Serious Note: Hivi wanawake wanatushindwa wapi ?nazungumzia usafi wa mazingira.

Serious Note: Hivi wanawake wanatushindwa wapi ?nazungumzia usafi wa mazingira.

Mimi ghetto langu limejaa vipisi vya sigara

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna msela wangu si ndo akajifanya uzungu! Kenda zake kununua ash tray na kuweka mezani! Bhana eh, ikawa ile tray kama sehemu ya wachoma mkaa na vile vipisi ndo kama magogo yenyewe yanasubiria kuingizwa kwenye tanuri! Vimejaa kibao!
 
Sifa ya mwanaume au gheto la kiume ni uchafu,
Ukiingia mpakaupige chafya mara tatu kwanza ndo unajua upo kwenye himaya nyingne.
ukilala kwake kesho unaamka na mafua mepesi yamekukamata,
Mwanaume kuwa msafi kupitiliza gheto kwake,me wa namna hyo umtilie mashaka kidogo.
maana huenda ana shida flan aisee.
Hongera ww ni mwanaume wa kweli.
Hujatutia aibu wenzio.
Duh! Yarabi tuokoe viumbe wako!!
 
Uvivu tu na uchafu, hamna lolote.
Mungu wangu! Yaani unatusemanga kaka zako bila staha!! Yaani wavivu; sisi!! Yaani yote tuyaweze, kasoro hili tu?! Halafu ngoja espy! Nilisoma siku moja kwamba kuna dogo mmoja enzi hizo kabla ya akina Nabii Mussa! Kwamba dogo alikuta mshua kapiga mbonji, huku vyombo vinaning'inia! Dogo badala ya kumfunika mshua, akawa anarushia vijiwe vidogo ili kulitungua buyu lililoshikilia chombo cha uzazi; kwa hasira; God akamlaani yule dogo na kizazi chake! Eti ndo wanasema Waafrika tunatokana na yule dogo! Hivi yule dogo hakuwa mwanaume yule?! Manake kuna laana zingine ni very special!
 
Hata Me nadhifa wapo si mavazi tu hata mazingira, kuna me fulani alimuazima mpangaji mwenzie ni ke ndoo atumie bhasi yule baada ya kuitumia ndoo akaosha akairudisha yule dada naona kitendo kile kilimgusa bhasi toka siku hiyo akawa anaosha ndoo

Sent using Jamii Forums mobile app
We bhana wee! Yaani unalinganisha usafi wa ndoo ya maji ya kuazima na ghetto! Hiyo hata mimi, naweza!
 
Nilikwambia ulipe kule niwe nafanya usafi unaniletea mambo ya haki sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
Sa' tulikubaliana wewe ulipe halafu mimi niwe nalelewa na wewe, au?! Na mimi nishakubali kulelewa! Tena jioni leo nachukua Bajaji kukufuata eneo la tukio, si utalipia?! Au nichukue teksii tu?
 
Sasa utalelewaje hata kufanya usafi hujui

Sent using Jamii Forums mobile app
Halafu we bhana kigeu geu!! Si nishasema kazi zoooooooooooooote nitafanya kasoro kudeki na kulishwa vibao!! Bhana eh, usin'tishe kama vp naweza kwenda kuuza shamba la urithi, nichukue hiyo apartment na wewe usiwe unatoa hata senti 5! Mambo ya usafi, sijui nini, namwajiri house girl! Kwanza nimeona tangazo JF la house girl mweney miaka 18, na form IV. Hapo vp?
 
Halafu we bhana kigeu geu!! Si nishasema kazi zoooooooooooooote nitafanya kasoro kudeki na kulishwa vibao!! Bhana eh, usin'tishe kama vp naweza kwenda kuuza shamba la urithi, nichukue hiyo apartment na wewe usiwe unatoa hata senti 5! Mambo ya usafi, sijui nini, namwajiri house girl! Kwanza nimeona tangazo JF la house girl mweney miaka 18, na form IV. Hapo vp?
Yaani hela ya ya kodi huna ila hela ya house girl unayo...! Nikilipa kodi mimi majukumu yote yaliyokuwa yangu unafanya wewe upo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom