Serious Note: Hivi wanawake wanatushindwa wapi ?nazungumzia usafi wa mazingira.

Serious Note: Hivi wanawake wanatushindwa wapi ?nazungumzia usafi wa mazingira.

Nimekuwa inspired baada ya kufika kwenye nyumba (soma: kabanda) moja hivi; ya hovyo hovyo tu! Kilichonifurahisha sasa! Yaani pazia la pale mlangoni nilitamani nijiviringishie; yaani saaaaaaaaaafi, utadhani katoka kulinunua Kariakoo! Niliyemwendea pale, ni mdada wa makamo na pale anaishi kwao.

Huku nikisita sita, akanikaribisha mpaka ndani! Ndo chumba chake hicho. Huko chumbani sasa; ingawaje ni chumba chenye kitanda cha kawaida lakini kimetandikwa nadhifu hadi kinatia nyege! Nilitamani nijitupie pale kitandani, lakini tunaheshimiana sana na huyu dada!

Nikakumbuka ghetto kwangu:- hili niliache kwanza kwa sababu mie ni rough tu tangia hapo! Na kama kuwa rough kunamfanya mtu asifike mbinguni, basi mie nitafanya kuisikia tu! Siku nilipokataa kujigawa bure hata kwangu mimi mwenyewe ni pale nilipotoka kwenye mihangaiko nikafikia sebuleni! Ghafla nikapata shida ya kutaka kutumia beseni! Nikahangaika kishenzi kulitafuta; hadi nje! Nikajuwa wakati natoka nililiacha nje na watu wamelilamba! Usiku naenda nalala, Hamaad! Si nalikuta kitandani!

Yaani beseni la kuoshea vyombo nililiacha kitandani!

Siku moja hivyo hivyo! Tafuta mswaki! Tafuta mswaki hadi ikabidi nikaunune mwingine! Baadae sana nauukuta kwenye jokofu!! Haraka zingine za kijinga sana!

Kwahiyo haya ya kwangu mimi tuyaache tu kwa sababu najijua mwenyewe, and I know God isn't fair at all. Haiwezekani anifanyie hivi bhana.

Turudi kwa mshikaji wangu mmoja hivi! Huyu mwana ukikutana nae mtaani unaweza kudhani anamiliki mtandao wa Dry Cleaners hapa mjini! Jamaa msafi bhana; we acha tu! Na vile jamaa jamaa ni white (though baadae nikagundua anapenda sana mafuta ya hovyo hovyo including ya kufanya nywele ziwe curled), lazima uamini akifika Kino, anaingia kwenye Dry Cleaner yake na kubadili, na akifika Mwenge, zile za Kino anapiga chini anapiga zingine!

Jamaa ni smart kwa 105%!

Rudi ghetto kwake sasa! Kudadadeki! Si kwa mara ya kwanza nafika ghetto kwake sikuamini kwamba yule mshikaji ndie huyu! Jamaa ni rough kuanzia mlango wa kuingilia sebuleni hadi chumbani! Huwezi amini, hiyo siku nilikuta kondom zilizotumika hapo hapo sebuleni! Yaani kaleta demu, lakini wakaamua kulala sebuleni na wakafanya yao hapo hapo!

Huo mshuka sasa!!

Na wala usidhani nilienda asubuhi sana!!!

Walioweka Grade ya A na A+ wala hawakukosea! Mi najua ni rough kiwango cha A lakini kuniweka pamoja na huyu mwana, itakuwa ni kunionea! Huyu hata A+ ni kumshusha bali ilitakiwa A++ kabisa!!

Halafu kuna huyu mdogo wangu; mdogo wangu kabisa toka nitoke!!

Dogo anajua kuvaa huyu!! Halafu hata akichukua mtumba wa jero lazima dogo utamtoa fresh tu!! Nadhani wakina mama wapenda viben10 watapata taabu sana kwa huyu dogo!

Huyu msen'ge na mwenyewe ukikutana nae mitaa ya Posta unaweza kudhani ni "Teller" pale BoT jinsi anavyokuwa smart!

Mara nyingi nilikuwa nikifika home kwetu huwa naishia sebuleni hadi naondoka!! Sasa siku moja nikaa pale hadi usiku sana kwahiyo nikaamua nilale tu! Sikupata shaka, kwa jinsi dogo alivyo nadhifu; nikatimba room kwake moja kwa moja nikitarajia nikalale huko!!

