SoC03 Serikali za Mitaa Ziimarishwe Ili Kuharakisha Maendeleo ya Wananchi

SoC03 Serikali za Mitaa Ziimarishwe Ili Kuharakisha Maendeleo ya Wananchi

Stories of Change - 2023 Competition

Tukuza hospitality

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2022
Posts
321
Reaction score
691
ConstantineJ. Samali Mauki

Utangulizi
Serikali za mitaa ni chombo cha utawala wa umma, kilichopewa madaraka ya kuamua na kuendesha shughuli zake katika sehemu ndogo ya nchi au Taifa. Hizi ni halmashauri za wilaya, miji, manispaa na majiji ambazo zinasimamia shughuli za maendeleo za kata, vijiji na/au mitaa katika sekta mbalimbali kama elimu, afya, kilimo, maliasili, na kadhalika.

Kwa mujibu wa tovuti ya TAMISEMI, madhumuni ya kuwepo kwa Serikali za Mitaa ni kupeleka Madaraka kwa Wananchi ambapo chimbuko lake ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika Sura ya 8, Ibara ya 145 na 146. Upelekeaji wa madaraka kwa wananchi unapitia katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na ndiyo, maana Serikali za Mitaa na ushirikishwaji wa Wananchi katika mchakato wa maendeleo vimetambuliwa katika Katiba na Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. kwa mujibu wa tovuti hii, tangu mwaka 1961 hadi sasa Ofisi ya Rais –TAMISEMI imekuwa ni Wizara inayojitegemea, Wizara chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na kwenye Ofisi ya Rais kama ilivyo sasa. Uamuzi wa wapi inawekwa umekuwa ukifanyika ili kuimarisha utendaji wa Ofisi hii. Serikali iliendelea na mfumo wa Serikali za Mitaa uliorithiwa kutoka kwa Wakoloni na kuutumia kama nyenzo za kuleta maendeleo kwa misingi ya Kidemokrasia. Kutokana na changamoto mbalimbali zilizoukabili utendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa baada ya uhuru mwanzoni mwa miaka ya sabini, Serikali ilifuta Mamlaka hizi na kuanzisha mfumo wa Madaraka Mikoani.

Kilelezo Na. 1: Viongozi wa Serikali Katika Mkutano wa ALAT
Viongozi wa Halmashauri Kikaoni.png

Chanzo: Google: Serikali za Mitaa

Changamoto za Serikali za Mitaa

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi (Machi 17, 2021) Ingawa halmashauri za wilaya zilikuwa na majukumu mazito zaidi kuliko yale ya halmashauri za miji, sehemu kubwa ya ruzuku kutoka Serikali Kuu kwenda kwa Serikali za mitaa ilitolewa kwa halmashauri za miji. Kutokana na changamoto ya upungufu wa mapato, halmashauri nyingi zilishindwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Hali hiyo ndiyo iliyojitokeza kwa serikali nyingi za mitaa katika kipindi hiki cha mwaka 1962-1972.

Kwa mujibu wa tovuti ya TAMISEMI, kutokana na changamoto mbalimbali zilizoukabili utendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa baada ya uhuru mwanzoni mwa miaka ya sabini, Serikali ilifuta Mamlaka hizi na kuanzisha mfumo wa Madaraka Mikoani.

Kwa mujibu wa tovuti ya TAMISEMI, serikali hizi za mitaa zilirejeshwa tena kati ya mwaka 1978 na 1984.

Moja ya sababu za serikali za mitaa kushindwa kutekeleza majukumu yake ni upungufu wa vyanzo vya mapato, kutokana na serikali kuu kuhodhi vyanzo muhimu vya mapato.

Jitihada za Serikali Kuimarisha Serikali za Mitaa
Kwa mujibu wa tovuti ya TAMISEMI, serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali. Mojawapo ya hatua hizi ni kuanzishwa kwa Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa ulioanzishwa mwaka 1998 ambao ulilenga katika kupeleka madaraka kwa Wananchi Decentralization by Devolution (D by D).

Serikali za Mitaa Zinaweza Kuimarika Zaidi
Serikali hizi za mitaa zitaweza kuwa na nguvu na ufanisi kuliko ilivyo sasa, endapo zitapata mamlaka ya kukusanya na kutumia mapato ndani ya eneo lake.

Pia naamni, serikali hizi zikifanya kazi chini ya serikali za majimbo (yaani mikoa ya sasa) zitakuwa na ufanisi zaidi.

Kwa muda mrefu serikali kuu imekuwa ikihodhi vyanzo vyote muhimu vya mapato, na kuziacha halmashari husika na vyanzo hafifu, na kutegemea ruzuku zaidi kutekeleza majukumu yake.

Serikali kuu inapaswa kuziachia halmashari zake kukusanya mapato yake na kuyatumia huku zikilipa serikali kuu kiasi kitakachopangwa kwa kila makusanyo, tofauti na sasa ambapo zinatakiwa kuomba fedha kila zinapohitaji kutekeleza miradi yake, jambo ambalo linachelewesha maendeleo ya wananchi. Kwa mfano, barabara kutoka kijiji A kwenda kijiji B, ikiharibika au daraja likivunjika, halmashari husika inapaswa kuomba fedha serikali kuu, na kusubiri muda mrefu, huku wananchi wakitaabika. Endapo halmashari zingekuwa zina mapato yake ya kutosha, changamoto kama hiyo ya barabara ingeshughulikiwa mara moja, pengine ndani ya muda usiozidi wiki moja.

Mapendekezo
Serikali ianzishe serikali za majimbo, na kuzijengea uwezo wa kuboresha serikali za mitaa (Halmashauri za wilaya, miji, manispaa, na majiji).

Serikali izijengee uwezo serikali za mitaa, na kuziruhusu kukusanya kodi (mapato) na kutumia ili kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Hitimisho
Serikali za mitaa zipo karibu na wananchi, na zina fursa ya kuwahudumia kwa ufanisi zaidi; zinapaswa kupewa nguvu na kuaminiwa na serikali kuu. Serikali kuu inapaswa kubaki na mambo machache na ya kimkakati ya kitaifa na ya kimataifa.

Marejeo
Historia ya taasisi | PO-RALG

Mwananchi (Machi 17, 2921), Ijue Historia ya Serikali za Mitaa Tanzania
 
Upvote 6
Serikali za mitaa zipo karibu sana na wananchi, lakini hazijajengewa uwezo vya kutosha! NI kawaida kuona mjumbe wa serikali ya mtaa hajui watu wanaoishi mtaani kwake, mtu anaweza kuhamia katika mtaa wake akaishi miaka mitano a zaidi, na akahamia tena kwingine, bila kumwona mjumbe wake wa mtaa. Hili ni tatizo kubwa la kiuwajibikaji.
 
Serikali za mitaa zitaimarika zaidi, endapo serikali za majimbo zitaundwa.
 
Back
Top Bottom