JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Kutakuwa na vyombo vya Serikali za Mitaa katika kila mkoa, wilaya, mji na kijiji, katika Jamhuri ya Muungano,
ambavyo vitakuwa vya aina na majina yatakayowekwa na sheria
iliyotungwa na Bunge au na Baraza la Wawakilishi.
(2) Bunge au Baraza la Wawakilishi, kadri itakavyokuwa, litatunga sheria itakayofafanua utaratibu wa kuanzisha vyombo vya Serikali za Mitaa; miundo na wajumbe wake, njia za mapato
na utaratibu wa utekelezaji wa shughuli za vyombo hivyo.
Ibara ya 146.-(1) inabainisha kuwa Madhumuni ya kuwapo Serikali ya Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchi.
Na vyombo vya Serikali za
Mitaa vitakuwa na haki na mamlaka ya kushiriki kuwashirikisha wananchi katika mipango na shughuli za utekelezaji wa maendeleo katika sehemu zao na nchini kote kwa jumla.
Ibara ndogo ya (2) inaeleza kuwa :- Chombo cha Serikali za Mitaa, kwa
kuzingatia masharti ya sheria iliyokianzisha, kitahusika na shughuli zifuatazo -
(a) Kutekeleza kazi za Serikali za Mitaa katika eneo
lake;
(b) Kuhakikisha utekelezaji wa sheria na ulinzi wa wananchi; na
(c) Kuimarisha demokrasi katika eneo lake na kuitumia demokrasia kuharakisha maendeleo ya wananchi.
Upvote
3