Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Mzee wa kijiji mimi nipo njia panda, Nadhani watanzania wote jana wamemsikia Mh. Raisi kuhusu hao wanafunzi wa Ukraine..... Kwa mdomo wake mwenyewe mbele ya runinga zetu amesema ya kwamba Wanafunzi hao walijipeleka wenyewe na wala serikali haihusiki kabisa na kupeleka wanafunzi huko (Hao 26) na serikari haiwezi kuwalipia wanafunzi wote ada kwa sababu kumsomesha mwanafunzi mmoja nje ya nchi ni sawa na kusomesha wanafunzi nane hapa nchini...... Swali kwako MWANAKIJIJI je hii hoja ya kwamba serikali imewatelekeza hao wanafunzi wewe umeipata wapi????????? Maana wengi tupo njia panda.

Hivi anachojua yeye kuwasomesha watoto wa walalahoi tena ukraine ndiyo ghali na ni sawa na kusomesha wanafunzi nane nchini je kumsomesha Ridhwan Uingereza na kumuweka si hosteli bali kwenye apartment yenye hadhi ni sawa na kuwasomesha wanafunzi wangapi Tanzania au Ukaraine.?Nina uhakika Fedha inayotumika kumsomesha Ridhwan Uingereza ingeweza kuwasomesha hao vijana wote wanaosoma ukraine.Hivi waandishi walikuwa wapi kushindwa kumuuliza hili?
 
KNKCU hata mimi naungana na wewe? Who is telling the truth?? Mr President au wanafunzi wa Ukraine?? Naomba JF mwenye evidence afanye scanning tuone hiyo ruhusa ilitolewa na nani....na bado mnasema eti "watu wana destroy evidence" .
Let us be serious na tusiwe culprit wa media hype....
Kama Serikali inakupa ruhusa ukasome halafu inakataa kukuhudumia na una vithibitisho...wana hoja ya kujibu. Naona kinachoendelea sasa ni kuzungushana tu. Hamna anayetaka kutoa evidence.
Nimemwelewa Mh Raisi..if these madai siyo genuine na serikali ika bow down then mchezo huu utaendelea...
 
Hawa Vijana wanasema kweli na ni kweli walijilipia nauli ya kwenda chini ya makubaliano ya kupatiwa mikopo kama wanafunzi wengine waliomba mikopo.Mh. Rais Ameupoteza umma anaposema kuwasomesha watu nje ni ghali inawezekana ni kweli kwa Nchi za Magharib lakini kwa nchi zilizokuwa mungano wa kisovieti ikiwemo ukraine si ghali kuliko Tanzania.Pili alichosahau mbona yeye wa kwake wa kumzaa anasoma nje tena kwa fedha ya serikali tena ni ghali kuliko Ukraine na gharama yake yeye mmoja tu inaweza ikasomesha wanfunzi wote Ishirini na tisa kwa gharama za Ukraine.
 
Do you have evidence??????????
Jamani lets be realistic au tunasikiliza tu maneno yao? Kama kuna evidence SERIKALI INA HOJA YA KUJIBU. Please provide the evidence barua ya serikali...etc
Na kama there is such evidence nitawashangaa sana wanasheria wetu "wa haki za binadamu/utawala bora"mbona wako kimya???
To me hii issue inakuwa kichekesho...kila mtu anasema lakini hakuna anayesema zaidi ya mwenzake. Wanasema the same thing for more than 4 wks. HAKUNA JIPYA!
Wale waandishi ndio usiseme....walikuwa wakijua watakutana na Mh kwanini hawakuandaa evidence...yule mwandishi hakuwa najipya zaidi ya tunachokijua. Angeweza hata kuwa na copy ya barua ya serikali kwa hao wanafunzi...
In short I find some of our journalists "very shallow".
KNCU Hayo unayoyaita "makubaliano" yalikuwa verbally au kwa maandishi???
 
Do you have evidence??????????
Jamani lets be realistic au tunasikiliza tu maneno yao? Kama kuna evidence SERIKALI INA HOJA YA KUJIBU. Please provide the evidence barua ya serikali...etc

EVIDENCE GANI TENA?
NA VIELELEZO VILIWEKWA HAPA NA MWANAKIJIJI NA SHULE ILIWAPOKE IKIJUA SERIKALI INALIPA.TAFADHALI REJEE NYUMA YA HII MAADA UTAVIONA
 
Hivi anachojua yeye kuwasomesha watoto wa walalahoi tena ukraine ndiyo ghali na ni sawa na kusomesha wanafunzi nane nchini je kumsomesha Ridhwan Uingereza na kumuweka si hosteli bali kwenye apartment yenye hadhi ni sawa na kuwasomesha wanafunzi wangapi Tanzania au Ukaraine.?Nina uhakika Fedha inayotumika kumsomesha Ridhwan Uingereza ingeweza kuwasomesha hao vijana wote wanaosoma ukraine.Hivi waandishi walikuwa wapi kushindwa kumuuliza hili?