Sitaki maswali kwanini niliamua kumwachia chumba chake na kurudi kulala kwenye makochi sebuleni!!

Mimi bhana ni rough kweli kweli lakini cha ajabu nataka nikienda kwa mwenzangu nikute nadhifu na kama kulala basi pawe nadhifu ingawaje kwangu hakupo hivyo!

Si Wahenga walishasema kwamba Kila Kitanda na Kunguni Wake, au?! Wa kitandani kwangu nadhani huwa wananionea aibu bhana, kwahiyo huwa wananisubiri hadi nilale fofofo ndipo wanaanza ndipo waanze kufyonya nutrients!

Si unajua tena Zimwi Likujualo Halikuli Likakwisha!!

Halafu nimemkumbuka mshikaji mmoja hivi ambae tulikuwa tunaishi nyumba moja huku yeye akiwa mwanafunzi wa chuo fulani! Yule dogo f'ala sana; yaani wala hafahamu shuka zinazotufaa watu kama sisi!! Dogo kuna siku kaanika mashuka yake, duh! Nikajiuliza sasa kama hapa dogo ndo kayapiga na ma-OMO au na ma-FOMA, yalikuwa katika hali gani kabla ya hilo zoezi!!

Ukweli mchungu ni kwamba, majority ya sisi wanaume tunakuwa rough sana kwenye magheto yetu!! Na linapokuja suala la mashuka, ndo balaa tupu!!! Demu usiende ghetto kwa mshikaji ukakuta kitanda kama cha Guest House ukadhani daily mchizi ndo anakua hivyo! Lazima jamaa atakuwa na shuka moja au mawili kwa ajili ya show huyo!!! Siku muibukie ghetto bila taarifa kama hujakuta anafungua mlango nusu nusu huku mwenyewe kabana mlangoni ili kama anayegonga ni unauthorized person basi aishie hapo hapo mlangoni!!

Msitake kutuletea umbeya wenu hapa, ebo!!

Mi ndo nimeanzisha mtindo wa kuweka fagio standby! Nikisikia "ngo ngo ngo", yaani mtu anakuja bila taarifa, fasta nakimbilia fagio langu na kulishika mkononi ndipo nafungua eti nijfanye hii shakala baghala anayoiona ni kwavile nafanya usafi!

Yaani bora mtu utupiwe Jini Mahaba utajua unakula bila kuhudumia kuliko majini mengine haya!!

Sasa swali langu ndo lile lile! Hivi nyie wanawake mnafanya fanya vipi?! Hebu nipeni siri yenu ili na mimi nijaribu manake kila ninapojaribu, wapi!! Seriously, naomba training ya "How to Keep Your Ghetto Clean and Organized 24/7!"
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inategemea na malezi aliyokupa aliyekulea,, asilimia kubwa watoto kiume african tunalelewa kimfumo dume,, tukiwa wadogo tulikalilishwa kuwa kuosha vyombo, kudeki , kupika tuwaachia dada zetu,, hapa ndipo mchawi wetu alipo,, hadi unafika umri flani ndo unaanza kukaa ghetto,, unapewa chumba na mzee wako pale home,, unaishia kubandika mipicha ya wasanii ukutani, kufua neti hadi ibadilike rangi hahaha,, kudeki kwenyewe ni pale itokee panya amekufa,, ila chumba cha dada yako kipo smart,,

Pamaja na hayo ukijielewa unabadilika na mambo yanaenda tuu,,

Hakikisha mtoto wa kiume umekosa sana basi angalau uwe na shuka 4, pazia za kubadirisha kadhaa, perfyum kadhaa hata shellis, soksi pea 7, boxa 10, vest 10, mengine ongezea mzee baba,,

Mimi mtoto tepetepe akiingia gheto najua lazima atanizulumu boxa, perfyum, n.k



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu utasikia nataka mwanamke msafi...huyo mwanamke msafi ataenda kwa msafi mwenzie


