Serikali yazungumzia tishio la Serikali ya Marekani kusitisha misaada

Serikali yazungumzia tishio la Serikali ya Marekani kusitisha misaada

Ni jambo la heri na busara kubwa kumaliza matatizo yetu kwa haki na amani. Ni ujinga kutatua matatizo yetu kwa shinikizo la wengine,ni upumbavu kutegemea maamuzi ya wengine kutatua matatizo yetu au kutarajia maendeleo.
Tumalize wenyewe na tujiandae kusonga mbele wenyewe.Tunaojidanganya kuwategemea,tujiulize wao walisaidiwa au kushinikizwa na nani?
 
Nawasitishe tu hakuna jinsi, dhahabu tunazo, gesi ya kufa MTU, mlima kilimanjaro, mbuga za wanyama Bandar sasa mungu atupe nini sie watanganyika??? Naomba mungu wasitishe tuone km tutakufa

Panua akili zaidi ukipata jibu utajiona sufuri-a(0)
 
Serikali imezungumzia tishio la Serikali ya Marekani la kusitisha misaada kwa Serikali ya Tanzania kutokana na mgogoro wa kisiasa Zanzibar na kukamatwa kwa maofisa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu.

Ofisi ya Ikulu jana ilisema masharti yaliyotolewa na Serikali ya Marekani yanatekelezeka na yatamalizwa kabla ya kikao cha Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Milenia (MCC) kukaa Desemba, mwaka huu.

Wiki iliyopita, Serikali ya Marekani iliitaka Serikali ya Tanzania kumaliza haraka mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar, vinginevyo upo uwezekano wa kusitishwa msaada wa zaidi ya Dola za Marekani milioni 472 (Sh. bilioni 999.4), za awamu ya pili ya fedha za MCC la nchi hiyo.

Fedha hizo za MCC awamu ya pili ni kwa ajili ya kuiwezesha Tanzania kusambaza umeme na kuwaunganisha wananchi wengi katika Gridi ya Taifa na uimarishaji wa taasisi zinazohusika na na sekta ya nishati.
Mambo ambayo Serikali ya Marekani iliitaka Tanzania kumaliza haraka ni suala mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar pamoja na kupata ufafanuzi wa watuhumiwa waliokamatwa kwa makosa ya mtandaoni, wakati wa Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu.

Akizungumza na Nipashe, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alisema suala hilo haliisumbui serikali na ni tatizo dogo ambalo linatatuliwa.

Alisema serikali ina uhakika wa kumaliza masuala hayo kabla ya kikao hicho cha Bodi ya MCC kukaa ambao masuala hayo yatakuwa yameshatatuliwa na kupatiwa ufumbuzi.
Alisema Bodi ya MCC ilikaa kikao chake cha kwanza Septemba, mwaka huu na inatarajia kukaa tena kikao chake Desemba, mwaka huu.

Alisema serikali ina uhakika Bodi ya MCC ikikaa kikao cha Desemba, mwaka huu itapitisha pasipo na shaka yoyote.
Aliongeza kuwa suala la sheria ya makosa mtandaoni, kuna watu walikamatwa na watafikishwa mahakamani ambapo mahakama yenyewe ndiyo itakayotoa hukumu na kama wana makosa watahukumiwa na kama hawatakutwa na makosa basi wataachiwa huru.

Balozi Sefue alisema suala hilo ni la kisheria, watu wametuhumiwa na wamepelekwa mahakamani ambako itaamua.
Kuhusu mgogoro wa Zanzibar, Balozi Sefue alisema kuna vikao vinavyoendelea vya kupata muafaka na mgogoro huo nao utamalizwa kwa haraka zaidi.

Marekeni ilieleza kuwa mambo hayo iliyotaka ipatiwe ufumbuzi, yataiwezesha MCC kuipima Tanzania katika sifa za kupata fedha hizo.

CHANZO:
NIPASHE
 
Naomba kuuliza,huo msaada ni kama mkopo ambao tutahitaji kuulipa baadae??? maana bil 900 ni pesa ambayo TRA wanaweza kusanya ndan ya mwez mmoja. Mie nadhan marekan wanamtest magufuli kuona kama anaobey. Kila nchi dunian sasahv inajua Tanzania has a new strictly sherrif (JPM) ambae analeta mapinduz ya kinyonyaji toka kwa viongozi na baadhi ya wawekezaji....so naamin lazma wapime waone msimamo wake kwao. Hata hvyo, kusolve issue ya znz ni muhimu sana ASAP
 
Nawasitishe tu hakuna jinsi, dhahabu tunazo, gesi ya kufa MTU, mlima kilimanjaro, mbuga za wanyama Bandar sasa mungu atupe nini sie watanganyika??? Naomba mungu wasitishe tuone km tutakufa

wewe kweli ''hardheaded'' kwaiyo wewe mtazamo wako tuendelee kuwa na migogoro ambayo inaweza kuepukika?
 