Tofauti iliyopo ni kwamba wale ni watoto wa walalahoi na Ridhwan ni Mototo wa kumzaa yeye...... kuhusu waandishi kumuuliza maswali kwanza ni waoga wa kuuliza maswali....... pili huyu ambaye alibahatika kuuliza kuhusu hilo swali la hao wanafunzi (Philip wa clouds fm) hakupewa nafasi tena labda yeye angepewa angeuliza maana ni yeye pekee ndio aliweza kuonyesha ujasili na kuuliza hilo swali ambalo watu wamelifumbia macho.
 
Do you have evidence??????????
Jamani lets be realistic au tunasikiliza tu maneno yao? Kama kuna evidence SERIKALI INA HOJA YA KUJIBU. Please provide the evidence barua ya serikali...etc
Na kama there is such evidence nitawashangaa sana wanasheria wetu "wa haki za binadamu/utawala bora"mbona wako kimya???
To me hii issue inakuwa kichekesho...kila mtu anasema lakini hakuna anayesema zaidi ya mwenzake. Wanasema the same thing for more than 4 wks. HAKUNA JIPYA!
Wale waandishi ndio usiseme....walikuwa wakijua watakutana na Mh kwanini hawakuandaa evidence...yule mwandishi hakuwa najipya zaidi ya tunachokijua. Angeweza hata kuwa na copy ya barua ya serikali kwa hao wanafunzi...
In short I find some of our journalists "very shallow".

Aliyewapeleka hao wanafunzi huko Ukraine anajulikana. Na jibu sahihi kabisa analo JJ Mnyika hapa: http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=38838#post38838. Kama Chadema walibackoff kwa kuwa waliambiwa wakati huo halikutakiwa kuwa la kisiasa, sasa hivi limeshakuwa la kisiasa zaidi kwa hiyo ushahidi uliopelekwa huko na huyo "Dr." utumike kuwanusuru hao wanafunzi, vinginevyo tutaendelea kubwabwaja tu hapa bila kufikia suluhu.
 
....To me all these are stories...huyu kasema hiv huyu kile....huyu anamjua agent. I do not see any evidence...Mrema claimed to have some na akaiambia serikali itoe evidence kwamba iliwakatalia hawa wanafunzi kwenda huko...mpaka leo hakuna na Mrema naye hajatoa za kwake....So what are we supposed to believe????
Kuna mtu yeyote anayeweza
1.Ku scan copy ya barua waliyopewa wanafunzi hawa kama sehemu ya kuhakikishiwa scholarship...kwamba tangulieni tutaleta pesa??
2. Au barua ya elimu ya juu ya kuwa offer scholarship/nafasi ya kusoma nje.

Short of that....tutasema tu na yataishia hapa......Ingekuwa vizuri zaidi tukawa na uhakika kwamba we are on the right track...
In short let us imagine if we were to take the govt to court tutaonyesha nini?
 
Na Alphan Mlacha
Tanlet:Suala la wanafunzi Ukraine linanuka rushwa
SAKATA la wanafunzi wa Tanzania waliokwama Ukraine, limeingia katika sura mpya baada ya Shirika la Elimu ya Sheria Tanzania (Tanlet), kudai kuwa limebaini kuwepo kwa harufu ya rushwa katika suala hilo.

Shirika hilo limesema pia limebaini kuwa wanafunzi hao ambao kwa sasa wamejisalimisha katika ubalozi wa Uingereza nchini Ukraine, wamekuwa waathirika kutokana na visasi na kukomoana kwa watu waliohusika katika taratibu zote za kuwapatia mikopo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Dk Sengondo Mvungi, alisema shirika hilo limepata habari kuwa kuna wanafunzi watatu kati ya 29 waliokwama Ukraine, wamepelekewa mikopo yao kinyemela na kuwaacha wengine bila ya msaada wowote.

Alihoji vigezo vilivyotumika kuwapatia mikopo wanafunzi hao na kuwaacha wengine 26. "Tunaitaka Serikali itoe tamko sahihi ni vigezo gani vilivyotumika kuwapatia mikopo wanafunzi hao watatu na kwanini wengine 26 wamenyimwa? Ili tuone kama haki kweli imetendeka".

