Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Opposition parties create fund for stranded students

2007-05-28 11:14:23
By Austin Beyadi

In an effort to assist the 29 Tanzanian students stranded in Ukraine, four opposition parties have formed a special emergency fund which will receive donations from well wishers.

The stranded students had allegedly gone to Ukraine after being promised they would receive education loans from the government upon their arrival.

Speaking to journalists in Dar es Salaam yesterday, the Civic United Front (CUF) Chairman, Prof Ibrahim Lipumba, said the funds had to be raised before Tuesday (tomorrow) which had been set as the deadline for the students to settle their arrears.

`They have been given a deadline of 29 May, 2007, failure to which they will hand over their passports and be evicted from hostels they are currently staying,` he said.

He said the matter was even more urgent because last week, the abandoned students had gone as far as seeking help from the Embassy of the United Kingdom, where they had camped for a week.

`We are confident that Tanzanians and well wishers will donate money to save lives of students who are left high and dry and are currently starving in cold weather in a foreign country,` he said.

He said that if Tanzanians could contribute Independent Day celebrations, where a lot of money was raised, then they would not fail to donate to students who had gone abroad in search for education.

Lipumba said if the stranded students will not clear their debts, they will be forced to cut short their studies and court cases will be filed against them for failing to comply with their agreements with the universities.

He claimed that the UK Embassy in Ukraine had offered to settle the students` bills and provide them with basic needs provided the government of Tanzania would write a letter confirming that the money would be repaid.

`The government is yet to write the letter,` he said.

He alleged that a government team, which was supposed to be sent to Ukraine to assess the situation early this month, had its trip cancelled.

SOURCE: Guardian
 
Gambate! nimeongea kijapan japo hakiruhusiwi. Namaanisha umoja ni nguvu tukaze buti tutafika tuu. Ni hatua nzuri. Admin sorry kwa kutumia Kijapan.
 
mwiiiiiiiiiiii nimerudi. hili porojo mnalotia looooooooooote bado hamjaonekana kufahamu lolote kutoka kwangu.na ndio tatizo la wasomi wa kileo mnaitazama siasa na dunia kwa mtazamo wa kisomi tu na kusahau kwamba jamii imejengeka kwa wasomi na wasiokuwa wasomi.hivi nikikwambieni hawa vijana hayo matatizo wamejitafutia mtakataa? nchi yenyewe inakopeshwa halafu na wewe ukategemee kupata mkopo kwa nchi inayokopeshwa si utakuwa chizi wewe? wale walobaki makwao wakalala wao hawajui thamani ya elimu? au ndo mnapigania haki? tetea haki ya mnyonge kabla haki ya msomi! kumeanzishwa account maalum hapa ya kuwasaidia vijana hao 29,ingekuwa la maana ikaanzishwa account ya kuwasaidia wasiokuwa na maji wakajengewa visima hapa bongo? okoa maisha kabla ya kuokoa kinachopamba maisha. watu wameongea na rais hapa kuhusu hao vijana 29,ningependa nimsikie mtu huyo huyo ajigharamie kuongea na rais kuhusu walokosa elimu ya msingi kabla ya waliokosa vyuo vikuu.tatizo lenu nyinyi sio kuwatetea hawa vijana bali ni kuwapa headline na umuhimu ambao mngeliwapa wanaostahiki kutetewa umuhimu kama huu basi nadhani tanzania ingekuwa ishakomboka zamani.mnaweza mkasema ndo mnaanza sasa lakini naona mmeanza chuo kikuu kabla ya shule ya msingi.wengie wenu hapa mna maisha ya kusoma magazeti kwenye internet ndo mkajua yaliojiri duniani. hamna ukweli wowote kuhusu wanyonge zaidi ya siasa za kusoma magazeti.hebu ingieni mitaani na vichochoroni muone hali halisi ya maisha ndo mtajua nani apewe umuhimu kwanza? mwanafunzi alokwenda ukraine kwa hiari yake? au raia mtanzania anaekosa pa kula na kulala bila hiari yake? mpigie simu raisi leo mwambie kuna wapemba waliachishwa masomo shule za chake chake wakiwa kidato cha pili kutokana na itikadi zao za kisiasa halafu anzisheni account wanafunzi hawa waendelezwe kabla ya wanafunzi wa ukraine,anzisha mfuko wa kusaidia mayatima leo wasome hapa jf ,nitakufahamu,kinamama wanauza miili yao na kuihatarisha na maradhi ili tu wapate kijio cha siku moja,saidia hawa kabla ya wengine.kama hamjaskia hayo basi mjue ni wanasiasa wa magazetini nyie na hamjui lolote kuhusu maisha.mkiona wenzenu wa ulaya wanauzulu watu kwa mambo kama haya ni kwasababu washayakamilisha ya msingi katika maisha ya binadamu,wana umeme,maji na mahitaji muhimu ya binadamu. hakuna atakaekukatazeni kutetea hapa ninachokuambieni angalieni lipi la kulipa umuhimu kwanza? hivi hao vijana leo wakiomba warejeshwe makwao hawatorejeshwa? si msomi lakini nadhani ukitaka deportation basi kwenu utarejshwa hata kama huna nauli.hivyo vijipesa mlivyokusanya kama vipo katafuteni mayatima muwape angalau wapate kijielimu cha kuandika a na b.ushauri wa bure.khaaaaaaaaaaa ndo maana nikaambiwa na mzee adhabu ya kaburi aijua maiti.ni kweli adhabu tunayoipata wanyonge tunaijua wanyonge tu .kama mngeijua basi mngetuchangia na sisi.aaaaaaaaaakh hebu ntoke zangu weee ulimwengu wa wasomi niwaachie wasomi wenyewe nisije nikaadhirika.

