Serikali zuieni chakula kuuzwa nje ya nchi, hali ni ngumu. Mbona mmeziba masikio?

Serikali zuieni chakula kuuzwa nje ya nchi, hali ni ngumu. Mbona mmeziba masikio?

Mbolea imepanda, gharama za kulima mpaka kuvuna ziko juu,
Unataka wapangiwe mahali pa kuuza,
Kama unaona kulima ni rahisi, kalime mpunga uje uuze kilo ya mchele 1,000/
 
Eeeh Mungu muumba wa mbingu na Ardhi hii hali iendelee hivihivi wakulima waneemeke wazidi kupiga hela mpaka wasaze watajirike mara mia. Kila siku nyinyi bana mneemeke hebu wacha wakulima wale neema
 
Ndugu zangu nimepita maeneo mbalimbali kwa mwaka huu tanzania hatuna chakula cha kutosha kwani kilo ya unga ni tsh 1300/=ukizingatia kipindi kama hiki cha wakati wa mavuno niritarajia itashuka kufikia tsh 900/= cha ajab imekuwa ndivyo sivyo...
Serikali ianzishe mashamba yake, mimi hapa shambani kwangu nimelima mahindi ya biashara na akiba ya kutosheleza mwaka huu
 
Mleta mada kwenye kilio Cha pembejeo uliwasaidia wakulima kulia
 
Kupitia Wizara ya Kilimo waziri lishauri baraza la mawaziri kufunga mipaka ya nchi hii.

Hali ya chakula sio nzuri maeneo mengi yame pata mvua chache na nyingi zimechelewa sana kwa msimu huu unaoishia 2021/2022.

Hivyo kupelekea wakulima wengi kutokulima kwa wakati na hata walio lima mazao mengi yaliungua hivyo kupelekea hali ya kupata mavuno kidogo ama kukosa mavuno.

Maeneo machache yaliyopata mavuno mazuri wafanyabishara wenye mitaji mikubwa wameanza kukusanya mahindi na mpunga kwa kasi sana..ili kuweka stoo na wengine wakisafirisha kwenda kuuza nje ya nchi.

Hii itapelekea muda si mrefu chakula kuadimika na kukosekana na kupeleka bei kuwa juu hata kwa kile kidogo kitakacho patikana.

Hivyo naomba serikali ichukuwe hatua za haraka sana kuzuia chakula kisitoke nje ya nchi ili kukabiliana na hatari inayokuja.

#MaendeleoHayanaChama
 
Tutalaza wajirani zetu na wafanyabiashara wetu njaa.
 
Kutokana na hali ilivyo ya Sasa. Serikali izuie chakula kisitoke nje hali mitaani ni mbaya mno. Chakula ndo kitu Cha msingi kabisa kwenye nchi.

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Ila suala chakula kwa kweli tusifanye mzaha!! Hali ni tete huko duniani!

Chakula kisitoke nje! India amezuia, Urusi amezuia, nk Tusipeleke chakula nje kwa kuvutiwa na bei maana tukikiuza tutakuja kukitafuta kwa bei kubwa zaidi wala hakitapatikana!
 
Modurator tafadhali kicha cha habari naomba urekebishe iwe zuieni chakula

Serekali izue chakula kuuzwa nje kwani wamemsaidia nani kulima? Mtembee na maVX kisha mje kutuzuia kuuza mazao yetu? Anayeona chakula kunapungua kwa sisi wakulima kuuza nje, aingie na yeye shambani ahakikishe njaa haiingii nchini.
 
Kwa sera hizi tutawashawishi vipi vijana warudi kwenye kilimo? Kama vipi serikali wanunue mazao kwa kupitia wakala wa mazao then wa-stoo ,

Nini faida ya kilimo kama wadau mnaleta mawazo ya kumkandamiza mkulima tuu?

Sijalima tena tangu nichome mtaji awamu ya tano .. ni sera za hivi hivi watu tukashindwa kuuza mahindi Nje ila mahindi ya malawi na Zambia yanaingia na soko la ndani lilikuwa la kidwanzi....
Aaaaah.......
 
Acha tuuze bei nzuri. Watu muna roho za kinyama kweli kweli.

Wakati wakulima wanalima wewe upo ofisini unafuta futa kiatu king'are afu leo kwenye kuuza unataka kuleta utahira wako.
 
Back
Top Bottom