"Mtaribu wa wanafunzi hao wa Ukraine, Dk Nurdin Jella, ametueleza kulikuwa na ukiritimba mwingi na uonevu katika kuwateua wanafunzi watakaopewa mikopo kusoma Ukraine ikilinganishwa na nchi nyingine.

Swali tunalojiuliza ni kama kuna rushwa katika uteuzi huo kwa maana ya maafisa kujipatia ‘kitu kidogo' ndipo waweze kuwateua kupata mikopo" alihoji Dk Mvungi.

Aliitaka Taasisi ya Kuzuia Rushwa nchini (Takuru), kufuatilia kwa makini nafasi za wanafunzi kwenda kusoma nje kama zinatoka kwa haki au ni watoto wa wakubwa tu ndio wanaokwenda kusoma nje.

Kwa upande mwingine, shirika hilo limepinga wazo la Serikali la kuwataka wanafunzi hao waliokwama Ukraine kurudi kuja kusoma nchini na limeonya kuwa hatua hiyo inaweza kuwasababishia matatizo makubwa wanafunzi hao ikiwa ni pamoja na kufungwa jela.

Limetahadharisha kuwa kuwatumia tiketi za ndege wanafunzi hao ili warudi nchini bila ya kwanza kuwalipia gharama za masomo ya mwaka mzima waliosoma nchini humo, kutasababisha wafunguliwe mashtaka na hatima yao itakuwa ni kuishia jela huko ughaibuni.

Dk Mvungi, alisema wanafunzi hao walienda Ukraine kujitafutia elimu na walikwisha fadhiliwa kwenye vyuo wanavyosoma hivyo ni wajibu wa serikali kuwawezesha waendelee na masomo yao badala ya kuendeleza malumbano na kuwaamuru warejee nchini bila ya kwanza kupata elimu iliyowapeleka huko kama walivyoomba.

"Serikali inadai wanafunzi walivunja taratibu kwenda huko Ukraine, tunataka kujua hizo taratibu zilizovunjwa ni zipi, sisi tunachoona hapa ni kiburi katika uongozi, bado tunayo kasumba kuwa mkubwa hakosei na mdogo kumkosoa mkubwa ni kashfa na kasumba hii isipoondolewa taifa litakwama" alisema Dk Mvungi.

http://mwananchi.co.tz/habari/habari7.asp
 
Bila ya shaka inawezekana wewe kama watanzania wengine wengi, umeshindwa kuelewa ni nani anasema kweli kati ya vijana hawa 29 na serikali. Kutokana na mazoea yetu ni vigumu kwa watu kuwaamini watu wa kawaida na ni rahisi kuamini viongozi wa serikali. Mara nyingi tumezoea kuwa kiongozi akisema kitu basi tunachukulia (assume) kuwa ni cha kweli. Inakuwa rahisi zaidi kuamini serikali hasa kama anayetoa kauli ya uamuzi ni Rais, Waziri Mkuu au Waziri fulani. Hivi sasa kuna watanzania ambao hawaelewi kama serikali imewetelekeza vijana hawa au vijana wamejitakia wao wenyewe. Binafsi najikuta napigana vita ya Daudi na Goliathi kwani nimebahatika kupata habari toka pande zote nne, wanafunzi, serikali, vyuo, na wazazi. Na pia nimepata habari toka wa mawakala wa vijana hawa wa Tanzania na kule Ukraine.

Habari hizi siyo kazi kuzipata zinahitaji muda tu na mtu kujituma. Inasikitisha kuwa siyo Rais, Waziri au Mbunge aliyelipa uzito unaostahili kiasi cha kuamua kutafuta ukweliwake na kufuatilia bila kusoma magazetini. Ninapoendelea kuwaombea ufadhili vijana hawa, nikijua utata uliojaa miongoni mwa watu najikuta tena nasukumwa kujaribu kulieleza jambo hili kwa kina na hasa kwa wasikilizaji na wale ambao mko kwenye mailing list yangu. Niyaweke mambo yafuatayo wazi na kutoa utata wowote.

Je vijana hawa walipatiwa mikopo ya kwenda kusoma Ukraine?
a. Hakuna barua iliyotumwa kuwaambia vijana wamepatiwa mikopo ya bodi ya elimu kwenda kusoma Ukraine. Hata hivyo, majina ya waliopata mikopo 2005/2006 kwenda kusoma Ukraine (wakiwemo vijana 29) yalikuwepo kwenye website ya bodi hadi yalipoondolewa hivi karibuni. Majina hayo yalipotangazwa kwenye batch 6, 7, 8 yaliorodhesha kiasi cha mikopo walichopewa na wapi walikuwa wanaenda kusoma. Orodha ya walioshinda mikopo hiyo ipo bodi na wizarani, hivyo serikali wanayo. Vijana hawa walipewa mikopo na hilo halina mjadala.