Elimu ya msingi Tanzania si bure ama serikali ya awamu ya nne imefuta hilo?
 
Basi tuwaunge mkono kwa vitendo na sisi tuchangie hata kama ni senti tano.

Mwanakijiji hongera kwa juhudi kubwa katika hili jambo.
 
Asante sana JF!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Mambo si ndio haya.It seems message imekuwa delivered! At least upinzani umeonyesha unaweza kuwa constructive. Can anyone endeleza mjadal aliouanzisha Mh Mrema? "watoto wa wakubwa wanaosoma nje ya nchi were give up to 10 m mikopo.."
Tukifanikiwa hili can we arrange for a JF Reunion! (joking)
 
Tutafika Kweli Kama waataalamu tunaowategemea ndio hawa!

From Tanzania Daima 28th May, 2007

MUUNGANO wa vyama vinne vya upinzani nchini wameanzisha harambee, yenye nia ya kukusanya fedha kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa Kitanzania wapatao 29 ambao wamekwama nchini Ukraine.
Wanafunzi hao wamejikuta katika hali mbaya baada ya kushindwa kulipia gharama za masomo na kuishi nchini humo, baada ya serikali kukataa kuwapatia mikopo chini ya mfumo wa kuwakopesha wanafunzi wa elimu ya juu.

Umoja huo wa vyama ulisema jana kuwa lengo ni kukusanya kiasi cha kutosha cha fedha ili kuhakikisha kuwa wanafunzi hao wanamaliza masomo yao katika Chuo cha Kharzin, nchini Ukraine.

Vyama hivyo vya upinzani vimefikia hatua hiyo baada ya jitihada za wanafunzi hao na wazazi wao kuitaka serikali iwasaidie kulipia gharama za masomo kupitia mfumo wa kuwakopesha wanafunzi wa elimu ya juu kugonga mwamba.

Uamuzi huo ulitangazwa jana na viongozi wa vyama hivyo vya siasa, katika mkutano na waandishi wa habari, ambao pia ulihudhuriwa na baadhi ya wazazi wa wanafunzi hao.

Wakizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika ofisi za Chama cha Wananchi (CUF), Buguruni jijini Dar es Salaam, viongozi hao walisema kuwa wameguswa sana na mateso ambayo wanafunzi hao wanapitia kutokana na kiu yao ya kupata elimu.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alitangaza kuwa umoja huo wa wapinzani umechanga sh milioni moja kwa kuanzia, na watafungua akaunti ya benki, ili wasamaria wema wengine wanaopenda kuwasaidia wanafunzi hao, wachangie.

Profesa Lipumba alisema fedha hizo ni mchango wa dharura kwa ajili ya kuokoa maisha ya Watanzania hao ambao imeelezwa kwa muda wa siku kadhaa sasa, hawana hata makazi maalumu.

Habari zinasema kuwa licha ya kufukuzwa shuleni na pia katika hosteli walizokuwa wanaishi baada ya kushindwa kulipia gharama zake, wanafunzi hao wamezuiliwa kurudi nyumbani hadi watakapolipa fedha wanazodaiwa.

