Serikali yazungumzia tishio la Serikali ya Marekani kusitisha misaada

Serikali yazungumzia tishio la Serikali ya Marekani kusitisha misaada

Nashindwa. Kwa nini hili ni tatizo? Tangaza mshindi tu.
 
Unafikiri Rais wako Magufuli hajui kwamba tuna dhahabu, gesi na mlima Kilimanajaro ? Wewe unafikiri kwa nini kanywea pamoja na kulijua hilo ?Watu wanawawekea vikwazo Russia iliyo na nguvu za kijeshi, inauza silaha za kufa mtu, ina mafuta na gesi kibao, itakuwa sisi ambao hata bajeti yetu wenyewe hatujitoshelezi !?
Mkuu 👍
 
Marekani ndio wakuu wao kwaiyo najua sasa watafanya haraka kumaliza mgogoro uliopo ila tuwe macho sababu marekani sio Rafiki mwema siku zote yeye ni adui wa nchi zote duniani, yeye hulinda maslai yake tu.
 
Ifike mahala nchi za kiaafrika zijitegemee kwenye mambo yake, na ndy matatizo ya kutegemea wahisani kutuendeshea maisha yetu. inafika wakati watatuamrisha kuhusu mashoga. Hapo ndipo utapoona nchi za afrika kuwa na masoko ya pamoja ili kukabiliana na vitisho vya hawa nguruwe, na si masoko tu viko vingi. Gaddaf walimuwekea vikwazo mbona aliweza kuunyanyua uchumi wa nchi yake, walimua gadaf si kwasababu ya kuwasaidia wa Libya ila kwa manufaa yao wenyewe.WAAFRIKA TUAMKE, TUBADILIKE, TUJIONGEZE NA TUPENDE VYA KWETU NA TUNUNUE VYA KWETU

Haya maneno naona umeamua kuongea kujifurahisha
 
Balozi Sefue alikuwa anakula mshahara wa bure tokea ateuliwe. Sasa baada ya Dr Magufuli kuingia ikulu ndo ameanza kazi
 
Kwa majibu hayo nampongeza sana rais wetu Magufuli kujibu kistaarabu. Nilikua nahofia sana jinsi atakavyo handle foreign issues na policy, nikifikiri atakuwa ana kiburi na hatatumia diplomacy lakini kwa kweli kaonyesha mwanzo mzuri. God bless him.
Kuna watu humu jamvini sijui kwa kutokujua dunia ya sasa inaendaje au kwa ubishi tu wa kijinga au sijui niseme nini, hivi kuna nchi ya ulimwengu wa tatu ambayo haitegemei misaada? Hivi Mugabe na kiburi chake leo Zimbabwe iko wapi? Kama taifa kama China lenye uchumi mkubwa sana lakini inapotokea kuna tofauti za masuala ya kiuchumi au kiusalama na USA wanakaa meza moja na wanajadili? Hawa wachangia mada ujasiri wa kusema tuachane nao na misaada yao kisa Rais wa awamu ya tano kaanza vizuri? Kwa lipi? Muhimbili, bandari etc. Serikali yenyewe inajua zaidi ya mnavyofikiri ndio maana wameamua kukaa kikao ujadili na kufanya maamuzi ya busara tusikurupuke.
 
Naomba kuuliza,huo msaada ni kama mkopo ambao tutahitaji kuulipa baadae??? maana bil 900 ni pesa ambayo TRA wanaweza kusanya ndan ya mwez mmoja. Mie nadhan marekan wanamtest magufuli kuona kama anaobey. Kila nchi dunian sasahv inajua Tanzania has a new strictly sherrif (JPM) ambae analeta mapinduz ya kinyonyaji toka kwa viongozi na baadhi ya wawekezaji....so naamin lazma wapime waone msimamo wake kwao. Hata hvyo, kusolve issue ya znz ni muhimu sana ASAP

Hio ni awamu ya pili unasahau awamu ya mwanzo, huo msaada sio hela ya kuchezea, tuache siasa, mshindi zanzibar atangazwe
 
Hivi unajua maana ya neno Marekani au wale wakiamua kukubania utajuta mnaweza ambiwa mwisho kusafiri kenya, hamkawii kuambiwa dhahabu zenu hazina ubora mtaziangalia? Wana mikwara balaa.

Hahahaha!
 
... hapa ni kama vile wanaahidi kwamba Seif ataapishwa kabla ya kikao cha MCC cha December mwaka huu.
 
Nawasitishe tu hakuna jinsi, dhahabu tunazo, gesi ya kufa MTU, mlima kilimanjaro, mbuga za wanyama Bandar sasa mungu atupe nini sie watanganyika??? Naomba mungu wasitishe tuone km tutakufa
Kuntu👉💥💥
 
Back
Top Bottom