Mbona serikali imesema vijana walijienda huko Ukraine wao wenyewe kivyao vyao?
b. Serikali inazungumzia suala la "wanafunzi kuondoka" na hata mara moja haijazungumzia kama walipatiwa mikopo au la. Hoja ya wanafunzi ni kuwa walishakubaliwa mikopo (angalia hiyo "a" hapo juu) kwenda kusoma. Kama walikubaliwa mikopo tayari na fedha zilikuwepo, na vijana hao hawakutumia mikopo hiyo ya 2005-2006 pesa hizo zilienda wapi na zilitumiwa na nani? Sasa ni kweli kuwa vijana hawa waliondoka "wenyewe" kwa maana ya kuwa walinunua tiketi wao wenyewe baada ya kuhakikishiwa kuwa mikopo yao (waliyokwisha kukubaliwa) iko njiani na hivyo wasiendelee kuchelewa (walikuwa wameshachelewa mara moja)

Je vyuo vikuu viliwatambua vijana hawa na ya kuwa walidhaminiwa na bodi hadi vikawapa nafasi?
c. Tunafahamu na ushahidi niliweka hapa http://www.jambophotos.com barua toka Chuo Kikuu cha Kharkov waliandikia bodi na wizara kuwahakikishia kuwa kutokana na vijana kucheleweshwa kuja chuoni mwaka huo, nafasi zao zitashikiliwa hadi Septemba mwaka jana (kwa maana hawahitaji kutafuta nafasi upya). Barua toka vyuo vikuu ilitumwa Februali mwaka 2006. Katikati ya mwaka jana bodi ikabadlisha vigezo na utaratibu wa utoaji mikopo (kama walivyofanya tena mwaka huu). Vijana wakaenda kwenye bodi na kuulizia kama mabadiliko hayo yataathiri safari yao. Wakahakikishiwa kuwa mabadiliko ya 2006 hayakuwahusu wao (ingeshangaza kama yangewahusu wakati wao walishakubaliwa mikopo. Huwezi kutunga sheria itakayomuadhibu mtu kwa kwa kosa ambalo kabla ya sheria hiyo halikuwa kosa). Wakahakikishiwa na Bw. Mbegu na wenzake kwa mdomo kuwa mikopo yao haina tatizo wao wakipata tiketi waondoke. Wanafunzi 41 kati ya 65 waliondoka Tanzania kwenda kwenye masomo Ukraine. Barua toka Kharkov ipo Wizarani na kwenye Bodi.

Sasa vijana hawa 41 waliweza vipi kupata pasipoti bila kuonesha wanaenda wapi na kwanini? Kama walikuwa wanaenda vyuoni si lazima wangekuwa na barua za mdhamini?
d. Kabla ya kuweza kuondoka vijana walitakiwa kupata pasi za kusafiria. Huwezi kupata pasipoti Tanzania hadi uoneshe ni wapi unakwenda. Vijana hawa katika kuomba pasi zao vijana waliandikiwa barua za kukubaliwa vyuoni na bodi kuonesha ndio wadhamini. Barua hizi ziko (bado ziko???) uhamiaji na ndiyo zilizowezesha vijana kupatiwa pasi. Serikali inajua hilo na wanalojibu.

Vipi kuhusu zile Visa?
e. Ukraine haina ubalozi Tanzania na ubalozi unaotumika ni ule wa Nairobi. Pasi za wanafunzi zilikusanywa na kupitishwa ubalozi wa Tanzania Kenya kwenda kwa ubalozi wa Ukraine ili zigongewe Visa. Huwezi kupata Visa hadi uoneshe wapi unakwenda na udhamini wako ni upi. Ubalozi wetu na ule wa Ukraine wote walijua wazi kutokana na vielelezo vilivyoambatanishwa mdhamini wa vijana ni bodi, vinginevyo serikali ieleze ilikuwaje Ubalozi wetu kupitisha pasipoti zaidi ya 40 kwenda kwa ubalozi wa Ukraine bila ya wao kutambua hawa vijana wote ni kina nani, wanaenda wapi? Serikali inajua hili na wanalojibu.