“Watanzania tuwe na huruma, tunaomba kila mmoja atoe mchango wake kupitia namba ya akaunti ambayo itatangazwa baadaye. Fedha hizi si za chama, ni kwa ajili ya kuwasaidia wananfunzi hao wanaoteseka… lengo letu ni kuwasaidia aidha waendelee na masomo au waweze kurudi nyumbani,” alisema.

Profesa Lipumba aliitaka serikali kufahamu kuwa maisha ya dhiki ambayo wanafunzi hao wanaishi yanaweza kuwasababishia mauti na kwamba si ufahari kupokea maiti za Watanzania wanaoishi nje.

Profesa Lipumba alionyesha kushangazwa na wanafunzi hao kususwa na serikali hivi sasa wakati walipoondoka mwaka jana walipewa baraka zote na serikali hiyo hiyo na kuahidiwa kupelekewa fedha za ada kupitia mfumo wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

“Inashangaza kuwa sasa serikali inawakana wanafunzi hao na kusema kuwa haiwatambui,” alisema baada ya kubainisha kuwa juhudi za wanafunzi hao kuwasiliana na Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia hazikuweza kuwapatia ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili.

Profesa Lipumba alidai kuwa wanafunzi hao walifikia hatua ya kuwasiliana na waziri wa wizara hiyo, Profesa Peter Msolla, lakini akadai kuwa waziri huyo amekuwa akikata simu kila wanapompigia.

Alisema katika jitihada za kuwasaidia watoto wao ambao wapo mbali, wazazi wa vijana hao waliwasiliana na viongozi wa Bodi ya Mikopo na wizara husika, lakini jitihada hizo nazo zimegonga mwamba baada ya maofisa katika ofisi hizo kushindwa kutoa ushirikiano wa kutosha.

“Inasikitisha kwa sababu hakuna hata ofisa mmoja wa serikali aliye tayari kusema wazi msimamo wa serikali kuhusiana na wanafunzi hao… wazazi wamekuwa wakipigwa danadana kama mpira kutoka ofisi moja hadi nyingine bila mafanikio yoyote,” alisema.

Akielezea jitihada za wanafunzi hao, alisema baada ya kushindwa kwa Waziri Msolla, walimpigia simu Waziri Mkuu ambaye naye hakuweza kuwasaidia na mwisho wakaamua kuwasiliana na Rais Jakaya Kikwete.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Profesa Lipumba, Rais Kikwete aliurudisha mpira huo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo, Nimrod Mkono na Waziri Msolla, na kuwataka wanafunzi hao wawasiliane na maofisa hao.

Mbali na hilo, Profesa Lipumba alisema wamepata habari kuwa Ubalozi wa Uingereza nchini Ukraine, ulisema uliipa Serikali ya Tanzania ofa ya kuwasaidia kuwalipia vijana hao na kuwapa misaada mingine ya kibinadamu endapo tu Serikali ya Tanzania itaandika barua ya kuahidi kurudisha fedha hizo kwa Serikali ya Uingereza, lakini serikali haijatoa jibu lolote hadi leo.

Alisema habari walizonazo ni kuwa wanafunzi hao walilazimika kujisalimisha katika Ubalozi wa Uingereza uliopo mjini Kiev, kuomba msaada wa hifadhi baada ya kutimuliwa katika hosteli walizokuwa wamepanga. Alisema vijana hao wapo ubalozini hapo kwa muda wa siku 14 hivi sasa.

“Mbali na kusimamishwa masomo, wanafunzi hao kwa sasa wamepewa hadi Mei 29 mwaka huu kulipa fedha wanazodaiwa vyuoni, la sivyo watanyang’anywa hati zao za kusafiria na kisha kufukuzwa kwenye mabweni wanamoishi, pia hawaruhusiwi kurejea nchini hadi walipe madeni wanayodaiwa," alisema Profesa Lipumba.

Alisema ukiondoa wanafunzi wa Ukraine, kuna wanafunzi wengine nchini Cuba, na Urusi ambao wana matatizo yanayolingana na hayo.

Alisema matatizo kama hayo yanatokea kutokana na Bodi ya Mikopo kuwa na sera za kibaguzi dhidi ya nchi zinazofuata siasa za kijamaa.

Profesa Lipumba alisema ingempasa Waziri Msolla kujiuzulu kutokana na matatizo lukuki yanayoikabili wizara hiyo, lakini imekuwa ni utamaduni wa viongozi wa Tanzania kutowajibika.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, alionyesha mshangao wake kwa msimo wa serikali kutokuwa na huruma na wananchi wake.

