Serikali zuieni chakula kuuzwa nje ya nchi, hali ni ngumu. Mbona mmeziba masikio?

Serikali zuieni chakula kuuzwa nje ya nchi, hali ni ngumu. Mbona mmeziba masikio?

Tajiri wa kinyankole

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
1,977
Reaction score
4,912
Ndugu zangu nimepita maeneo mbalimbali kwa mwaka huu tanzania hatuna chakula cha kutosha kwani kilo ya unga ni tsh 1300/=ukizingatia kipindi kama hiki cha wakati wa mavuno niritarajia itashuka kufikia tsh 900/= cha ajab imekuwa ndivyo sivyo, mchele kilo tsh 2100/= hapo ni mikoa ya kanda ya ziwa!

Maeneo mengi naona rwanda burundi na kenya wananunua chakula na kupeleka nchini mwao tunajuwa siyo dhambi lakini kwa wakati tulio nao hapakuwepo sababu kuruhusu chakula kuuzwa nje ya nchi, sukari; cement, nondo, vifaa vyote vya ujenzi kwa ujumla kwa sasa havishikiki sasa hivi bora liende / fedha inekuwa ngumu vijana wanashinda chini ya miti wakiwaza nakuwazua fursa imekuwa ngumu kupatikana, biashara kwa jasiriamali zimekuwa ngumu kwani kila siku nikulipa ushuru huku hakuna faida yoyote.

Aidha nachojiuliza hivi ni kweli serikali haioni yanayoendelea wakati huu haioni kelele zilizopo za malalamiko mengi kwa wananchi ya vitu kupanda bei?

Tanzania yetu imekuaje mbona kama tunazama shimoni.
 
Wanakula na kusaza, wamevimbiwa hivyo, wameweka pamba masikioni.
 
Kwani huyu anayetaka chakula kisiuzwe nje alikuwepo wakati wakulima wanavuja jasho?

Mimi nadhani mkulima ahurumiwe. Awe huru kuuza pale anapoona anapata bei nzuri.
 
Kuwa na akili ni bahati mleta mada hakubahatika....
 
Acha kutoa ushauri wa kijima wewe. Kwann wewe usilime chakula cha kulisha familia yako?

Yaani mkulima alime kwa hela yake halafu wewe kwa uvivu wako apangiwe wapi pa kuuza?

Mbona wewe mishahara wako unaoupata kwenye shughuli zako hatukupangii mahala pa kuutumia?

Mazao ndiyo mshahara wa mkulima, mwache autumie atakapo.
 
Hukuwepo wakati watu wanalima unataka kuja kuwapangia kwa kuuza....
 
Kwa kweli mleta mada mi sijajua ni utoto au utu uzima uliopitiliza yaan wakulima wanateseka na kupambana na hali ngumu na ghalama kubwa ya mbolea na madawa bila msaada halafu we unaleta ufahamu wako wa kwenye kijiko cha chai wasirusiwe kuuza chakula.

Wengine matusi na kudharauliwa huwa mnataka wenyewe.

Mvua wakati zinanyesha we hukuziona acha utoto basi tusije wakulima tukakwambia huna akili ukasema tumekutuna bure?
 
Walipokuwa wamezuia mliwatukana sana haohao serikali sasa wameruhusu mnataka wazuie tena?

Kila mtu atumie akili yake kutunza chakula anayetaka kuuza chote auze tu afe na njaa
 
panapotokea fursa ya Wakulima kunufaika na kazi za mikono yao mnaleta sera za ujamaa na uzalendo eti wazuiwe wasiuze nje ya nchi kwny bei nzuri ili sie Wavivu na maskini tupate chakula kwa bei chee

kikiwa kingi hadi bei kuwa ya chini sana hatukumbuki kuishauri serikali kuwafidia kwa hasara wanayopata

kwanza inakuaje Burundi wenye uchumi mbovu waweze kununua chakula kwa bei nzuri kuliko sisi wenye uchumi mzuri, amani, mshikamano n.k

Serikali ikikubali ushauri huu wa kunyanyasa Wakulima Bora Comrade Kinana anyofoe picha ya Jembe kwny Bendera ya Chama chetu aweke picha ya dula la madera
 
Ndugu zangu nimepita maeneo mbalimbali kwa mwaka huu tanzania hatuna chakula cha kutosha kwani kilo ya unga ni tsh 1300/=ukizingatia kipindi kama hiki cha wakati wa mavuno niritarajia itashuka kufikia tsh 900/= cha ajab imekuwa ndivyo sivyo, mchele kilo tsh 2100/= hapo ni mikoa ya kanda ya ziwa!

Maeneo mengi naona rwanda burundi na kenya wananunua chakula na kupeleka nchini mwao tunajuwa siyo dhambi lakini kwa wakati tulio nao hapakuwepo sababu kuruhusu chakula kuuzwa nje ya nchi, sukari; cement, nondo, vifaa vyote vya ujenzi kwa ujumla kwa sasa havishikiki sasa hivi bora liende / fedha inekuwa ngumu vijana wanashinda chini ya miti wakiwaza nakuwazua fursa imekuwa ngumu kupatikana, biashara kwa jasiriamali zimekuwa ngumu kwani kila siku nikulipa ushuru huku hakuna faida yoyote.

Aidha nachojiuliza hivi ni kweli serikali haioni yanayoendelea wakati huu haioni kelele zilizopo za malalamiko mengi kwa wananchi ya vitu kupanda bei?

Tanzania yetu imekuaje mbona kama tunazama shimoni.
View attachment 2215005
Acha Kila mtu auze anapotaka Chakula mnataka kuwapangia watu bei mbona bidhaa zingine mmeshindwa? Kila mtu apambane na Hali yake
 
Mkuu acha chakula kipande wakulima tumeteseka sana mbolea kutoka elfu 50 hadi laki moja na 40. Halafu bado unataka wauze bei ya chini tena unashauri masoko mazuri ya nje yafungwe je unataka wakulima wapate hasara kubwa ili msimu mpya wasilime kabisa chakula kisiwepo kabisa au vipi.
 
Wakulima nao wafaidike sasa

Unalalamika bei ya mahindi kwa nini hukulima?
 
Ndugu zangu nimepita maeneo mbalimbali kwa mwaka huu tanzania hatuna chakula cha kutosha
Chakula kipo cha kutosha. Sema chakula cha bure ndio hamna.

Serikali ina mazao ya kutosha kwenye maghala ya kuhifadhia chakula.

Iwapo njaa itatokea, wafanya biashara wataweza kununua mazao hayo na kuyaingiza sokoni.
 
Back
Top Bottom