Mbona tuliambiwa wanafunzi 17 walikubali maelekezo ya serikai na "wakaamua" kusoma nyumbani na mikopo yao ikahamishiwa katika vyuo vya nyumbani?
d. Kutokana na (c) hapo juu kati ya wanafunzi wote 29 , 2 walitangulia (ambao sasa wanalipiwa na serikali) wale 27 wengine walienda na ndege moja na kwa taratibu za Chuo cha Kharkov ni lazima uwe na tiketi inayoonesha kurudi pia vinginevyo hawakuruhusu kuingia Return Ticket a Must. Hivyo hao 27 waliweza kuingia na kupokelewa vyuoni ikieleweka wazi kuwa bodi ya mikopo ndio wadhamini. Kumbuka kuwa hawa sio wanafunzi pekee wa kitanzania vyuoni hapo na mpango wa malipo ya shule haukuwa tofauti na wa wanafunzi waliotangulia. Wanafunzi 12 kati ya wale 17 waliweza kuondoka lakini walirudishwa kule kule Kiev baada ya tiketi zao kutoonesha "kurudi". Balozi Chokala alitumia ushawishi wote kuwasaidia ilishindikana. Hawa walirudi Tanzania na mikopo yao ikahamishiwa Tanzania na wanasoma kwenye vyuo vya Tanzania pamoja na wale wenzao 5. Hawa ndio 17 aliowazungumzia Gesimba kama na wao wangefanikiwa kuingia tungekuwa tunazungumzia vijana 41 waliokwama Ukraine!! Serikali inafahamu hilo na inajua hilo, na wanalo jibu.

e. Kutokana na (d) hapo juu hawa wanafunzi 17 waliporudi Tanzania hawakuomba mikopo upya kwani walishakubaliwa mwaka 2005-2006 (wakati ule ule na wale 29) na wenyewe walianza masomo hivyo hivyo kwa kuchelewa. Majina yao na vyuo vyao ninayo na nimeshayaweka hapa hadharani. Kama serikali iliweza kutumia mikopo ya 2005/2006 kuwasomesha vijana hawa hapo nyumbani bila kuhitaji waombe tena mikopo, iweje wale waliokwishaondoka wakataliwe na kutakiwa kuomba tena mikopo? Wale walioko Ukraine 3 walishaanza kupokea mikopo yao licha kuondoka wakati ule ule, kwa makubaliano yale yale na ahadi ileile na wale 26, majina yapo na nimeyaweka hadharani. Serikali ilitumia vigezo gani kuwalipia hawa 3 na kuwaacha hawa 26? Serikali inafahamu na inalojibu.

f. Serikali imedai kuwa "waliwashauri" vijana hawa wasiende huko kwa vile haina pesa (kumbuka walishakubaliwa mikopo-pesa zilikuwepo!). Hakuna wakati wowote serikali (wizara na bodi) iliwaandikia vijana au familia zao kabla ya kuondoka na kuwataka wasiondoke au kuwaambia wakiondoka basi hilo lwao. Hakuna barua, hakuna tangazo, hakuna taarifa kwa vyombo vya habari wala nini! Kama waliwaambia kwa mdomo tu bila kuwaandikia tutaamini vipi kuwa hawakuwambia kwa mdomo watangulie? Kumbuka serikali imesema "haiwatambui" baada ya vijana kufika na kuanza masomo Ukraine na baada ya mabadiliko ya 2006. Kabla ya hapo bodi wamekutana nao wamewasaidia kupata pasi na visa, na wakawahakikishia kuwa mabadiliko ya 2006 hayawahusu.

Mbona Rais amesema serikali haisomeshi wanafunzi tena nje kwani ni ghali na kuwasomesha huko ni sawa na kusomesha wanafunzi watatu nyumbani?

g. Kuhusu suala la serikali kuwasomesha wanafunzi nje, hili nalo ni kichekesho. Kama kweli serikali haina pesa za kuwasomesha watu, mbona hawajawarudisha wanafunzi wote wa kitanzania ambao wanasoma kwenye vyuo vya nje? Hapo Ukraine kuna wanafunzi wengine zaidi ya 80 wanaolipiwa fedha na serikali na hivyo ninavyozungumza wamepokea fedha zao siku ya jumanne na jumatano kupitia ofisa wa Ubalozi wetu Moskow Bw. Francis. Kama kweli serikali haitaki kusomesha tena nawafunzi nje kwanini wanafunzi hawa wamekubaliwa mikopo kusoma China. Vijana wa Ukraine mikopo yao ilikuwa ni ya dola 3000 kwa mwaka, linganisha na hawa wa wanaosoma China Mikopo ya Wanaosoma China. Vijana hawa walikubaliwa kiasi cha dola 3000 kwenye mikopo yao wakati wale wanaoenda kusoma Uchina wamekubaliwa mara 3 zaidi, lipi gumu? Wale wanaosoma China kwa mwaka huu unaoisha sasa walikubaliwa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia nane, 800,000.000/=! kwa mwaka. Vijana hawa 29 hawahitaji zaidi ya shilingi milioni 70 kwa mwaka!! Kama ni ghali hivyo kwanini wasisitishe mikopo yote ya nje na pale wanapowarudisha hawa 26 (wakifanikiwa) wawarudishe na wale wote wanaosoma US, UK, China, Urusi, India, Libya n.k!!