Alisema inashangaza kuona kuwa hata Rais Kikwete hajalizungumzia suala hilo, licha ya kushindwa kutoa msaada kwa wanafunzi hao.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema kwa sasa watalizungumzia suala hilo kama wazazi ambao wameonyesha kuumizwa nalo na si kama wapinzani, ili wanafunzi hao waweze kupata misaada ya kutosha kutoka kwa wahisani mbalimbali.

Akizungumza huku akibubujikwa machozi, mmoja wa wazazi wa wanafunzi hao aliyejitambulisha kwa jina la Isais Magombana, ambaye mtoto wake Isabela Magombana naye amekwama Ukraine, alisema wanashangazwa na serikali kuwageuka na kuvunja mkataba waliofikia nao mwanzoni na kuwasababishia watoto wao adha kubwa ughaibuni.

Mzazi mwingine, Elinipa Sonda, alisema kuwa ametaarifiwa na mtoto wake, Adam Yusuph ambaye yupo Ukraine, kuwa walilala nje ya bweni kwa muda wa wiki mbili kabla ya kwenda ubalozini kuomba msaada baada ya kutishiwa kunyang’anywa hati zao za kusafiria.
 
Mh Admin ...sasa we have about 3 threads zinazoongelea hii ishu...can we join them....kuna hii, ile ya interview ya mkjj na Mh Presidaa na hiyo nyingine.
Any details za hiyo account number?
 
Hivi ni lini wasomi wa Tanzania watathaminiwa? Kwanza, wanapata elimu kwa shida na taabu.Pili, wakimaliza masomo yao wanahangaika kupata kazi.Tatu,wakipata kazi mshahara ni kama mkia wa mbuzi.Mambo haya ni mpaka lini wajemeni?
 
mwanakijiji hongera sana.
wana jf pia hongera wote. sasa tunangoja details
za hiyo account. tafadhali wasisahau kutoa na swift code
ya benki
 
Tunawashukuru Wote Waliosaidia Kwa Hatua Moja Au Nyengine Kufanikisha Suala Hili, Kwa Mchango Mdogo Au Mkubwa, Na Nnawaambia Kubwa Lijaalo. Wazee Wetu Walivyotuusia
 
Mama Lao ni kweli your message was delivered,na pia imekuwa implemented well.

MWKJJ,hujampigia tena msola?
 
mpaka kielewe, atanikatia tena simu na sina hamu ya kujidhalilisha hivyo... jamani hizi hongera hasa za nini? Watu mpeane hongera baada ya vijana kurudi shuleni na serikali kubadili uamuzi wake...
 
I was wondering the same thing too......congrats for what if the problem has not been resolved?

Ingekuwa wameanzisha harambee na kuchangisha fedha za kuwalipia hao vijana then ingekuwa sawa kupeana hongera and pat each other on the back. Sasa hivi wametoa tamko tu kwa hiyo mapambano bado yanaendelea hadi kieleweke......
 
ni rahisi kupongezana kwa kauli nzuri kuliko kwa vitendo vizuri. Habari ambazo zinatiririka sasa hivi ni kuwa afisa mmoja (ngazi za juu) amezungumza na kusema serikali inawataka vijana hao "kurejea chuoni mara moja, wale wenye uwezo wa kurudi nyumbani warudi, na wale wasio na uwezo waombe watu wawasaidie nauli ya kurudi"..... !!! habari zaidi baadaye..
 
Jamani still michango si bado inahitajika maanake hapa itakua rahisi kwa watu waliokua na mpango wa kuwasaidia hawa vijana wakakaa tena kando.Tafadhali ka tunajua kutoa hongera namna hii basi tuzidi kuchangia hawa vijana.
Mkjj!!
Kuwataka waombe misaada kwa watu wenye uwezo wawasaidie kurudi nyumbani?! Hili bado ni kosa kubwa na aibu nyingine serikali inajitia.Plz mkjj usimpigie tena,tutampigia through petition!Kama ataweza kuikata ile nayo basi tutamwona,wakala mkubwa wa Shetani!
 
MKJJ

Mimi naona zifanyike juhudi za dhati kupitia jumuiya za Watanzania waliopo USA, UK, JP, Scandnavia etc kufanya utaratibu wa kuchangia mfuko wa kuwasaidia vijana hawa. Hilo ni wazo langu, naomba ulifikirie...ukihitaji contacts za viongozi wa Jumuiya ya waTz UK nijulishe.
 
Back
Top Bottom