- Thread starter
- #41
Kwa hiyo hii habari ni ya Kenya!
Ni habari ya JAMII AFRICA, imejitosheleza kichwa cha habari na maelezo ya kina yenye manufaa chanya kwa jamii pana Africa Mashariki na mamlaka husika, ili kutafuta mikakati ya kunusuru jamii .
Kwa hiyo hii habari ni ya Kenya!
A kettle calling a pot black; anyway washauri JF; by the way ukitaka upotee kabisa tegemea huyu ndugu googlemkuu tumia google keyboard(Gboard) inapatikana playstore, naona typing errors nyingi, zima autocorrect
Sisi tusio na ajira tutakula wapi?Ni vzuri,kwa mara ya kwanza serikali ya ccm inafanya jambo lenye tija
Haha sawa mkuuA kettle calling a pot black; anyway washauri JF; by the way ukitaka upotee kabisa tegemea huyu ndugu google
Hawajazuia kamari,wamezuia matangazo tuSisi tusio na ajira tutakula wapi?
NIMEKURUPUKASoma kwanza uelewe, haraka ya nini kupongeza CCM? CCM na mambo ya Kenya wapi na wapi wewe kumbe CCM inaongoza hadi Kenya
NimekurupukaNi huko Kenya
Acha kusoma heading na kukimbilia kuisifu CCM yako😂😀😃
Kweli aisee,kuna sisi akili kubwa huwa tunasoma heading na aya ya kwanza unajua uzi unazungumzia nin unashuka kucommentMteta mada umekosa ethics za kuleta Habari
@Mods ungezeeni neno Kenya kwenye Heading
Wamenikamata leoMkuu acha uvivu Soma mpaka mwisho
Wabongo wamejaa mazima😁Kuna watu watajua ni Tanzania, Kumbe ni Kenya
Na ndivyo inavyobidi dunia ya leo ya mambo mengi kusoma kila herufi ni kupoteza muda unachofanya ni heading kwa uhakika alafu huku chini unapitisha macho, unless ni kitu kinavutia ndio unasoma vizuri; ukifanya kazi ya kusoma neno kwa neno utakosa muda wa kufanya mengine... (Kwahio waleta uzi inabidi kuwaangalia walaji)Wamenikamata leo
Tatzo nyuz nying za humu hurudia rudia maneno kwahyo ukisoma aya ya kwanza unaelewa kila kitu ila leo nmechemka
Ni Kenya hiyo dogo!Ni vzuri,kwa mara ya kwanza serikali ya ccm inafanya jambo lenye tija
Wafute na simba na yanga uraibu umezidi.SERIKALI, kupitia Bodi ya Kudhibiti na Kusimamia Kamari (BCLB), imesitisha matangazo yote ya kamari katika majukwaa yote ya vyombo vya habari nchini kwa kipindi cha siku 30, kufuatia ongezeko la shughuli za kamari na uraibu unaoathiri jamii.
Katika taarifa iliyotolewa Jumanne, Aprili 29, Mwenyekiti wa BCLB, Dkt Jane Mwikali, alithibitisha kuwa marufuku hiyo itaanza kutekelezwa mara moja na itadumu kwa muda wa siku 30.
Kulingana na bodi hiyo, marufuku hiyo inawahusu waendeshaji wote wa kamari waliopewa leseni na shughuli zote za utangazaji wa kamari kupitia televisheni, redio, mitandao ya kijamii, magazeti, mabango ya barabarani, magari, SMS, kampeni kupitia barua pepe, arifa za simu na ushawishi kupita watu maarufu, na wanamitindo mtandaoni.
“Kutokana na hali hii, na kwa mujibu wa mamlaka yake kisheria Bodi ya Kudhibiti na Kusimamia Kamari (BCLB) inaagiza kusitishwa mara moja kwa matangazo yote ya kamari na shughuli zinazohusiana na kamari katika majukwaa yote ya vyombo vya habari kwa kipindi cha siku thelathini (30) kuanzia tarehe ya taarifa hii,” ilieleza taarifa hiyo.
Bodi hiyo ilieleza kuwa inahofia sana kuongezeka kwa matangazo ya kamari katika kipindi cha kuanzia saa kumi na moja asubuhi hadi saa nne usiku, hali inayowaweka watoto na watu walio hatarini katika hatari ya kuathiriwa na uraibu wa kamari.
Shughuli hizo ni pamoja na kubashiri, michezo ya kubahatisha, bahati nasibu, mashindano ya zawadi na shughuli zote za kuhamasisha zinazohusiana na biashara hiyo.
Katika kipindi hiki cha marufuku, waendeshaji na watoaji huduma za kamari watalazimika kuwasilisha mipango ya tathmini na utekelezaji wa hatua madhubuti za kuhakikisha kamari inachezwa kwa uwajibikaji, kwa mujibu wa masharti ya leseni yaliyotolewa na BCLB.
“Wakati wa marufuku hii, waendeshaji wote wa kamari wenye leseni wanapaswa kuhakikisha wanazingatia kikamilifu sheria na kanuni zote zinazohusu kamari na utangazaji wake nchini Kenya,” iliongeza.
Aidha, BCLB ilitangaza kuwa kikosi kazi cha mashirika mbalimbali kimeundwa, kikihusisha wizara ya Usalama wa Ndani, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Mamlaka ya Mawasiliano Kenya, Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru Kenya, Idara ya Upelelezi wa Jinai, Bodi ya Ukaguzi wa Filamu, Baraza la Vyombo vya Habari Kenya, Kituo cha Kuripoti Fedha na BCLB. Kikosi hicho kimepewa jukumu la kuunda sera na
Baraza la Vyombo vya Habari Kenya pia limetakiwa kukamilisha na kutekeleza mwongozo mpya wa kuhakikisha matangazo ya kamari yanadhibitiwa ipasavyo katika vyombo vya habari na wananchi kuripoti shughuli zozote haramu za kamari kwa BCLB au kituo cha polisi kilicho karibu.
Hakika kwa mara ya kwanza😀😀Ni vzuri,kwa mara ya kwanza serikali ya ccm inafanya jambo lenye tija
😀😀😀hata wao wanapima upepo kwanza si umesikia wanasitisha kwa muda wa siku 30 kwanza?Wako wapi wale MACHAWA waliokuwa wanasema Betting ni AJIRA?
Betting haiwezi kuwa AJIRA, labda kwa wafanyakazi wa betting companies.😀😀😀hata wao wanapima upepo kwanza si umesikia wanasitisha kwa muda wa siku 30 kwanza?