Kwanini serikali haiko tayari kukiri imekosea na kwa kutumia nguvu zao zote wanaendelea "kuwakana vijana hawa"?

Jibu siyo rahisi kiasi hicho lakini linalotarajiwa. Kwa maoni yangu, and I'll be very frank.

- Kwanza, Rais Kikwete hajaamua kutafuta ukweli bali yuko tayari kusikiliza wasaidizi wake ambao ndio watuhumiwa kwenye sakata hili. Rais anapoandika barua wizarani na kwenye bodi kuwataka wampe maelezo ya kuhusu vijana hawa, barua inamfikia Msolla, Kabaka, Katunzi, Gesimba, Mbegu, na Nyatega, hawa wote watoe jibu gani? Hawa hawana jinsi bali kukaza uzi ule ule yaani "mheshimiwa Rais vijana hawa tuliwaambia wasiondoke wakaondoka na sisi hatuna fedha za kuwasomesha". Kina Msolla na wenzake wanaficha na kutetea ajira zao!!

- Pili, viongozi wa bodi na wizara kama nilivyosema kule kwingine wameapa vijana hawa hawatawashinda, na wako tayari kusema na kufanya lolote lile kuhakikisha hawasomi Ukraine na hata wakirudi wasisome tena (kumbuka vigezo vya kupata mikopo vilibadilishwa pia).

- tatu Rais Kikwete licha ya kujua ukweli huu wote ambao ni rahisi kuupata ameamua kuwatetea wasaidizi wake kwani hayuko tayari kumwajibisha mtu yeyote anayeboronga au kuvuruga maisha ya wananchi. Utawala wa Kikwete kama iliyomtangulia ni rahisi kusema "tunathamini elimu" na wanapiga vita ufisadi lakini shoka likiwekwa kwenye mpini hawawezi kuukata mti! Rais Kikwete kama viongozi waliomtangulia hana nia, sababu, uwezo, na kusudi la kuhakikisha viongozi waliochini hawanyanyasi wananchi au kuwaonea. Pale wizarani kuna watu wamekaa kwenye "viti vyao vya enzi" kwa zaidi ya miaka kumi wakiendelea na biashara yao ya "elimu ya juu" huku wakiandika mikopo kwa wanafunzi hewa, huku mawakala wao walioko Urusi na Ukraine wakikata hizo fedha na kuzirudisha Tanzania. Ninapowaandikia hivi, kuna racket kubwa ya fedha za elimu ya juu inayowahusisha maafisa wa ngazi za juu wa wizara hiyo.

- Watu na waandishi kwa ujumla wamefikia mahali pa kuamini kuwa Rais wa Tanzania hadanganyi au hana uwezo a kudanganya, kuongopa au kulaghai. Watu wengi wanapomsikiliza Rais wanafikiri wanamsikiliza mfalme na hivyo neno lake ni amri, na matakwa yake ni sheria. Rais kasema "wameondoka wenyewe" so that settles it! bahati mbaya kwao, tupo watu kama sisi ambao tunaweza kunusu harufu ya uozo toka mbali.

Alichosema Rais hakina ukweli hata chembe na yeye na wasaidizi wake wanajua. Wametegemea kuwa kwa vile Rais kasema basi yote yatafikia mwisho. Rais aliposema watu hawali mapanki, tulitakiwa kunyamaza, aliposema silaha haramu hazipitishwi Tanzania tulitakiwa kunyamaza, aliposema tumwache Mkapa astaafu kwa amani, tumetakiwa kunyamaza, aliposema umeme utapatikana kwenye miezi miwili na ikapita tulitakiwa kunyamaza, aliposema ukame wetu ni mapenzi ya Mungu tulitakiwa kunyamaza, aliposema tutadai pesa zetu toka serikali ya Uingereza kwa kuachilia kampuni "yao" watutapeli, tulitakiwa kunyamaza, na sasa amesema "nimeambiwa wanafunzi waliondoka wenyewe na serikali haikuhusika" tunatakiwa kunyamaza!!!

