Serikali yazungumzia tishio la Serikali ya Marekani kusitisha misaada

Jee wakisema hawanunui dhahabu gesi na madini mengne na wakisema hawaji kwenye huo mlima mtafanyaje, yaani hayo co maneno ya kuongea bora uombe mgogoro umalizwe kwa amani tu
 
Wasitutishe. Hizo 1bn tutazipata hapa hapa rais anapotumbua majipu. Tukibanana wenyewe hatuhitaji pesa za wazungu hata kwenye miradi ya maendeleo. Ukwepaji kodi kwenye bandari, vat, kodi ya mapato, migodi, Maliasili na utalii, ubadhirifu serikalini na kwenye mashirika ya Umma vinatisha! Vithibitiwe. Mambo yetu ya ndani tutayamaLiza wenyewe.
 
Ukishindwa kujitawala, kutawaliwa ni haki hako ya msingi
 

Kwa hiyo wewe una akili na unajua sana kuliko huyu Kiongozi msemaji wa ofisi ya IKULU ambaye amenukuliwa akisema haya kuhusu MCC????

Acha kuwa VUVUZELA endapo kama huelewi maana ya MCC na misaada yake kaa utulie na usome hoja za wenye kuelewa umuhimu wake na maana yake.
 

Ifike mahali nchi za kiafrika zitangaze mshindi halali. kwani wamarekani ndio waliosema msiimtangaze mshindi halali? Hayo masoko ya pamoja tutayaweza wapi wakati tunataka kuendeleza hila? Hii sheria ya mtandaoni ilitungwa rasmi kuhakikisha watu hawatoi taarifa za hayo makontena 347 yaliyopotea. Wewe baki unalazimishia kujitenga kimataifa ili mtawale kimabavu.
 
Hamna shida yatamalizwa tu kwanza tuwashughulikie hawa mijizi
 
Jipu si lazima kuiba pesa na rasioimali za nchi, ni pamoja na kupora madaraka. We hukuchaguliwa na wananchi lakini unang'ang'ania kubaki ktika nadaraka , we ni jupu la kutumbua tu!!!! Yupo aliyejipa kazi ya kutumbua majipu, atalishughulikia.
 

Kweli mkuu bora tukubali tu kiungwana hawa jamaa no hatari sana Mara wanaingiza nchi katika orodha za nchi zinazohifadhi magaidi hawachelewi hawa
 

Hakuna haja ya vyama vingi kuwa anaeshida asipewe nchi
 
yatatuliwe si kwa mizengwe kwa amani Kila upande uridhike tusijiingize kwenye ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu Na pia suala la Zanzibar busara zitumike kuweka mambo sawa .
 
naipenda amani ya zanzibar ila tunakoelekea sidhani kama tutahitaji sana misaada ya watu weupe
 

Kwa majibu hayo nampongeza sana rais wetu Magufuli kujibu kistaarabu. Nilikua nahofia sana jinsi atakavyo handle foreign issues na policy, nikifikiri atakuwa ana kiburi na hatatumia diplomacy lakini kwa kweli kaonyesha mwanzo mzuri. God bless him.
 

Uelewe kwamba kiasi kikubwa cha makusanyo ya mapato yetu hutumika kuendesha serekali yaani matumizi. Miaka yote fedha za maendeleo zimetoka kwa wafadhili. Lakini kwenye mambo ya sera za nje kinachotazamwa si misaada tu. Tunahitaji kuwa na mahusiano mazuri kwa kua mbali na hayo kuna mambo mengine ya kiuchumi na masoko na kijamii ambapo Tanzania tunayahitaji na hatuwezi kamwe kuishi kama kisiwa.
 
Nchi imejaa kila takataka ya mali bado matamko yanatutisha!shity.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…