Nawasitishe tu hakuna jinsi, dhahabu tunazo, gesi ya kufa MTU, mlima kilimanjaro, mbuga za wanyama Bandar sasa mungu atupe nini sie watanganyika??? Naomba mungu wasitishe tuone km tutakufa
Wakati unaomba misaada hiyo dhahabu mbuga havikuwepo? mtabana mtaachia tu
 
Mshindi atangazwe,tudai katiba yetu yenye maslahi mapana kwa taifa,tupilia mbali ile ya ccm changa la macho
 
Ifike mahala nchi za kiaafrika zijitegemee kwenye mambo yake, na ndy matatizo ya kutegemea wahisani kutuendeshea maisha yetu. inafika wakati watatuamrisha kuhusu mashoga. Hapo ndipo utapoona nchi za afrika kuwa na masoko ya pamoja ili kukabiliana na vitisho vya hawa nguruwe, na si masoko tu viko vingi. Gaddaf walimuwekea vikwazo mbona aliweza kuunyanyua uchumi wa nchi yake, walimua gadaf si kwasababu ya kuwasaidia wa Libya ila kwa manufaa yao wenyewe.WAAFRIKA TUAMKE, TUBADILIKE, TUJIONGEZE NA TUPENDE VYA KWETU NA TUNUNUE VYA KWETU
 
Kuna Thread ilianzishwa hapa wiki iiyopita kuhusu taarifa hii ya misaada wa MCC.

Kuna watu hapa ambao hawajui lolote linaloendelea katika Dunia hii wakaanza kutoa maneno mengi yasiyo na misingi yoyote na hata uelewa hayana. ya kwamba Tanzania inaweza kuishi bila msaada huo wa MCC, mara oooohhh Magufuli ameanza kukusanya pesa hivyo zitatosha kuendesha shughuli za Serikali!!!!!

bila shaka sasa mnabaki na aibu kwa taarifa hii toka IKULU. Au nayo mtaikataa??????

Jadili hoja kwa msingi wa hoja na siyo kuweka siasa kila kona hata pasipo stahili.
 
Nawasitishe tu hakuna jinsi, dhahabu tunazo, gesi ya kufa MTU, mlima kilimanjaro, mbuga za wanyama Bandar sasa mungu atupe nini sie watanganyika??? Naomba mungu wasitishe tuone km tutakufa

Hiyo pesa sio ishu hapo ni kitisho tu. Ishu ni kwamba Marekani inataka muafaka Zanzibar. Na muafaka ni mzee wa Sawa Sawa kupewa nchi.
 
Ifike mahala nchi za kiaafrika zijitegemee kwenye mambo yake, na ndy matatizo ya kutegemea wahisani kutuendeshea maisha yetu. inafika wakati watatuamrisha kuhusu mashoga. Hapo ndipo utapoona nchi za afrika kuwa na masoko ya pamoja ili kukabiliana na vitisho vya hawa nguruwe, na si masoko tu viko vingi. Gaddaf walimuwekea vikwazo mbona aliweza kuunyanyua uchumi wa nchi yake, walimua gadaf si kwasababu ya kuwasaidia wa Libya ila kwa manufaa yao wenyewe.WAAFRIKA TUAMKE, TUBADILIKE, TUJIONGEZE NA TUPENDE VYA KWETU NA TUNUNUE VYA KWETU

Suala siyo nchi za Kiafrika pekee. Unapozungumzia Marekani, jua unazungumzia giant. Inamkoromea yeyote, japo level ya kukoroma hutegemea na ushawishi wa nchi na nchi.
 
Nawasitishe tu hakuna jinsi, dhahabu tunazo, gesi ya kufa MTU, mlima kilimanjaro, mbuga za wanyama Bandar sasa mungu atupe nini sie watanganyika??? Naomba mungu wasitishe tuone km tutakufa

unawaza kwa kutumia nn? Ukute na wewe ulitolewa ada ukaenda shule ukatoka kapa bila kujua nn maana ya marekani??
 
Wasipomtangaza mshindi aliyeshinda kwa uhalali basi Marekani waendelee kushikia hizo pesa za msaada .ile masisiem waisome namba vizuri
 
matazizo ya Zanzibar yamalizwe mapema na kwa amani, kila upande uridhike, pasiwe na kutumia nguvu wala hila, Tanzania ni moja nasi tuwe wamoja,

Dawa ni kumpa ushindi aliyeshinda na suvinginevyo
 
Marekani ina mambo yake; wamemvunja mrusi na umoja wake, hapa hata wakiamua kumleta/kumwingiza mtu wamtakaye au atakayewapa maslahi wanafanya hivyo...
Angalia nchi zilizo na vita, akiingia mmarekani pale lazima atamleta mtu wake..Angalieni sana kauli za Marekani

Hapa kinachotakiwa ni kumpatia haki yake aliyeshinda ambaye ni seif
 
we nawe ,,kwani havikuwepo hivyo vitu toka mwanzo,,bado tunahitaji hizo fedha,,unafikiri rea na miradi ya maendeleo vijijini inafanywa na serikali,,hebu google upate uelewa,,tena zitafanya kazi nyingi maana za nyuma zilikua zinaliwa sana

Huyo unaye mjibu ni kati ya wasiyo jua nchi inajiendeshaje yeye kazi yake ni kupiga makofi na vigeregere na kuimba iyere iyera
 
Back
Top Bottom