Uamuzi ni wenu, lakini ningekuwa na uwezo na suala hili badala ya kususa wanafunzi na kukaza uzi ningechukua tahadhari.

a. Ningewasimamisha viongozi wa bodi na kuunda tume ya huru ya uchunguzi itakayosimamiwa na Jaji wa Mahakama ya Rufaa, ikiwa na wajumbe toka taasisi muhimu huru na isiyo na Mbunge au kiongozi yeyote wa kisiada ili kutafuta ukweli.

b. Wakati tume inafanya kazi, ningehakikisha deni la watoto hawa kwanza linashughulikiwa na wanaishi kwa amani bila hofu ya kupoteza nafasi zao au kufikishwa mahakamani.

c. Endapo inagundulika vijana "hawakuelewa" au walikosea kitu fulani, basi badala ya kuwarudisha tunahakikisha kosa kama hilo halitokea tena na wanaendelea na masomo baada ya kujaza fomu au chochote ambacho hawakukamilisha.

d. Endapo itaonekana kuna uzembe kwenye wizara na bodi wale wote wahusika wanafukuzwa kazi kudanganya na kuhataratisha maisha ya vijana wa kitanzania kama fundisho na wakati huo huo kuwaomba radhi vijana hawa na kuwaacha waendelee na masomo pasipo upungufu wowote ule.

e. Kuhakikisha suala kama hili halitokei tena.

Hata hivyo nina uhakika serikali haitabadili msimamo wake hata tukiweka kila kitu hadharani na nyaraka zote hadharani... wameshasema wao ni nani hata wabadili kauli zao? Rais kasema nani atamfanya abadilike..! Mfalme ameshaamuru nani atamhoji? Na watanzania tumeamua kukaa kimya isipokuwa sauti dhaifu za watu wachache. Ndugu zangu tuwasaidie vijana hawa kwenda shule. Michango yenu inahitajika. Tumebakiwa na very few options, tuliweza kuwashawishi shule kuwaombea muda hadi tarehe 10 ya mwezi huu. Sijui nini kitatokea. Lakini nitaisikitikia nchi yangu kwa kitendo hiki, na binafsi sitawasemehe, na nitahakikisha kuwa siku moja watalipa. Haiwezekani watu wachache watawale nchi kama wafalme au wana wa wafalme!
 
I am really curious to know kama kweli hawa wanafunzi waliaidiwa kusomeshwa na serikali na kuwa waende tu halafu pesa zitatumwa. We need concrete evidence to counteract the Government's stand especially after it has now been reinstated by the President himself. Mambo matatu yananitiza:

i) Ikitokea kwamba ni kweli serikali iliwapeleka hawa wanafunzi kwa udhamini wake halafu sasa inawakana, mimi naanza kujawa na woga wa kutisha kuhusu maadili ya serikali hii na hasa Rais mwenyewe maana sasa inaonekana serikali haioni tatizo kudanganya. Hapo tutakuwa tupo katika matatizo ya kutisha kuliko tunavyoweza kufikiria na kuandika hapa na hii lazima kila mtu mwenye akili lazima atishike. Tunajua viongozi wa siasa hudanganya, lakini sio kwa kiwango cha kutisha kama hiki. What is boggling my mind though is, kwa nini imekuwa vigumu sana kutoa ushahidi wa kuonesha kwamba serikali ipo wrong?

ii) Kama ikithibitika kwamba ni kweli hawa vijana walikataliwa udhamini na serikali na wao wakaamua tu kwenda kwa matakwa na njia zao, naogopa kusema kuwa tutakuwa tunaionea kuinyoshea serikali vidole. Kusema kweli serikali itakuwa haiwajibika na kukwama kuendelea kwa masomo kwa hawa vijana zaidi ya kuwasaidia kuwarudisha salama nyumbani. Tukumbuke tu kuwa wapo watanzania wengi ambao wapo nje ya nchi wakijisomesha kwa gharama zao. Tutakuwa tuna-set a very dangerous precedence kama watu watakuwa wanaenda kusoma nje kwa matakwa yao halafu wakikwama tunawanyoshea vidole serikali. What is boggling my mind on this one again is, iweje hawa vijana waende kusoma nje ya nchi kwa mapenzi yao kisha wakwame fee halafu waamue kuizushia serikali? Hii kweli inawezekana? Hivi imekuwaje hata wazazi wao wasitoe hizo barua za udhamini wanapoongea na waandishi wa habari pale Dar es salaam? Kama kweli hawa vijana wameizushia serikali, naogopa kwamba Taifa letu linaanza kuwa na watu wasio na woga, tena ujasiri wa kuzusha mambo makubwa namna hii?!

iii) Katika vyuo vingi duniani vyuo huwa vina kumbukumbu ya kuonesha pamoja na mambo mengine, wadhamini wa wanafunzi wote wanaosoma katika vyuo husika. Kumekuwa na ugumu gani kwenda kuhakiki udhamini wa wanafunzi hawa kule vyuoni kwao?

