi inadai kuwa maadam wanafunzi hao hawakwenda kuanza masomo katika muhula waliokubaliana katika mkataba, basi mikataba yao inahesabaika kuwa imeharibika na hawamo katika bajeti iliyotengwa kwa ajili ya kuwakopesha wanafunzi wanaotakiwa kuanza masomo katika mwaka 2006/2007.

Mbaya zaidi ni kwamba bodi inataa kabisa kuwa na mawasiliano na wanafunzi hao kabla ya kuondoka hapa nyumbani kwenda Ukraine kwa ajili ya kuanza masomo ya elimu ya juu.

Matokeo yake, tangu wafike huko, wanafunzi wamekuwa wakitumia muda mwingi kuhangaika mahali pa kula, huku wakisumbuliwa na utawala wa vyuo husika kwa kuwa wote hawajalipa ada. Ilifika mahali wanafunzi hao wakawa wanashinda mitaani kujaribu kupata fedha za kujipatia mahitaji muhimu, ikiwamo chakula.

Hata wizara pia imeshindwa kulitolea ufumbuzi tatizo hilo na hadi sasa haijulikani serikali inafanya nini ili kuwasaidia wanafunzi hao angalau waweze kurejea nyumbani baada ya kufukuzwa katika vyuo vyao kutokana na kukosa ada.

Ndiyo maana mwishoni mwa wiki, wazazi wa watoto hao walikutana jijini Dar es Salaam na kumwomba Rais Jakaya Kikwete aingilie kati suala hilo ili ama wanafunzi wapewe kopo huo, au aserikali ifanye utaratibu wa kuwarejesha nyumbani.

Tunachukua nafasi hii kuungana na wazazi wa wanafunzi hao ambao bado wamejisalimisha katika ubalozi wa Uingereza mjini Kiev. Tunasema hivyo kwa kuwa vijana hao walikwenda huko kwa ajili ya kupata elimu ambayo kwa bahati mbaya wameikosa.

Kwa watu walioishi maisha magumu kiasi hicho katika nchi ya kigeni, ni wazi wamepata mateso ambayo pengine hawajawahi kuyashuhudia maishani na kuna uwezekano mkubwa wakaanza kujishughulisha na vitendo viovu ikiwamo biashara ya dawa za kulevya au hata ujambazi.

Tunaamini kwamba ni jukumu la serikali kuwasaidia raia wake waliokwama ugenini kama ilivyo kwa vijana hawa ambao walifuata taratibu zote za uhamiaji kabla ya kuingia katika nchi hiyo na kwamba mateso waliyoyapata yanatokana tu na taratibu za kirasimu ndani ya serikali yetu.
 
mwanasiasa.. yaani hii habari ilinifanya ninyong'onyee mapema leo... natamani ningepewa uwaziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu, just for two hours... I promise you hawa vijana wangekuwa shule wanasoma..!!

Ndugu yangu MJJ, usiwape benefit ya kunyong'onyea..Kwenye imani yangu tunaamini kuwa jaribu kubwa = muujiza mkubwa; tena ukiona yamefikia hapa ujue kifo chao wababe kimefika. pamoja na kujikausha kwao naamini wameshtushwa na suala zima la hawa vijana...acha tuendelee ku-petition, lazima iende na mtu!
 
Back
Top Bottom