Hakuna ugumu mkuu tatizo ni uvivu tu hebu jaribu kuacha uvivu utaweza tu. Mbona mengine hamuoni uvivu? Halafu acheni kuona kama uchafu kwa mwanaume ni sifa! Kuna wanaume utasikia mwanaume unatandika kitanda ili iweje? Mwanaume unafua socks ili iweje? Mwanaume unaosha vyombo ili iweje? Hizo ni kazi za wanawake bhana! Hivi uchafu ni sifa? Mkiacha hili mtaweza pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inategemea na malezi aliyokupa aliyekulea,, asilimia kubwa watoto kiume african tunalelewa kimfumo dume,, tukiwa wadogo tulikalilishwa kuwa kuosha vyombo, kudeki , kupika tuwaachia dada zetu,, hapa ndipo mchawi wetu alipo,, hadi unafika umri flani ndo unaanza kukaa ghetto,, unapewa chumba na mzee wako pale home,, unaishia kubandika mipicha ya wasanii ukutani,
Hii wala sio an African thing! Kwenye familia za Kiafrika, kupika kupo exclussively kwa wanawake! Hata kama wanawake ndio hao hao na issue za kuosha vyombo, lakini suala la kuosha vyombo hata watoto wa kiume huwa wanafanya hata kama sio kwa kiwango kikubwa!

Tukirudi mtaani, wanaume hawaoni taabu kupika; shughuli ile ile ambayo makuzi yake ilikuwa ni ya wanawake! Lakini linapokuja suala la vyombo ambalo hata watoto wa kiume hushiriki; tatizo! WHY?!

Huyu mtu haoni taabu kufua na kunyoosha vizuri nguo zake, ambazo huenda wakati yupo mdogo alikuwa anafuliwa na dada zake au mfanyakazi! Lakini linapokuja suala la kufua taulo tu, balaa tupu (sipendi kuwa na taulo kwa sababu najua nitaishia kulitupa tu)!
 
Halafu utasikia nataka mwanamke msafi...
NDIYOOOO! Kumbe ulitakaje?! Sasa na miuchafu uchafu yako ulitarajia uende nyumba ya nani!!!!
huyo mwanamke msafi ataenda kwa msafi mwenzie...
Watch out, n'shasema watu wanakuwa na zana za emergency!
Hakuna ugumu mkuu tatizo ni uvivu tu hebu jaribu kuacha uvivu utaweza tu. Mbona mengine hamuoni uvivu?
Hapo ndipo unatakiwa ujiulize! Hivi mtu anayevunja mawe, kuzama migodini, kufanya kila aina ya kazi za shuruba ndo aone uvivu kupangalia ghetto?! There's something more than uvivu; and that's what am trying to find out!!
Halafu acheni kuona kama uchafu kwa mwanaume ni sifa!
Sijawahi kusikia kuna mwanaume anaona sifa kwa hilo suala, na ndio maana:-
Wachafu nyie khaaaa!!!!!

Hebu nitoe mashuka na boxa huku uvunguni maana nlishasahau kbs..

SIPENDI UCHAFU MIE!
Mwana hapo anaamua kuyaweka madini uvunguni! Angeona sifa, angeyaacha tu yawe maonesho!!!!!
Kuna wanaume utasikia mwanaume unatandika kitanda ili iweje? Mwanaume unafua socks ili iweje? Mwanaume unaosha vyombo ili iweje? Hizo ni kazi za wanawake bhana! Hivi uchafu ni sifa? Mkiacha hili mtaweza pia
JF ni zaidi ya uijuavyo! Kwa ufupi, ni wanogesha genge tu hao! Wanakerwa na urafu wao lakini wanashindwa kuona msingi wa tatizo!!! Atasemaje kazi za mwanamke wakati ghetto yupo peke yake?!
 
Samahani mkuu huyo ni wewe kwa avatar.?
mbona kawaida hata hatushangaani ila nakushangaa wewe unashangaa au we mgeni wa kiumeni naona kama umekabidhiwa uume siku hizi za karibuni [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

mi kweli gheto si mpangiliaji kwa kulitambua ilo tangu hata nilipokua kwa wazazi mama alikua hanishangai maana baba nae alikua ivi ivo

gheto kwangu mi ni kitanda mashuka mepesi kwa kufua, masofa mepesi kwa kusafisha si vitambaa



Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Unknown device
 
Back
Top Bottom