Kwa kuwa kumejitokeza utata wa namna hii na kwa kuwa muhula wa masomo unakaribia kwisha tayari kwa vyuo kufungwa, ninapendeza hatua mbili zichukuliwe:

a) hawa vijana walipiwe fees wanayodaiwa kwa sasa kupitia serikali ama michango ya hiari kama inavyoendelea.
a) Iundwe tume ya uchunguzi ili kutambua ukweli wa jambo hili. Ukweli ukipatikana utuweke huru. Kama serikali itapatikana na hatia maafisa wa serikali wachukuliwe hatua za kinidhamu na kisheria. Kama itathibitika kwamba hawa vijana hawakwenda Ukraine kwa udhamini wa serikali, basi wao na wazazi wao wawajibike kurudisha pesa ambazo watakuwa wamelipiwa katika (a).
 
KikweteShein_frontpic_102.jpg

Real Jk At His Best.

WHY TALK ABOUT BOGUS STUDENTS WHEN WE HAVE TAIFA STARS AND REAL MADRID TO THINK ABOUT.
 
Mzee shukrani sana for the explanations.
Now I understand!!
Ma journalist mnaosoma huku.......investigate facts...haya mmebandikiwa hapo....msilale
 
Mzee Mjj.
Mpaka sasa hivi hawa vijana wanahitaji fedha kiasi gani ili waweze kuendelea?
Kuna uwezekano wa kuwapatia wafadhili, ila wataka kujua in total watahitaji kiasi gani ili wasirudi majumbani, na je, ufadhili huo ni wa muda gani; yani, ni kwa mwaka huu tu au miaka miwili au mitatu ijayo?
 
hadi hivi sasa wanahitaji karibu shilingi milioni 40, ambazo zitalipa madeni yao yote na cha kufanya baada ya hapo kitafuatia.
 
kwa hesabu zangu za harakaharaka; hizo milioni 40 zinaweza kupatikana ikiwa:

-watu 200 wenye mapenzi mema watachanga laki mbili (200,000) kila mmoja
-watu 300 wenye mapenzi mema watachanga laki moja na thelathini na tatu tatu....(133,333.333) kila mmoja
-watu 400 wenye mapenzi mema watachanga laki moja(100,000) kila mmoja
-watu mia tano wenye mapenzi mema watachanga elfu themanini (80,000) kila mmoja
-watu mia sita wenye mapenzi mema watachanga elfu sitini na sita..(66,666.66) kila mmoja
watu mia saba wenye mapenzi mema wakichanga elfu hamsini na saba..(57,142.8571) kila mmoja
-watu mia nane wenye mapenzi mema wakichanga elfu hamsini (50,000) kila mmoja
-watu mia tisa wenye mapenzi mema wakichanga elfu arobaini na nne (44,444.444) kila mmoja
-watu elfu moja wenye mapenzi mema wakichanga elfu arobaini (40,000) kila mmoja.

Na, kama wanachama wa JF wote (1281 as of today) wakichanga shilingi za Kitanzania elfu thelathini na moja, mia mbili na ishirini na tano (31,225.605)tu kila mmoja!

Nimetoa mchanganuo huu ili kuonyesha kuwa tukipenda, tunaweza kuwanusuru hawa wenzetu wasome. Ni wakati muafaka wa-TZ tuache tabia ya kuona shida ya mwenzetu ni yake binafsi, na tuache pererere nyingi, maneno yawe machache vitendo viwe vingi!
sasa Jf imekomaa, hili suala Mwanakijiji amelivalia njuga, si lake, hao watoto sio wake, ameingia gharama mpaka kufikia hapa, na tuonyeshe kuwa tumekomaa; tufanye harambee ya hizo hela. Milioni 40 ni nyingi ukiziangalia hivyo, lakini ukilinganisha na watu tuliopo tunaoweza kuchangia hata senti hizo sio hela za kurudisha wanafunzi nyumbani
 
Mwendapole:
Wakati wa maneno umekwisha. Hili ni jambo linalowezekana kutekelezwa kabisa.
Ninapendekeza pia JF iwahusishe matajiri wetu pale nyumbani. Tupitishe kapu kila mahali na kwa kila mtu anayeweza kutoa 30,000/

Uongozi, usimamizi na utekelezaji wa jambo - tuujadili haraka.
 
Back
Top Bottom